[Vituko Vya Bibi Huyu - Eddy Sheggy]
Nikitazama milima ya kwetu eeee,
machozi yanitoka kwa uchungu na mawazo
Tulitoka wawili ninarudi peke yangu,
Baba na Mama wataniuliza Bibi yako yuko wapi
Natamani gari lisifike upesi,
kwa ile aibu nitakayo pata mbele ya wazazi
Kwa vile miezi michache imepita nilitoka na bibi yule
Alianza kuweka chumvi kwenye chai,
nilikua na wageni wakatoka bila kuaga
Akaweka sukari kwenye mboga,
nikaonja haviliki tukalala na njaa
Juzi juzi kavunja kioo cha dirisha,
apate kuchungulia wapitao njiani
Walisema dalili ya mvua ni mawingu
Niliyempenda kanitoroka maa
(Kanitoroka nateseka) Walisema.........
[Sheggy]
Vituko eee vituko vya bibi huyu.......................
Sitaweza kumsahau oo mama aa
Sitaweza kumsahau oo bibi eeee
Alikua kama Helkopta,
ndege isiyochagua mahali pa kutua ee
Kila mtaa hapa jijini tazameni oh
Hana bwana mmoja wala wawili nifanye nini oh mama aa
(Walisema.............................)
[MOYO FICHO LA SIRI- BENDI(SHEGGY)]
Ama kweli moyo ni ficho la siri mama
Ningelijua nisingempa penzi langu loote nimeeangaika mama
Kupoteza wakati wangu bure oo mama
Kusahau wapenzi wangu woote..ooo mama..sababu yake bety,
oo..mama ee mama..ee bety
sikumoja nilipokuwa nikimsindikiza Shangazi yangu air port nilishangaa,
Kumkuta Bety eee,akimpokea rafiki yangu katokea masomoni
Nillishikwa na butwaaa aliponijulisha ya kwamba eti ni mchumba wake katokea masomoni.
Nimeachwaa ninashangaaa,mwenzenu nalia sheggy
(Chorus)
ooh najuta Sheggy ,najuta ooh kumpenda Cathy
oooh Sheggy najuta ooh kumpenda Cathy,
Nayakubali ya kale,asiyekubali kushindwa si mshindani mama..oooh ...mamaoooh x2
(rudia chorus)