[Mwanzo] Rudi Table
(Hawa ni wana Segere Matata, Tabora Jazz,wakati huo Shem Karenga na
wenziwe wakiwa wanatamba kwenye ulimwengu wa muziki)
Asha usifuate mambo ya dunia,
Majirani wasikudanganye ewe Asha,
Hata ndugu zangu wasikudanganye Asha,
Wazee wetu wamekwisha tupa uhuru Asha,
Ukitaka ndege mimi nitanunua Asha, x2
Kibwagizo:
Asha wewe, kumbuka Ashaa,
Mema mengi niliyokutendea,
Vijana wa mjini wasingekutambua mama,
Mema mengi niliyokutendea,
Kumbe wewe hukumbuki fadhila wangu,
Mema mengi niliyokutendea
[REMMY
- Tabora Jazz Band]
Aaaah, Remmy,
Uliyoyasema sasa nimekubali,
Kumbe dada Remmy hatutaaachana ,
Jiepushe walimwengu, xe
Ninashukuru kwa umefikiri,
Jambo la maana,
Sasa maisha tutayadumisha,
Daima milele Mungu atujalie x2
Kibwagizo:
Dada Remmy sasa sikiliza ooh,
Ndio bwana ndio bwana,
Tulia tuyajenge maisha ooh,
Dada Remmy dada Remmy,
Nitakufa bure juu yakooo,
Dada Remmy dada Remmy
Tulia tuyajenge maisha ooh,
Bila wasi wasi Remmy
[CHAKULA
KWA JIRANI - Tabora Jazz(Segere Matata)]
Visa
alivyotenda Wallace mama aaa aaaa
Sintovisahau
maishani mwangu
Alinihamisha
kwetu mimi aaa aaa
Aliniambia
nihame kwetu na kazi niache
Kumbe
anidanganya nihame kwetu,kisha anipe tabu mimi
Halali
nyumbani Wallace sijui yu wapi
(Chorus)
Chakula
nakula kwa jirani mimi
Mafuta
ya taa kwa jirani jama
Sabuni
naomba kwa jirani mimi
Mwishoe
jirani wamechoka jama
Wallace
kanifukuza niende kwetu
Na
kazini wamekwisha nifukuza