Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]         Table

[CHIAPO - Vijana Orchestra]

(CHIAPO utunzi ni wake Chiriku, solo likiwa chini ya Hamza Kalala, 

solo la pili chini ya Kitime, 

gitaa la kati likiwa chini yake Manitu Mussa au Baba watoto, 

kinanda kikiwa kinapapaswa na Abdul Salvador.)

 
ah chiapo
(wote)
unalotenda Chiapo
kwa kweli sio sahihi we kaka
umtendeapo wema mtoto wa kike
usijaribu ulipwe ujira wa mapenzi  
jali asante
 
mi Dora nasumbuka
napita kuhangaika huku na kule
kazi ofisini mwako zataka watu
wanizungusha Chiapo tukutane Mizengwe
wataka nini? .... sema
(rudia)
 
(wote)
tenda mema malipo kwa mungu ...... trumpets
dunia ya'mungu tena ni duara ....
leo kwangu kesho kwako ....
(rudia x 3)

 Rudi mwanzo  

[MFITINI - Vijana Orchestra]


Enyi walimwengu nambieni dawa ipi niitumie eeh,
Mfitini nimuumbue,
Kanikosanisha na majirani ehh,
Kila anionaye ananuna,
Naonekana muongo, mzandiki eeeh,
Haki nimepakwa ukungu,
Nipeni dawa jamani eeeh x2


Kibwagizo:

Nilifanya kosa mimi,
Kumkaribisha nyumbani,
Nikamfahamisha kama ndugu


Akaanza kuharibu jina langu,
[Hapa mtaani]
Akaanza kuharibu jina langu,
[Ati mimi ni kibaka]


Nilfanya kosa mimi,
Kumfahamisha kwa ndugu zangu,
Na majirani zangu


Sasa najuta mimi
[ oooh mimi]
Sasa najuta mimi,
Kwa aliyonitendea!


Sina tena thamani iiihh,
[oooh mimi]x2


Hebu niipeni dawa jamani,
Mfitini nimuumbue ,
Asizoee

Rudi mwanzo  

[Matembezi Ya Jumamosi - Vijana Orchestra]


[Mmoja]
Samahani Rafiki Kalala kwa hayo nitakayosema eee
Matembezi ya jumamosi naona hayanifai tena ee
Rafiki eee, jamani ooooo
Rafiki eee, mwenzenu oooooo

Mimi nilishazowea eee
Matembezi ya Jumamosi

(repeat)
Nitafanyaje nami ninaoa eee

(Chorus)
Nimeshituka ee nimeshituka e bwana
Nimeshituka matembezi ya Jumamosi

Naona yatanikosesha e

[Mmoja]
Nilipoamua ndoa yangu i karibu
Ilinibidi nipige moyo konde
Nipunguze maraha
Bila kufanya hivyo ee
Ndoa yangu isingefana kweli

[Wote]Nimeshituka ee...

Rudi mwanzo  

 

[Zainabu(Lumbesa) - Vijana Orchestra] 


(wote)
baba mkwe nimekuja mimi unisaidie
kunipatanisha na mke wangu
ehee zainabu ehee zainabu
ehee zainabu namshangaa
ehee hajali kitu ehe hajali kitu mama

(wote) kibwagizo
maisha sasa ni magumu
inatubidi tuyabane matumizi

(Momba)
lakini mke wangu yeye haishi kusemasema

na kudai kila siku twende kwenye starehe
lakini mke wangu haishi kununa nuna
ingawa kila jumapili tunaenda sagarumba

(wote) kibwagizo

(Nashon)
anaposema twende kula kuku wa hotelini
watoto wetu wanapiga miayo nyumbani
anasahau kama nimevuliwa madaraka
na hivi sasa mimi ni lumbesa sokoni Tandale

(wote) kibwagizo

(Nashon)
anaposema twende kula kuku wa hotelini
watoto wetu wanapiga miayo nyumbani
anasahau kwamba nimevuliwa umeneja
na hivi sasa mimi ni Lumbesa sokoni Kariakooo

(wote)kibwagizo

Rudi mwanzo  

[PENZI HALINA UMAARUFU - Vijana Orchestra]

 

(Chini yake Chiriku Hemedi wa Maneti kijana kutoka Kilosa Morogoro. Utunzi

wake Hamza Kalala wakati huo alikuwa mgambo tuu bado hakuwa Komandoo. )

Nalala siishi kuweweseka,

Kalala eehe,  Najiuliza, yalonipata mimi eeh,

Jinsi penzi lilivyogeuka,  Kalala eeeh ,

Na kuwa sumu, napata kizunguzungu eeeh


yele yele oh mama oohh Najuta oh
yele yele yeleee
nilikuwa natesa mke wangu pasipo sababu iliyonipa kichwa oo
nilimchukua maarufu
kalala eh na kumbe penzi halina umaarufu
nilimchukua maarufu
kalala eh na kumbe penzi halina umaarufu x 2

(wote)
najuta najuta oo umaarufu umeniponza x 2
mke kaondoka leo namkumbuka eee
mke kaondoka kumbe penzi halina umaarufu ahee

huyu niyeoa, sina la kusema oh x 2
mshahara nikipata
bajeti apange yeye
anajenga nyumba kwao
mimi kwangu midabwada ehhh

(rudia wote)

Rudi mwanzo  

[SHOGA KIDAWA - Vijana Orchestra]


Kabla ya kuvuka mto usitukane mamba,
Usimuudhi mchinja mbwa wazimu utakurudia,
Waswahili walisema mama, x2

Jumamosi kama ya leo hata cha kuvaa sina,
Shoga Kidawa kanipandishia na kanzu zake,

Kakasirishwa na kitendo cha kumwita mumewe mzee
OOhh masikini Zena Bali eeeh,
Ohh hata cha kutokea sina x2

Pamba, pamba moto x2  

Rudi mwanzo  

 

[ILIKUA NI LIFTI - VIJANA OCHESTRA(Hamza Kalala)]

 

Haikua jambo baya kwangu

Kwa yule kijana kumpatia lifti

 

Kama unavyohamu yapata wiki ya tatu

Gari langu lina matatizo ya kuzimikazimika ooo Mume wangu eee

 

Kutoka nyumbani Oyster Bay kufika Salender

Gari langu lilinizimikia eeee

Yule kijana alinisaidia kusu**ma Mume wangu eee ooo ooooo oooooo

 

(CHORUS)

Kilichonishangaza sio lifti Mama Watoto

Ni tabasamu na vicheko mlivyokuanavyo ndani ya gari

Nilichanganyikiwa midomo ilianza kunicheza

Mithili ya mtu aliyemeza kipande cha moto Mama watoto

 

Rudi mwanzo

 

[Stella - Vijana]

 

Hata majirani zangu niliwasikia 

Walikusifu kwa ukarimu....

Stella eee

Miezi mitatu ya majaribio Kalala kabaki ninajiuliza

Hata Mkai nikamueleza siku nitakayofika huko......

Stella eee

Eeeeee eee Mwadelwa....

Stella eeee

(Chorus)

Nikupe nini ee, nikupe nini ee, nikupe nini ee aaoo eee

Nikupe nini eee, Nasema cha kukupa sina

Iliyobaki mimi na wewe tu tuoane

 

Rudi mwanzo

[Hamida - Vijana Jazz Band(Maneti)]
 
 
Napata ugonjwa wa moyo niwapo mbali nawe
 
Naomba usiniache mama Hamida mama
 
Hebu sema nisikie, sauti yako nijue
 
Hebu sema
 
Naomba usiniache .......  

[Rudi mwanzo]

[Shoga - Vijana Orchestra]

Nimesitushwa na ujumbee,

Ulionitumia kupitia kwa jirani yetu 

Ambaye huwa anatusukaa

Umesema ukiniona ama zako ama zangu

Aaahaa ssababu eti nafuatafuata mumeo..

 

Shoga eeeeeh eeehee ukinirudi utanionea bureeee

Shoga eeeh eeeh jeuri hiyo mimi sinaaaahh x2

 

Shoga unanionea bure,(oooh jamani eeh) 

Shoga sina kosa na weweee, 

Aaah ushoga wetu ulianza tangu utotooo 

Tulichezea vifuu na sasa tuna wajukuu,

Aah sipendi matata

 

Oooh kuvunja heshimaa,

Aaaah kugombanisha watu...

Nakataa sipendi matata

Cha mtu sikitaki nakataa,

Aaah ahh sikuzoea 

Aah nakataa sipendi matata

Hata na chokochoko nakataa,

Aah naogopa ngeu ( nakataaa sipendi matata)

 

Shoga unanionea bure

 

Ohh nyodo hiyo sina,oooh nalia ooh  ooh 

Nakataa sipendi matata

Ooh jeuri hiyo sina, ooh sikuzoea ahh 

Nakataaa siipendi matata

 

Shoga unanionea bure

[Rudi mwanzo]

[VIP - Vijana Orchestra]

Ahera hakuendeki, dunia haikaliki

 nimepatwa na mfadhaiko x2

 Si maji wala soda itakayozima 

kiu yangu ila ni wewe, VIP

Baada ya kazi ngumu ya kutafuta pesa, 

na kisirani cha kufokewa na boosi,

 

Nahitaji VIP wa kunibembeleza, 

nakutaka wewe mama unibembeleze

Si kwa maneno ila kunitomasatomasa, 

kwa mikono laini yenye bangiliii,

 unipe busu mwanana na kunipumbaza weeee VIP!

 

Chorus:

Binadamu hanunuliwi kama nguo VIP,(mpeeenzi)

Ungekuwa dukani ningekununua nikuweke ndani,

Lakini nikikuchukua bila mapenzi yako

 utanitorokaaaaa

 

Nina nia ya kuwasha moto wa mapenzi kwaaakooo,

 kwa uzuri ulio nao VIP,x2

 

Natamani penzi hai, sio penzi la ndotoooni, 

tafadhali nakuomba VIP,

 tafadhali nakusihi VIPiiii,

 ili niondokane na ndoto za mapenzi!!

 

Binadamu hanunuliwi kama nguo

 

Ukinikubali ,VIP ,VIP 

mimi niko tayari , kubadili dini!

Ukinikubali , VIP ,VIP 

nitatoa mahari ya mbuzi saba,

Hata kama sina , VIP,

 nitafanyafanya mipango niwe na wewe sambamba (sambamba)x2

 

Binadamu hanunuliwi kama nguooo VIP .......

[Rudi mwanzo]

[Mwisho Wa Mwezi - Vijana]

 Mwisho wa mwezi x2 una raha mamaaaeh 

Mwisho wa mwezi ukifika una raha ya pekeex2

 Utaona watu wengi wana nyuso za furaha eee

Kwa vile wana pesa eeh pesa ehhx2

 

Ukifika mjiniii,ama kweli utashangaaa

Mmoja: (Watu wanavyopishana kutafuta mahitaji)

Wote:  (Watu wanavyopishana kutafuta mahitaji)x2

 

Utaona watu wengi wana nyuso za furaha eee     

Kwa vile wana pesa eeh pesa ehhx2

 

Wengine hotelini, wengine madukani,

Wengine kwenye mitumbaaaaaaa (ni raha tuuu)x2

 

Kwa wale wafanyakazi, kazi huenda mbio

Viwandani ofisiniiii, (ni raha tuuu)x2

 

Mwisho wa mwezi ukifika hata lugha hubadilika eeh

Habari gani hugeuka kuwa How are you   

Hakuna taabu hugeuka kuwa No sweat    

Samahani wanasema sorry oooh sorry    

 

Mwisho wa mwezi una mambo, 

ooh ama kweli ni furaha tu ( ni furaha tu)     

 

Mwisho wa mwezi ukifikaaa, ukifika eeehh

Abiria chunga mzigo wako kaakaaa

Mwananyamala Posta eeeh

Manzese Kariakoo

Tandika Shule ya Uhuru mama 

Ogopa kanya boyaa

 

Mwisho wa mwezi una mambo eeeeh, 

ama kweli ni furaha tu ( ni ruraha tu)x2     

[Rudi mwanzo]

[JIKO LIMENUNA - Vijana Orchestra]

 

[Wote]

shemeji nisaidie

mume wangu haonekani

toka jana hatujakula ah chakula

kwani jiko limenuna

watoto wanalia njaa

kwa uchungu nami hulia eh

nikifikiri sina pesa oh pesa kwani jiko limenuna eh

 

[Chiriku Maneti]

peleka barua yako nyumbani waelezee wazazi wako oh

oh naona imani

oh naona huruma

ndio maana jana tulipokutana

nilikusabahi

 

[Wote]

ukaninyamazia shemeji eh

ni afadhali ya mdogo kulikoni huyu mkubwa eh

hakawii kuniuliza wapi baba

mama mimi naona njaa

mama mimi ataka pipi

mama mimi ataka soda 

nikifikiri sina pesa oh pesa kwani jiko limenuna eh

 

(solo ya Hamza Kalala)

 

[Wote] kibwagizo

Kama ni kuolewa mambo yenyewe ni hivyoo

ubora nirudishe kwetu 

kwa baba yangu na mama yangu

nikatulie mimi

 

[Maneti]

matatizo mengine kusema kweli unaweza kulia jama

inakuwaje mume wangu leo analala nje jama

 

[Wote] kibwagizo

 

[Maneti]

kama ningelikuwa na hasira mimi ningejinyonga

lakini moyo wangu wote mimi kwa watoto jamaa

[Rudi mwanzo]

[Sema Roho Itulizane - Vijana Orchestra]

Unikubali eeeeh eeeh 

Unikubali eeeh mama,

 

Ninachokitaka kwako wewe

Ni kauli yako tuu

Sema roho itulizane

Hata kama hunipendi, bora kunidanganya

Ili roho itulie

(Chorus)

Nifahamishe mama eeeh,

Kauli yako ni ipi eeeh,

Mawazo yako niyajuee,

Isinipate taabu kwa ajili yako wewe!!

[Rudi mwanzo]

 

[Mary Maria - Vijana Orchestra]
 
  Maneti : [Mary !!! Maria!!Angalia ninavyoteseka juu yako Maria,
Wala usingizi sipati juu yako Maria, wasililize awamu ya pili wanavyolia juu yako Maria]
 
 
Kwa kweli sasa nimenaswa
Sina ujanja eeeh eeeh,
Sina ujanja eehhh
Kupenda sawa na ajali
Haina kinga eeh eeh
Haina kinga eeh
 
Nilivyomuhusudu mtoto Mary sijapata kupenda toka nizaliweeeee
Na wala sitapenda mpaka nife,
Mpaka nife, mama Mary eeeh
 
Nasononeka oooh mama, nasononeka,
Ninateseka ooh mama, ninateseka,
Aaaah nimezama kwenye dimbwi  
Oooh la mapenzi x2
 
Aiya yaya Maria wangu ( Maria wangu)
Aiya yaya Maria ooooh Maria (I love you)
 
Ni wewe Maria, Maria wangu
Ni wewe wa kufa na kuzikana eeeh
Hakuna mwingine zaidi yako
 
Angalia penzi langu kwakoooo
Nitakuwa wa milele Manetiiii
Nakuomba ulitunze penziiiii
 
Ni  wewe Maria , Maria wangu ayaya  
 
Aya yaya Maria
 
Awamu ya pili, pamba moto!
 
Rudi mwanzo  

 

[PENZI HALIGAWANYIKI II - Vijana Orchestra]

 Chorus)

[Wote]

Vipi  sasa we bwana waleta matata

Kwa vile napendeza na nimetakata x2

Kila nikipita macho yakutoka

Utadhani balbu..bwana we bwana e

Kila nikipita wageuza shingo

Utadhani Feni ..bwana e bwana e

[Kida Waziri]

Kumbuka mateso ulonipa

Kulala na njaa na watoto

Maudhi yako siwezi sahau bwana eeh

Mateso yako siwezi sahau bwana eeh

Aiyo siwezi tena/(bwana) aiyo ee

Aiyo ninae wangu, aiyooo

Aiyoo sirudi tena aiyooo eeeh ...samahani kaka

[Wote]  

Hivi sasa we bwana waleta matata.....

Rudi mwanzo

 

[Aza - Vijana Orchestra]

[Maneti]

Aza eeeh , umelikatili pendo laaangu,

 

[Wote]

 Aza, Aza mbona nilikwisha kuahidi

 

[Maneti]

Ahadi ya kwetu, ahadi ya ndoa 

Vipi sasa , Aza eeeeeeeh

 

Mama yoyoyoyo,

Sheri wangu Aza eeh 

Mama yoyoyoyo,

Aza mela naumia.

 

[Maneti]barua yako Aza eh 

[Wote]ilinishangaza hasa ulipoeleza unavunja mipango ya ndoa

[Maneti]lakini Aza ni kipii 

[Wote]kilichokusibu hadi Aza ugeuke na kumbe tulishapanga

 

[Wote]

Ningelikwisha oa, toka siku za nyuma

Lakini ilibidi 

Nisubiri ahadi

Umalizie kozi ya masomo Tabora

 

 

(Kibwagizo) 

 

[Wote]

Aza eeeeh Aza maamaaa

Umenipa aibu kwa ndugu na jamaa zangu Aza

 

[Maneti]

Matarajio yangu Aza ni kuishi pamoja

Vipi leo Aza umenigeuka

 

[Wote]kibwagizo

 

[Maneti]

Aza wangu mama eh umenishangaza Aza 

Vipi leo mama eh umenigeuka

 

Aza eeeh Aza maamaa.....

[Rudi mwanzo]

 

[THEREZA – Vijana Orchestra]

Aibu, aibu ,aibu , 

Umenipa, umenipa aaaah mamaa

 

aibu, aibu, aibu,

umenipa, umenipa, aaahh Thereza

 

[Nashon]

Umenikataa siku ya harusi mbele ya kasisi bibii

Umenikimbia mbele ya wazazi na rafiki zangu Thereza ah

 

[Wote]

nasema kwa heri kwa uchungu 

moyo wangu unawaka ahh mamaaa

 

[Nashon]

Umenambia unaye mwingine wa kukuliwaza na kukupumbaza bibiii

Hiyo pete yangu usiirudishe ni uthibitisho

Wa penzi langu kwako 

 

Vyombo

 

[Wote]kibwagizo

Najiuliza kila mara na kujuta moyoni

Ni penzi gani analokupa huyooo

Ni dawa gani aliyokunywesha 

Ukachanganyikiwa na kuisahau 

Sura yangu siku ya harusi x2

 

[Nashon]

Thereza ... Thereza

penzi gani anolokupa wewe Thereza

nami pia nitakupa Thereza

akikupa busu la shavu mpenzi Thereza oh

nitakupa la kinywani ohh Thereza

bibiii ohh mamaaa

 

[Wote]kibwagizo

 

[Nashon]

Thereza ... Thereza

chakula gani anachokupa mpenzi Thereza

nami pia nitakupa Thereza

akikupa wali na sombe mpenzi Thereza oh

nitakupa wali na pondo Thereza

bibiii mamaa

 

[Wote]kibwagizo

 

[Benjamini]

Bibiii ni mji gani hujafika weweeee

Hoteli gani hujalala mama

basi sema na lipi unataka ili nielewe uniponye roho yaangu

 

[Wote]kibwagizo

 

[Benja]

bibii ni nguo gani hujavaa weweeee

Kinywaji gani hujakunywa mama 

Basi sema raha ipi unataka ili nielewe niipoze roho yaaangu

 

[Wote]kibwagizo

 

[Nashon]

Thereza .... Thereza

penzi gani analokupa huyo kijana

nami pia nitakupaa Thereza

Kama pochi nami ninalo mpenzi Thereza

Sema nitakukatia .. Thereza

bibiii ahhh mamaa

 

[wote]kibwagizo

[Rudi mwanzo]

 

[Matapeli - Vijana Orchestra]

(Chorus)

[Wote]

Bwana Mangushi nakupa pole kaka

Watu hao ni walaghai....walaghai

Wanaitwa MATAPELI eee

EE Wanaitwa Tapeli kaka

 

[Mmoja]

Watu hao wameenea sana, kila pembe hapa mjini

Kazi yao kuibia watu jina lao MATAPELI

 

[Wote]  

Bwana Mangushi nakupa pole...

Rudi Mwanzo

[Vicky – Vijana Orchestra]

Vick nakuona bado umekasirika,japo maelezo nimekwambia

Wewe usifuate mambo wanayokwambia,

Mimi si muhuni Vicky watakupoteeza!

 

Ni aibu kubwa Vicky tukitengana,

Na hata wazazi wetu watashangaa,

Wao wanajua sisi tutaoana,

Sasa ndio vipi Vicky tukitengaaana!

 

Kibwagizo:

 

Mateso nitapata,Vicky eeeh ,

Mafikara mengi Vicky hayatakwisha ,(mi nnasema) x2

 

Japokuwa duniani..........

Kwa uchungu na mawazo usingizi sitopata.

 

Kibwagizo:

Mateso…………  

Rudi Mwanzo

 

[TANGA -  Vijana Orchestra]

 

Tanga eeeh

Tanga eeeh 

Tanzaniaaaaa

 

Tanga eeeh mji wa pili kwa ukubwa,

Mkoa unaopendeza na wenyeji wastaarabu sana,

Mji unaopendeza na wenyeji wastaarabu sana,

Tanga oooh , Tanga x2

 

 

Kibwagizo.

 

Nauliza kwenu wenyeji jambo moja,

Neno la Tanga maaana yake iko wapi,

Tanga ni la msiba , au kutangatanga,

Kuuliza sio ujinga jama ndugu zangueeeeh,

 

Dar es salama ni bandari ya salama,

Neno Tanga maaana iko wapi?,

Tanga iko wapi jamaaaa?

 

 

Kibwagizo:

 

Nauliza kwenu wenyeji jambo moja........ 

[Rudi mwanzo]

[PENZI HALIGAWANYIKI I -  Vijana Orchestra]

 

[Kida Waziri]

Oooh naamini eeeh  

Methali za wahengaaaaa  

Dunia hiiii, vyote vinagawanyika  

 

Mali na shamba pia vinagawanyika   

Aaaah aaaah sio penzi jamani  

Utafanya kila njia upande mmoja litazidi (x2)  

Oooh mume wangu eeee  

 

Ulinitaka radhi eeeh  

Wataka oa mke mwingine wa pili  

Uwezo huoo wa kukutunza hunao   

 

Aaaah aaah matokeo ya penzi  

Limezidi elemea kwa mke mwenzangu eeeh (x2)  

Nakuomba sana mume wangueeeeee  

Nikumbuke japo na watoto (x2)  

 

Hunijali kwa chumvi  (hunijali kwa sukari taabu nyingi ninapata na watotoooo) 

  Hunijali kwa mavazi  (hunijali kwa maradhi kweli penzi haliwezi gawanyika eeeeeh)

 Pamba , pamba moto, awamu ya pili shambuliaaaaa  

 

Rudi mwanzo  

 

[AMBA - Vijana Orchestra]
 
Maisha ya Amba eeeh,
Na taaabu za dunia Amba eeh,
Kaishi kwa taabu Amba eeh,
Kasoma kwa taabu Amba eeh Amba eeex2
 
Baba na mama yake Amba,
Uwezo ulikuwa mdogoo,
Ndio ilimfanya Amba,
Asimalize masomo aanze kuhangaika,
Na kutafuta kazi ee h Amba eehx2
  
Kibwagizo;
 
Mungu ni Mungu , wala  Mungu jamani si Athumani eeh,
Na taabu zote, alopata Amba kafanikiwa eeh,
 
 
Amba emepata kazi eeh,
Amba kawa baharia,
Amba kajenga na nyumba kwaaaoo!x2

[Rudi mwanzo]

 

[Wivu - Vijana(Hemedi Maneti)]

 Wivu eee, wivu ni ugonjwa jamani , wivu juu ya mume wangu unaniua!

Wivu eee , wivu ni ugonjwa jamani , wivu juu ya mume wangu utanikondesha aaaah, 

Hospitali ya wivu sijaijua aaa jamani ningekwenda siku moja nikatibiweee

Wasinisemeseme wenzanguuu eeeh mamaaa ,

Wananisengenya wenzanguuuu bibiee naona haya mama!

Hata saa zako za kurudi kazini hazieleweki mume wangu eeeeh 

Mara saa kumi, mara saa mbili usiku nikueleweje 

Unanipa wasiwasi mume wangu eeeh ninakonda!!

 

[Maneti]

Penzi lako linataka ati nishinde ndani tu mama, 

Tutakula niniiii, mamama, tutavaa nini bibiiiii

Aeee mimi , mimi eee niseme nini mama x2 

Jambo moja nawaomba ngoja niseme 

Acheni nifanye wivu kwa wangu kipenzi 

Bila wivu atajuaje kama kwelli nampenda oooh

 

Hata nikienda kazini unaona wivuuu mama, unaona donge maaaax2

(rudia chorus)

[Rudi mwanzo]

[ Mama Chichi - Vijana Orchestra] 

 

Mara nyingi duniani mtu hukisifu kilicho chake,

Ni vizuri duniani mtu kukisifu anachopenda,

 

 

Kwa hiyo na mimi aaah,

Kwako Diana,

Sina budi kufanya hivyo 

 

OOOhhh kwa vile unatimiza,

Yale yote ambayo anayostahili 

Kuyatenda mke wa mtu!

 

Aiyolele iyo,

Mama Chichi yoyo,

Aiyolele iyo,

Mama Chichi mama x2

 

Barafu wa moyo wangu Mama Chichi,

Mwenye mapenzi yaki Pangani Mama Chichi,

Yanayofanana na yale ya njiwa Manga tunduni,

Sikiliza maneno yangu ,

Mama Chichi mama

 

Aiyo lele iyo ,

Mama Chichi maama x2

 

Sura za binaadamu ni kutopenda maendeleo ya wengine

(Kama kiwangawanga)

Kwa hiyo sisi tupendane mapenzi ya njiwa,

Kwani upendo na uaminifu ndio heshima ya ndoax2

 

Aiyo lele iyo... 

 

[Pambamoto - Vijana Orchestra] - tizedboy

Kuna wala kushinda ee
Una kushinda Igoma eee
igoma ya kumwitue eee
 
Pambamoto
Awamu ya pili
 
[Mmmoja]
Nakula fusali sili usali
Tusindzage manya ya musua ee
Elambo ya Malaika  e Mungu
Atulize mizimu yote ee

 

 

[BUJUMBURA - Vijana Orchestra] - Uzegeni
 
Bujumbura ia Burundi ehh  
Bujumbura mama ehh  
Bujumbura ia Africa
Bujumbura mama ehh
 
iyele iyele iyele Bujumbura
 
(Maneti)
tumefikaa Bujumburaa ehh  
tumepokelewa kwa shangwe
kina mama walifunga vibwebwe
asiye mwana alibeba jiwe
Bujumbura iliwaka moto eh  
pambamoto iliwasha moto ehh  
 
tumefikaaa Bujumbura ehh  
tumepokelewa na wana Shani
kina mama walifunga vibwebwe  
Bujumbura iliwaka moto ehh  
pambamoto iliwasha moto eh  
 
iyele iyele iyele Bujumbura
 
Buja ................ Buja ............ Buja

 

 

[MAMA WA KAMBO - Vijana Orchestra] - MWANAMALUNDI

(.......)
wengi wao husema, eti mama wa kambo si mama iyooo

hiyo si kweli mimi si amini eeeeeh

mama wa kambo ni sawa ni wengine eeehh
 
ukisema hivyo mimi ndiye aliyenilea eeeeh

kanisomesha mpaka nimemaliza eeeh

chuo kikuu nimefikia eeeh
 
Nilichogundua vijana wengi hukosa adabu iyoooo

akishajua huyu si mama yangu eeeeh

humdharau na kumsimanga eeeeeeh

ndipo mateso yanapoanza hiyooooooo
 
HEMEDI MANETI:

 NATOA WITO KWA VIJANA WENZANGU

TUSIWADHARAU MAMA ZETU WA KAMBO

KWANI KUFANYA NI HIVYO NI SAWA NI KUMDHARAU..................

 

[Mwenge Ndio Tochi Yetu - Vijana Orchestra] - Mtukwao

 

Mwenge ndio tochi yetu,
Itakayowamulika,
Wasaliti wa ujamaa

Wasaliti wa viongozi na chama chetu cha mapinduzi!
 
Wana CCM wote,[hongeraaaa]
Sasa tufungue macho [hongeraaa]
Kama nyuma tulilaala,
Mbele tusilale tena,jamaa
 
Kama nyuma tulilala, mbele tusilale tena,
OOooh tusilale tena,
 
Marehemuuu Karume,
Marehemu Dr. Cleruuu,
Waliowapoteza,ni ndugu zetu hawa watanzania tuonaowafahamu
 
[Hapa anaingia Maneti kama sikosei]
Kama nyuma tulilala
 
[Wote]
Mbele tusilale tena
 
[Maneti]
Oo tusilale tena
 
[Wote]
Mwenge ndio Tochi yetu..........

 

 

[TWALALAMIKA PEMBENI - Vijana Orchestra] - Mtukwao
 
Twalalamika pembeni,
Hatupewi madaraka,
Na huku nyuma nyuma twajiweka,
Tutamuongoza nani eeeh x2
 
Twalalamika pembeni,
Hatupewi madaraka,
Na huku nyuma nyuma twajiweka,
Madaraka atawapa nani eehx2
 
Kibwagizo:
 
Jukumu letu sasa vijanaaaaaaah,
Tukiongoze chamaaaaax2
 
SIjui ni mwaka gani unyonge utatutoka,
Vijana ni zamu yetu, chama tukiimarishe,
Tushiriki kwenye chama,
Tuoneshe nia zetu,
Kwa muongozo wa chaaaamaaa eeeeh
 
Jukumu letu sasa v ijanaaaaaah
TUkiongoze chamaaaaax2