Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]    Rudi Table

[KESI YA KHANGA - ZAITA MUZIKA]

Mama nipe nauli nikamfuate Monika eeh,
Amekimbia Zambia na treni,
Kisa cha kukimbia madeni yamemzidi eeh,
Doti kumi za khanga alizokopa hajalipa x2

Anatafutwa na polisi popote apatikane,
Na mimi rafiki yake niko nje kwa dhamana eeh,
Nililala rumande siku mbili kituoni,
Usumbufu nilioupata kwa kweli sina raha eeeh,x2

Gitaaa la nguvu kutoka kwa Kasheba.

Mahakamani wameshapanga siku ya kusikiliza,
Asipofika nitapelekwa jela kutumikia kifungo,

Ehh Monica eeeh uko wapi
Rudi mwanzo

[Dezodezo - Zaita Muzika] -  Mtukwao

Che che cheche,
Unapenda vitu vya chee,
Unapenda dezodezo ,
We bwana we yatakushinda
 
Che che cheche,
Pombe unaomba omba,
Sigara hutaki kuacha,
We bwana we umetuchosha.
  
Che che cheche,  
Kodi ya nyumba hulipi,
Maji yameshakatwa aaah,
Operesheni kata umeme inakuja
 
Kibwagizo:
 
Che che cheche,
Wewe mtoto wa kike ,
Wacha umbea mbea