Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]        Rudi Table

 

 

[Nachunga Heshima - UDA]

 

[Wote]

Tulizaliwa wote kijiji kimoja

Lakini ulishindwa kunioa kwa sababu , ulisema sina tabia nzuri e

 

Sasa nimeolewa kaka, unaanza kuleta maneno na chokochoko

Kujifanya wewe unazo PESA nyingi, univurugie

 

Wenyewe tumetulia, Kama ni tabu zetu

Kama raha ni matokeo

Kama unachoringia ni pesa kaka, pesa si msingi

 

(Chorus)

 

[Wote]Ninachojali kujani ni utu pia na heshima kwa mume wangu

[Mmoja]Kama unachoringia ni pesa ee mimi sina haja nazo

[Wote]Ninachojali  ni utu pia na heshima kwa mume wangu

[Mmoja]Usifikiri nimeshasahau wewe kashfa na vitendo vyako kaka eee

[Wote]Ninachojali  ni utu pia na heshima kwa mume wangu.......

(Bayankta....Baynkata...Ndio yenyewe eeee)

[Rudi mwanzo]

 

[Nenda Ukaishi Salama - UDA Jazz Band]

 

Umekumbwa na kitu gani kipenzi changu nashangaa 

Matatizo yako ni nini kufanya jambo la karaha

 

Hebu nieleze kosa langu,  Lililovunja mapenzi yetu

Ukaondoka bila kuaga,  

 

Wanishangaza we mke wangu ahaaaaa(x2)   

 

Kuondoka kwako mke wangu Suzy kulinipa kichaa

Na huyo bwana uliyenaye, mimi sisemi nashangaaa

 

Nilikueleza toka mwanzo,  Huyo kijana ni rafiki yangu

Wamtambua toka zamani ,  Iweje sasa ni bwana wako aahaaa(x2)  

 

(Chorus)

 

[Wote]

Nenda ukaishi salama (Suzy) 

Nenda ukaishi salama ( huko uendako)  

 

[Ubao]

Kuna methali  inayosema,  Mtenda mema hulipwa mema

Kwa hayo yote uliyofanya,  Nakutakia maisha memaaaa.....Suzana, 

 

[Wote]

Nenda ukaishi salama (Suzy) 

Nenda ukaishi salama ( huko uendako)  

 

[Ubao]

Pamoja na kuyafanya hayo,  Na rafiki yangu nakueleza, 

Aliyefanya mipango hiyo,  Unitoroke namuelewaaaa,   Suzana,

 

[Wote]

Nenda ukaishi salama (Suzy) 

Nenda ukaishi salama ( huko uendako)  

 

Rudi mwanzo

 

[Talaka Ya Makosa - UDA Jazz Band]

 

[Wote]

Ukifikiri sana mimi sina makosa

Mimi nilishakueleza hao si watu wema

Nawe hukusikia mume...sasa ona tumeachana

 

Ushabiki wao....na uongo wao....sasa umevunja unyumba  wetu

Na heshima imepungua.....!

 

Nilifanya makosa kwa kweli mke wangu

Sikutaka kuyachunguza nakuomba turudiane

(Uaaaa)

 

(Chorus)

[Wote]

Makosa ni yako we Ngoya...hukuchunguza we Ngoya

Ukaamua we Ngoya...Kunipa talaka e Ngoya

Nirudi kwetu e Ngoya...Kwa baba na mama we Ngoya

Leo wataka turudiane tena heheheee

 

Mimi nimeshapata e Ngoya...Mchumba mwingine we Ngoya

Kurudiana e Ngoya...HAITAWEZEKANA e Ngoya

Ibaki heshima e Ngoya...Juu ya watoto e Ngoya

[Rudi mwanzo]

 

 

[Pesa Ni Matokeo - UDA Jazz Band] 
  
[Wote]
Ulipokuwa una pesa kijana, ulifanya mengi makubwa
Hata ndugu zako we kijana hukuwakumbuka
Sasa unatangatanga kwa shida pesa zimekwisha waona aibu
 
[Mmoja]
Na ndugu zako wanakuchukia ee.....marafiki wanakukimbia!
Pesa zako ulizoringia zimekwisha umefilisika
 
[Wote]
Ulipokuwa una pesa kijana, ulifanya mengi makubwa........... 
 
(Chorus)
 
[Wote]
Ukipata pesa kijana we....o kijana
Uwakumbuke nduguzo oo
Maisha ya anasa punguza uwatunze vema wanao oo
 
[Mmoja]
Ulipokuwa unazo pesa wewe
Pesa nyingi ulizivamia ukapoteza  heshima yako
Watangatanga kuomba chakula
 
[Wote]
Ukipata pesa kijana we....o kijana
 
[Mmoja]
Mapesa ukipata unayachezea kwa maraha mengi we kaka we
Ukafikiri oo una KISIMA cha kuzichota hizo pesa kaka
 
[Wote]
Ukipata pesa kijana we....o kijana.......

[Rudi mwanzo]