Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

Mwanzo    Rudi Table

[Vigelegele - WESTERN JAZZ]

(......... )

[Roza - WESTERN JAZZ]

Ninatizama dirishani oooo

Nona ni mvua yanyesha oo

 

Hakuna kilichobakia oooo

Ila ni huzuni na uchungu ee

 

Ingawa umeondoka ee dada

Kuniacha pweke na ukiwa tele

 

Nakutafuta mpenzi unipoze moyo

Naona hakuna hakuna mtu wa kunifija

 

Mpenzi nauliza utarudi lini ee?

Mateso yanitoke nifurahi na mpenzi

 

Oo Ambroza

 

(Chorus)

Sheri rudi rudi mpenzi wa roho

Sheri rudi naomba nakufa kwa pendo

 

Rudi Mwanzo

 

[JELA YA MAPENZI - WESTERN Jazz Band]
 
Ingekuwa wenye kugombania mapenzi wana jela ya peke yao mwenzangu,
Laaabda hiyo ningeweza,
Lakini jela ya namna hiyo hapa duniani bado haijatokea ,
Ikiwa nitagombania mapenzi nikipelekwa kwa hakimu nikishindwa,
Nikiwa sina faini,
 
Nitapelekwa gerezani,
Faida gani nitapata,
Na wewe nitakukosa,
Mateso ndio yatazidi
 
 
Kibwagizo
 
Kwa hiyo mwenzangu wewe [ ooo mwenzangu]
Tangu leo ufahamu , [ooooh,oooh]
Kugombania mapenzi,
Mimi mwenzio siwezi  x2  

Rudi Mwanzo