Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

Aliporejea kwenye kambi, akaamuru msafara ung´oke waendelee. Akaendelea na safari yake kwa huzuni na majonzi mengi mpaka akafika mji mkuu wa kaka yake.

Sultan Shahriyar aliposikia mdogo wake anawasili, akatoka kwenda kumlaki kwa furaha na shangwe astahiliyo Sultani. Akamkumbatia na kumkaribisha jijini mwake lililojiandaa kumpokea.

Lakini wakati Sultan Shahriyar alipokuwa akimfurahisha na kumtumbuiza mdogo wake, Sultan Shahzaman akawa mawazo yake yote yako kwa yule mkewe na vile vitendo vyake vya ufisadi alivyokuwa akivifanya pale sofani.

Ijapokuwa alikuwa na huzuni na majonzi, hakuna yeyote aliyejua wala aliyemweleza mkasa ule. Lakini Sultan Shahriyar alitambua kuwa kuna lililokuwa likimkera mdogo wake lakini hakutaka kuuliza.

Alifikiri labda ni mambo ya utawala wa nchi au kuondoka kwake ndiko kulikokuwa kukimtia wasiwasi. Basi baada ya siku chache walakini, Sultan Shahriyar akaona ni kheri amwalike mdogo wake waende wakawinde ili apate kumwondoa mawazo. Lakini Shahzaman akajibu kuwa anaumwa na hawezi kwenda kuwinda. Hapo Sultan Shahriyar akaenda peke yake.

Wakati Shahzaman alipokuwa ameketi peke yake karibu na dirisha la chumba chake lilioelekea bustanini huku akiwaza juu ya masaibu yaliyompata, mara mlango ukafunguka na wajakazi ishirini wakiongozana na watumwa ishirini wakatokea. Katikati ya wajakazi hao alikuwamo malkia, mke wa kakiye, ambaye uzuri wake ulikuwa hauna kifani. Wote wakaelekea moja kwa moja mpaka kwenye chemchemi, wakavua nguo, wakakaa chini majanini.

Endeleya!