[Stendi Ya Basi - Toma Toma Orchestra]
[Wote]
Kila siku mke wangu unarudi saa za usiku
Ufikapo nyumbani macho yau yau
Nimevumilia aa sasa nimechoka
Leo nataka unieleze wapi unakochelewa
(repeat)
(Chorus)
[Wote]
Nachelewa STENDI ya basi bwana eee
Tabu ya mabasi waijua mume wangu e.....nihurumie bwana
[Mmoja]
Mbona wasichana wenzako wote wanawahi nyumbani
Sasa ni kitu gani kinachokufanyisha uchelewe eee
[Wote]
Nachelewa STENDI ya basi bwana eee......
[Mmoja]
Tabia kama hiyo mimi oo sitoipendelea
Jaribu kuwahi nyumbani eee utunze watoto wetu
[Wote]
Nachelewa STENDI ya basi bwana eee
[Mmoja]
Mume wangu USINIELEWE vibaya....ni kweli ninayosema
Jaribu kunihurumia mume wangu e
[Mmoja]
Mume wangi nakuomba eee ...oo ninasema
Jaribu kunihurumia mume wangu e
[Wote]
Nachelewa STENDI ya basi bwana eee
[Mmoja]
Nimezipata HABARI zao nasikia mke wangu eee
Ukitoka kazini unaelekea kuzurura mitaani!
[Wote]
Nachelewa STENDI ya basi bwana eee..........