Mara malkia akaita, "Masudi! Njoo!" Hapo pandikizi la mtumwa likatokea ambalo, mara lilipofika, likamkumbatia malkia na kufanya naye mapenzi pale bustanini!
Wale watumwa nao hali kadhalika wakawa wanazini na wale wajakazi. Wakaendelea na mapenzi yao mpaka kulipoanza kuchwa na wakati wa Sultani kurejea mawindoni ulipokaribia.
Shahzaman alipoona vile, akafiri: "Wallahi mkasa ulionipata mimi si mkubwa kama huu ninaoushuhudia hapa!" Hapo ile huzuni aliyokuwa nayo ikamtoka, akaanza kula na kunywa, kwani toka alipowasili kwa kaka yake chakula kilikuwa hakimshuki rohoni.
Sultan Shahriyar aliporejea, akashangaa sana kumwona nduguye kabadilika na yumo katika hali nyingine.
"Imekuwaje, ndugu yangu," akauliza Shahriyar, "kuwa nilipoondoka ulikuwa dhaifu uliyepauka na sasa unaonekana mwenye siha na mabadiliko hivi?"
"Mintaarafu ya siha na unyonge wangu," akajibu Shahzaman, "nitakusimulia sababu lakini sithubutu kukufunulia sababu zilizoleta mabadiliko hayo. Lakini jua kuwa, baada ya kupokea mwaliko wako, nikaanza safari ya kuja huku. Kwa kuwa nilisahau ile lulu ya thamni kuu niliyokupa zawadi, ikanibidi nirejee nyumbani nikaichukue. Nilipoingia ndani, nikamkuta mke wangu amekumbatiwa na mmoja wa watumwa wangu wamelala kwenye sofa wakifanya mapeni! Unaweza kukisia jinsi nilivyohisi! Ghadhabu zilizonipanda zilinifanya niwaue wote wawili papo hapo.
Endeleya!
Copyright © 2001 2002 Mombasa Web, Inc. All rights reserved..