Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]    Rudi Table

 

[JULIE - WASHIRIKA TANZANIA STARS]

 

 

Julieee, nikupe nini uridhike 

Julie cha kukupa sina 

Julie ee unihurumie maaamaaaa (x2)

 

Ufukara nilionao eeh mamaaa 

Ufukara umekuwa kashfa  

Kwa mapenzi yaaangu kwako , kwako Julie  

Nikawa radhi hata kuidhiki nafsi yangu Julie 

Na idiriki dunia nzima kunitenga 

Napenda ufahamu hivyo Julieee  

 

Lakini si wewe kipenzi 

Mwenzio nnasema, nasikitika iyoooh  

Mama aaaaa ,

Oooh mamaaaa 

Nasikitika iyooooo  

Julie eeeh Julie eeeeh   

 

Rudi mwanzo

 

 

[Nakonda - Washirika TZ Stars]

 

Mume wangu ana matatizo yananifanya nikonde,

Siku hadi siku mimi mwenzegu eeeh x2

 

 

Kibwagizo:

 

Kuniletea mke mwenzangu ndani ya nyumba,

Si jambo la kushangaza hiloooo,

Kinachoniuma moyon ni kulala sebuleni eeeh,

Mimi na watoto jama! x2

 

 

Yeye na kimada wake hunitafuta tafuta eeh,

Wanapotoka kwenda kwenye starehe zaoo x2

 

Kibwagizo:

 

Kuniletea mke mwenzangu ndani ya nyumba...

 

 

Watoto nimemzalia aaah,

Mume huyu,

Warithi wake wa kesho,

oooh mume huyu

 

Kibwagizo:

 

Kuniletea mke mwenzangu...

 

Rudi mwanzo