Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]    Rudi Table

 

[Wape Wape Vidonge Vyao - Golden Star(Tanga)]

 

[Wote]Wape wape ee vidonge vyao, wakimeza wakitema shauri yao

 

[Njemba]

Wanawake ni wajanja na uerevu wanao,

Waona baba likija wambiwa ni shemejio,

Mwalishwa sahani moja kumbe ni mume mwezio...jomba

 

[Wote]Wape wape ee vidonge vyao, wakimeza wakitema shauri yao

 

[Bibie]

Kulishwa sahani moja wewe na mume mwenzio,

Usikione kihoja dunia yetu ya leo,

Wake nasi tuna haja ya matumizi na nguo

 

[Wote]Wape wape ee vidonge vyao, wakimeza wakitema shauri yao

 

[Njemba]

Wanawake ni wajanja hakika nimekubali,

Waona baba likija limevaa suruali,

Mwalishwa sahani moja kumbe ni mume wa pili......jomba

 

[Wote]Wape wape ee vidonge vyao, wakimeza wakitema shauri yao

 

[Bibie]

Kulishwa sahani moja wewe na yule fulani,

Usikione kioja wala usione shani,

Kumbuka nasi ni tu waja tuna mengi twatamani

 

[Wote]Wape wape ee vidonge vyao, wakimeza wakitema shauri yao

 

[Njemba]

Wanawake ni wajanja na kisha wana vituko,

Waona baba likija wambiwa shemeji yako,

Mwalishwa sahani moja kumbe ni mume mwenzako...jomba

 

[Wote]Wape wape ee vidonge vyao, wakimeza wakitema shauri yao

 

[Bibie]

Japokuwa msikizi nikupe iliyo sawa,

Waume wa siku hizi yenu tunayaelewa,

Waweka mwana wa kazi ukarudi kamuowa... jama

 

[Wote]Wape wape ee vidonge vyao, wakimeza wakitema shauri yao

 

[Rudi mwanzo]

 

[Makombo - JKT Taarab]


[Njemba]

Nnapiga Kigolibo,Wenzangu nisikieni

Japo niwe na Muambo, Sina kitu mfukoni

Katu siyali MAKOMBO, Yaliyoachwa mezani

Nahofu kunuka shombo, La Makombo mdomoni

[Wote]

Naomba jihadharini nyie wapenda Makombo

Mtavunja ujirani, Kwa kugombea Makombo

Mwenzenu kawategeni, Mwisho mtaimbwa nyimbo


[Njemba]

Wengi wakila Makombo, Hujiona WAMEWINI!

Wakishajaza matumbo, Hujigamba mitaani

Husema hata Kimombo na miluzi mdomoni

Hawaelewi Makombo aliyeacha ni nani[Wote]

Naomba jihadharini nyie...........[Njemba]

Naapa sili Makombo, Yaliyoachwa mezani

Na hata yawe Makombo, Ya Gosi na Biriani

Wayapambe kwa mapambo, Kama mlo harusini

Ili mradi Makombo, Sitakula ABADANI![Wote]

Naomba jihadharini nyie...........[Njemba]

Ni heri niende Yombo, Kwa mama ntilieni

Nikae kwenye Kiwambo, Kwenye Jamvi ya chini

Nipakuliwe Kitumbo, Wali kutoka Mekoni

Kuliko kula Makombo, Yalosazwa Hotelini

[Wote]

[Rudi mwanzo]

 

[Kupeana Ni Kikoa - JKT Taarab]

[Wote]
Kiumbe wacha vioja kumkatili mwenzio, Japo kidogo si hoja umgawie mwenzio
Kitoe upate tija aaa, kama si kesho ni leo

[Bibie]
Kupeana ni kikoa wazee waliyanena, Kiumbe ukipokea kutoa usije kana
Huo kwetu ni usia aa, katuagiza RABANA!

[Wote]
Kiumbe wacha vioja kumkatili mwenzio,..........

[Bibie]
Wengi sana twawaona viumbe wenye hiyana, wana mali nyingi sana wala idadi hazina
Ukiwaomba huguna aa, pengine hukutukana!

[Wote]
Kiumbe wacha vioja kumkatili mwenzio,..........

[Bibie]
Zingine wanazonyima wala hawakununua, Shambani wamezilima pato wakajipatia
Kwa kuwa hawana wema aaa, Kutoa hukatazia

[Wote]
Kiumbe wacha vioja kumkatili mwenzio,..........

[Bibie]
Kaagiza SUBHANA si leo zamani sana, Binadamu KUPEANA ni tendo la kiungwana
Viumbe tukinyimana aaa, Tutamuudhi RABANA!

[Wote]
Kiumbe wacha vioja kumkatili mwenzio,..........

[Bibie]
Nawausia wenzangu nyie mnaonyimana kaburini kuna RUNGU, Langoja lenye wenye HIYANA!
Msipoyashika yangu uu, Wachoyo mtakiona

[Wote]
Kiumbe wacha vioja kumkatili mwenzio,..........

[Bibie]
Bahili ana hatia kesho siku ya KIAMA peponi hatoingia, Mlangoni atakwama
Atakwenda kuungua aaa, Kwa moto waa JEHANNAM'A

[Wote]
Kiumbe wacha vioja kumkatili mwenzio..........

 

[Rudi mwanzo]

 

[Jamani Mapenzi - JKT Taarab]

 

[Wote]

Jamani mapenzi, yananitatiza eeeh (x2)

Kulala siwezi, kusema siwezi  

Chakula sitaki, nakiiona sumu x2 

 

[Bibie]

Mapenzi yamenivaa, nami ugenini  

 Akili imenipaa, hata njia siioni

 

(Mapenzi yana hadaa, ya kweli nawambieni )(x2) 

 

[Wote]

Jamani mapenzi, yananitatiza eeeh......... 

 

[Bibie]

Nilikwenda kwa waganga, wanaojua mizungu (x2)

Samba angalimtwanga, ageuke nungunungu,  

(Maliwa kazibananga, nikarudi sina changu) (x2) 

 

[Wote]

Jamani mapenzi, yananitatiza eeeh......... 

 

Haiba imepotea, uzuri umenitoka,(x2)

Mali imeangamia, maradhi hayakutoka,  

Mwenzenu nimepotea, muokozi kanitoka,  

 

[Wote]

Jamani mapenzi, yananitatiza eeeh........

 

 [Bibie]

 Enyi wenye ukarimu, siri nawatobolea,(x2)

Moyo umepata sumu, madawa hayakufaa,  

(Kupenda kitu adimu, nawambia kuna baa)(x2) 

 

 

[Wote]

Jamani mapenzi, yananitatiza eeeh........

 

 [Bibie]

 Ya kweli nawambieni, myatie akilini x2 

 Msipende ugenini, mtaingia hatiani

(Mtalala majiani , wazimu tele vichwani)(x2) 

 

[Wote]

Jamani mapenzi, yananitatiza eeeh........

 

Rudi mwanzo

 

 

[Chura - JWTZ Taarab]

 

[Bibie]

Chura nakuulizia unipe jibu makini, kwa kila inyapo mvua wakimbilia bwawani

Huna nguo za kufua na wala huna sabuni, nijibu yapate tua maji utayafanyani

 

[Wote]

Chura punguza vituko na wako uhayawani, umezua sokomoko watu hawaeleni 

Ukivunjika mgongo, dawa atakupa nani?   

 

[Bibie]

Mwenzenu nilikisia ni mlinzi kisimani, mtu utamzuia maji akiyatamani

Akaja dada Rukia na ndooye mkononi, chura ukajing`atua ukajitosa pembeni

 

[Wote]

Chura punguza vituko na wako uhayawani, umezua sokomoko watu hawaeleni 

Ukivunjika mgongo, dawa atakupa nani?   

 

[Bibie]

Chura bora kuamua wende kulima shambani, mazao kujipatia wende kuuza sokoni

Nguo kujinunulia isitiri maungoni, au ukitaka ndoa nenda kaoe nyumbani.   

 

Rudi mwanzo

[Njiwa Peleka Salamu - JKT Taarab]

 

[Bibie]

Njiwa peleka salamu uuu, O kwa yule wangu muhibu

Umweleze eee afahamu uu, Kwamba nnapata tabu

Hali yangu mahamumu uu, O maradhi yamenisibu

 

Ewe Njiwa ewe Njiwa...

 

[Wote]Peleka salamu

[Bibie]Kwa yule kwa yule

[Wote]Wangu Muhibu

 

[Bibie]

Usiku kucha nakesha aaa, O na yeye ndiye sababu

Iwapo aa hajui  maisha aaa, O Itamfika aibu

Pendo langu halijesha aaa, O ndilo linoliadhibu

 

Ewe Njiwa ewe Njiwa...Peleka salamu...Kwa yule kwa yule....Wangu Muhibu

 

[Bibie]

Njiwa usihadaike eee, O nenda ulete majibu

Nenda upesi ufike eee, Mkimbilie Swahibu

Mbele yake utamke eee, O ni yeye wa kunitibu

 

Ewe Njiwa ewe Njiwa...Peleka salamu...Kwa yule kwa yule....Wangu Muhibu

 

[Bibie]

Ukifika tafadhali iii, Sema naye taratibu

Ukisema kwa ukali iii , Mambo utayaharibu

Kamwambie sina hali iii, O kufariki si ajabu

 

Ewe Njiwa ewe Njiwa...Peleka salamu...Kwa yule kwa yule....Wangu Muhibu

 

[Njemba]

Njiwa rudisha majibu uuu, Mwambie nimepokea

Kukosea ni wajibu uuu, Si mimi na yeye pia

Kwa nini ajiadhibu uuu, Afikirie yeye dunia

 

Ewe Njiwa ewe Njiwa...Peleka salamu...Kwa yule kwa yule....Wangu Muhibu

 

[Njemba]

Njiwa rudi utokako ooo, Ukanene ninenayo

Nitakuja huko huko ooo, Na sio kesho ni leo

Nije mpa BURUDIKO ooo, Utulie wake moyo

 

Ewe Njiwa ewe Njiwa...Peleka salamu...Kwa yule kwa yule....Wangu Muhibu

 

[Njemba]

Maisha yamenitinga aaa, Siogi wala silali

Hatifasi na Uganga aaa, Maisha kuyakabili

Na mimi nitajinyonga aaa, Tuzikwe wote wawili

 

Ewe Njiwa ewe Njiwa...Peleka salamu...Kwa yule kwa yule....Wangu Muhibu.......

[Rudi mwanzo]

 

 

[Sina Mimi Sina - J.K.T Kiwira Mbeya]

 

Sina mimi sina, mwingine zaidi ya wewe

Sina mimi sina, atakaye kushinda wewe

(repeat)

 

[Bibie]

Mngetulizana mliopo muelewe, nitakayonena kwa makini muyajue eeee

Nitakayonenna kwa makini muyajue, kwamba sijaona duniani mfanowe eee

 

[Wote]

Sina mimi sina, mwingine zaidi ya wewe........

 

[Bibie]

Ni yeye hakuna mimi anipendezae, wala kulingana huyo simuoni  miye eee

Wala kulingana huyo simuoni  miye, peke yake mwana mimi nimuuguwae eee

 

[Wote]

Sina mimi sina, mwingine zaidi ya wewe........

 

[Bibie]

Yeye wa daima mimi nitaishi nae, ingawa mwasema kwamba si mzuri yeye eee

Ingawa mwasema kwamba si mzuri yeye, kwa tabia njema nimempenda mwenyewe eee

 

[Wote]

Sina mimi sina, mwingine zaidi ya wewe........

 

[Bibie]

Hakuna nasema mimi  nampenda yeye, wangu muadhama roho ANIRIDHISHAE eee

Wangu muadhama roho ANIRIDHISHAE, naomba uzima maisha sote tukae

 

[Wote]

Sina mimi sina, mwingine zaidi ya wewe........

[Rudi mwanzo]

 

[Nipeni Nafasi - Maalim(Zenji)] - tizedboy


(Chorus) 
Nipeni nafasi nimsifu Mpenzi wangu 
Kwa sifa halisi kapewa na Mola wangu 

[Yeye peke yake] 
Nasifu na mwendo, atembeapo Azizi 
Suo kwa vishindo, Viatu havikwaruzi 

(......) 
Mengine ni Siri, Mengine ni Siri, mengine ni Siri 
Sisemi mkasikia........ 

Mtotoooo.... [Wote] 

Nipeni nafasi...

[Rudi mwanzo]

 

[Msijitie Kizunguzungu - Taarab]  - laola


Mwasema kwa nini(x2), Pendo napoteza 
Kumpa fulani, eti najiponza 

Lakini moyoni(x3), Ananiliwaza 

Sivyo enyi walimwengu, Pendo langu kuniharibia 
Msijitie kizunguzungu, Yeye mwenyewe amesharidhia aa 

 

[Rudi mwanzo]