Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]        Rudi Table

 

[Chatu - OSS]

 

[Wote]

Chatu mkali kwa nini wamuogopa!

Mnyama asiye kivuli hana mfupa !

Tena jabari awindapo hana pupa!

Apenda machakani mjini hakuzoea

(repeat x 3)

 

Hutega njiani usiku amekusudia

Ni mwepesi kubaini adui kumfikia

Usimchezee ndugu utaangamia!

Ukufike mtukutu ujute kuzaliwa

(Chorus)

Usimchezee chatu ohoo! chatu ehee!

Dongo usimtupie, utaukosa ushindi! x 2

[Then Chongo anaingiza mashairi!]

Natoa onyo kwa yeyote anayechezea chatu ni hatari

Atakuwa asipate lolote la manufaa

Na ajali imkute bila ya kutegemea!

Atakuja adhirika ajute na Dunia

(repeat chorus)

 

Rudi mwanzo

 

[Homa Imenizidia - OSS]

 

Homa imenizidia miyeeeee ooo, kutwa nashinda nalia

Jua linapochomoza , machozi miye hunitoka

Kisa alichonitenda Rehani , sitokisahau kamwe

Amenishawishi nimuache mume wangu,  ili tuishi naye

 

Nimeachana na mume wangu nimekwenda kwa Rehani ooo

Baada ya muda si mrefu asema niondoke sina tabia nzuri yooo

(repeat 2 lines )

 

(Chorus)

 

[Wote]

Maaama yamenikuta, mamama yamenikuta.....(repeat x 2)

 

[Bichuka]

Ndugu zangu mlioolewa mjihadhari na wadanganyifu

Mkaachana na waume zenu mtapotea

 

[Wote]

Maaama yamenikuta, mamama yamenikuta.....(repeat x 2)

 

[Bichuka]

Nimesimama katikati ya nyia panda....ya njia panda

Jua linazidi kuzama, mamamamamamamamamaamaam eeee

 

[Wote tena hadi mwisho]

Maaama yamenikuta, mamama yamenikuta.....(repeat x 2)...............

 

[Rudi mwanzo]

 

[Nimechoka - OSS ]

Nimechoka eeeh,
Nimechoka na vituko vyako,
Afadhali eeeh,
Tuachane kwa usalama,
Iwapo familia yako inakutegemea bwana wee,
Naona nibaki masikini huru kuliko kuwa tajiri mtumwa papa! x2


Sijazeeka eeeh,
Bado ningali kijana,
Nitaolewa eeeh,
Kama ulivyonioa wewe,
Sipendelei sana kunyanyaswa sababu ya mapesa yako,
Nimeamua leo bila aibu, bila chuki nenda papaa.x2


Kibwagizo:

Gaba eeeh [Gaba ]
Gaba yoyoooo,
Nakubali matatizo nitapambana nayo,
Uzuri wangu oooh kaka,
Utanisaidia oooh x2


Gaba eeeh [Gaba ]
Gaba yoyoooo,
Usifikirie kwamba nitarudi aaah, kwako,
Nakuruhusu uende oa kaka mwingine ooooh,

Duku duku eeeh, x2
Huyo huyo chunusi

[Rudi mwanzo]

[DUKUDUKU NI WASIWASI WAO - OSS]
 
Mara ya kwanza uliniomba tucheze,
Muziki wa kwetu siwezi kukataa,
Mara ya pili ukarudia tena,
SIO kwa kucheza ila kunifinya jicho.

Uliza kwanza ,
Kabla ya kufanya upuuzi wako bwana weee!
Nimeshaolewa,

Nimekuja kucheza,
Nimekuja kufurahisha mwili wangu bwana weee!,
Mimi ni muke wa mtu.

Nimekuja kucheza,
Duku duku ni wasiwasi wao bwana weeee,
Muziki wetu unatia fora,

Wasiwasi wao,
Muziki wao baridi kwetu hakuna shida ooh,
Wacha waseme!!

[Rudi mwanzo]


[FORD - OSS]

 

Ford eheee!

Wewe bado kijana mdogo Ford ee 

Ford eheee!

Kutokana na kazi yako ya biashara

Maendeleo yamekujia haraka Ford eheee!

Umeweza kununua gari na kujenga nyumba ya kisasa 

Pombe ulikuwa hunywi sasa unakunywa kupindukia Ford 

 

(Chorus)

 

[Wote]

Maisha uliyonayo sasa Ford eheee! jihadhari na anasa ooh!Ford 

 

[Bichuka]

Usipende kunyanyaaaasa vijana wenzio ....yo Ford eee, Ford nakuambia

Angalia......madharau kwa vijana wenzio sio mazuri ee Ford nakuambia

 

Wote]

Maisha uliyonayo sasa .........

 

Rudi mwanzo

 

[Uzuri wangu wa Tausi - OSS]

 

[Wote]

Uzuri wangu wa Tausi mama

Maringo kwetu kawaida

Wenzangu wananisengenya, nikipita wao hukonyezana

Wamesahau kazi zao, kutwa nzima kunichunguza

Maringo kwetu kawaida, hamuwezi kunyamaza eeee.......

 

(Chorus)

Hamuwezi kunyamaza, hamuwezi kunyamaza, hamuwezi kunyamaza

Mpaka mseme kila siku eee

 

[Mmoja wao]

Wasiwasi wenu wa nini ngoja niseme ukweli....SEMAAaa

Mwili wangu mzuri, kila vazi linakubali

Uzuri wangu wa kuzaliwa/TAUSI , maringo kwetu kawaida

Nikisema

[Wote] Utakubali

[Mmoja wao] Nikitembea

[Wote] Utakubali

[Mmoja wao] Nikicheza

[Wote] Utaingia wasiwasi

 

(Chorus)

Hamuwezi kunyamaza, hamuwezi munyamaza, hamuwezi kunyamaza

Mpaka mseme kila siku eee............

 

Rudi mwanzo

 

[CHRISTINA MOSHI - OSS]

 

[Mmoja]

CHRISTINA MOSHI sikiliza maelezo yangu katika wimbo huu mama aaa

Naelewa penzi hili ni bado ni changa, usije tena ukabadisha baadaye

[Wote]

Tulipokubaliana kwa hiari, tulikuwa wawili wa tatu Mungu wetu(x2)........

(Chorus)

[Wote]

Pendekezo langu kwako uwe kama BENKI

Benki mahala pa usalama......

Akiba yangu ya mapenzi nakupa wewe Moshi ee mama aaaa (x2)

[Mmoja]

Uwezo sina ningekujengea NYUMBA

Uwezo sina ningekununulia GARI

Uwezo sina ningekupeleka ARUSHA,

Ukapunge hewa nzuri na kutazama wanyama mbugani

 

Bali matatizo madogo hayatonishinda

Nitajipigapiga ili niyatatue...sababu

 

[Wote]JUNGU kuu halikosi ukoko

[Mmoja] Sababu

[Wote]JUNGU kuu halikosi ukoko

[Mmoja]

Mpenzi MOSHI lea hili penzi letu

Usiliweke JUANI litajuja nyauka......

 

[Wote]

Pendekezo langu kwako uwe kama BENKI...........

(Mwisho)

 

Rudi mwanzo

 

[Homa Imenizidia - OSS(Bichuka)]

 

Homa imenizidia mie oo,kutwa nashinda nalia

Jua linapochomoza machozi mie hunitoka

 

Kisa alichotenda Rehani,sitakisahau kamwe

Alinishawishi nimuache mume wangu

Ili tuishi naye

 

Nimeachana na mume wangu

Nimekwenda kwa Rehani

Baada ya muda si mrefu

Asema niondoke sina tabia njema

 

Chorus

Mama yamenishindax2

Ndugu zangu mlioolewa mjihadhari na wadanganyifu

Mkaachana na waume zenu mtapotea

 

 

Niko katikati ya njia panda...ya njia panda

Jua linazidi kuzama mamamamamamama

 

Rudi mwanzo

 

[UMBEA - OSS]

 

Tunapogombana mimi na wewe

Sababu ya maneno ya watu

Tunapokua mimi na wewe

Hakuna kinachotukosanisha

Lakini utokapo kwenda mjini

Unarudi na mambo chungu mzima

Oooo Mpenzi wangu

Kinachonishangaza sijui kwa nini

Watu hupenda kukueleza maneno ya fujo

 

Kwa vile wanajua wewe ni mwepesi

Kuyasikiliza na kuyaamini

 

CHORUS

 

Sikia Mama

Haya ninayokuambia

Achana na yote wanayoyasema

Umbea utavunja ndoa yetu Mama

 

[Rudi mwanzo]

[NIMLILIE NANI - OSS(Dukuduku)]

Nimlilie nani jamani anipe mawazo

Nimpende nani mie anipende nani

Kila ninayempenda Mama yangu hampendi

Yeyote anayenipenda Baba yangu hamtaki

Nikikaa nyumbani nagandamizwa na maneno

Eti wenzangu wameolewa

Mimi bado nipo ndani

 

Nikipunga hewa jioni naitwa mimi jobless

Sielewi sielewi Hawa kweli ni wazazi wangu

Au si wangu

(CHORUS)

Jibu nitapata wapi jibu litoke wapi

Anwani yangu nawaambieni jina langu ni Shida

Posta moja mbili tatu Temeke mtaa wa matatizo

Namba Moja kwenye kona

[Rudi mwanzo] 

[NAPATA PRESSURE - OSS]

 Massamba wa kwetu rudi Mpenzi uniponye

Wiki mbili tangu uondoke mimi taabani

Mapigo ya Moyo hunienda haraka

Usiporudi upesi mimi hoi Baba

 

Mpenzi shauri yako usiporudi upesi

Jinsi navyokulilia wote wanajua

Ugomvi wa nyumbani ni jambo la kawaida

Hatua uliyochukua ni kali sana kwangu

 

CHORUS

 

Massamba nakulilia Baba

Samahani niokoe Mpenzi

Nimekoma Cherie eeeeh

Wivu sio Mapenzi

Sitorudia tena kukusumbua

NAPATA PRESSURE BABA 

  [Rudi mwanzo]

[Somboko Amba - OSS]
 
 
[Wote]
 
Umeshakuwa mtu wa makamo Somboko Amba eee
 
Na mambo ya starehe hukuyaanza leo
 
(repeat)
 
 
 
Ujihadhari na marafiki chungu nzima
 
Kuna marafiki wa uongo na wa kweli
 
(repeat)
 
 
 
Rafiki wa uongo humjua mwenzie wakati wa faraja
 
Na rafiki wa kweli wakati wa matatizo...
 
(repeat x 3)
 
 
 
(Chorus)
 
 
 
[Wote]
 
Usiamini amini mtu yoyote umuonaye
 
Hebu nisikie mwenzangu Somboko Amba ee
 
Siku hizi kila mahali, lalamiko la maisha
 
Dunia ya leo ni vuta nikuvute
 
 
 
[Maalim Ngurumo]
 
Umeshakuwa mtu wa makamo Somboko Amba ee
 
Na mambo ya starehe hukuyaanza leo
 
JIHADHARI  na marafiki hao chungu nzima!
 
Kuna rafiki wa uongo wengine wa kweli  
 
 
 
[Wote]
 
Usiamini amini mtu yoyote umuonaye
 
Hebu nisikie mwenzangu Somboko Amba ee
 
Siku hizi kila mahali, lalamiko la maisha
 
Dunia ya leo ni vuta nikuvute
 
[Maalim Ngurumo]
 
Umeshakuwa mtu wa makamo Somboko Amba ee
 
Na mambo ya starehe hukuyaanza leo
 
Tazama una MZIGO mkubwa wa familia!
 
Panga siku za kutoka utulie nyumbani
 
 
[Wote]
 
Usiamini amini mtu yoyote umuonaye............
 

[Rudi mwanzo]

[Ziada - OSS]

 

Umenieleza mazuri toka mdomo wakooooo,

Bila kusita nikaamini , bila shaka aaah mama,

Kumbe mwenzangu una mengi moyoni,

Usije ukapata taabu, ukaanza kilio,

Niachie mimi nilie, nimekwisha zoeaaaa!x2

 

 

Shemeji usiondoke,

Sikiliza uwe shahidi eeh,

Mapenzi yamenipa kichaa,

Mpaka ikawa fujo,

 

Ziada yuko nyumbani yapata mwaka wa tatu,

Namuita Ziada sauti inakaa ndani bila kuitikiwa eeh,

 

Amenikatisha tamaa na mapenzi yake ohhhhh,

Mama oooyeeee

 

Yolelee, eeeh ,

Mamaa mimi namlilia Ziada eeh,

Mimi namlilia Ziada,

Machozi yamenitoka,

Nachoka leo kulia

 

Ahhh walimpenda Ziada,

Muke wangu walimtamani Ziada,

 

Yolele eeeh , aaaah,

Mamaa  ..

[Rudi mwanzo]

 

[MPAKA MANGA - OSS]
 
Oooo Mpaka Manga watoto umemaliza
Utakula na nani sasa uko pekee
Ubaya wako unajulikana Papa
Ubaya wako sasa umemaliza famille
 
Fikiria mbele siku zinnazokuja utaishi na nani
Oooo Mpaka Manga
 
Utateseka wakati utakua Mzee
Familia yako wameanza kukutambua
Uzeeni wako utakua hauna msaada
 
Watoto umefukuza Mama yao katoroka
Sasa usingizi hauupati kulala kwa vidonge
Ndoto hauoni
 
Mchana huna raha sababu unaishi pekee
Ooo Mpaka Manga Hongera Mpaka Manga
Kazi yako nzuri sasa umekwisha

[Rudi mwanzo]

 

[TAKADIRI – OSS]

Makosa yangu sherieeee

Nakuomba mpenzi mezea,

Sitayarudia tena, nafikiri nimeshaelewa x

 

[Gitaa la nyuzi dozeni kutoka kwa Supreme Ndala Kasheba]

 

Machozi yanidondoka oooh 

Chakula hakimezeki ninaposikia x2 

 

Sitarudia rudia tena

Nakuomba unisamehe,

Takadiri wangu ,

Nakupenda kweli tambua,

Kwa asilimia tisini mapenzi yangu kuelekea kwako x2

 

Nipeleke Lang`ata kwa kaka Bushiri,

Kupitia Longido kwa shangazi Mwajuma,

 

Machozi yanidondoka oooh,

chakula hakimezeki ninaposikiax2

[Rudi mwanzo]

 

[SALMADA - OSS]

 

(Skassy Kasambula akiwa na wana OSS pale Safari Resourt,

kibao hiki amekiimba akishirikiana na Dingutuka Molay, Tchibanda Sony, Benno Villa, Kabeya Badu,

Numbi Kileba, Mobali Jumbe, Hassan Bichuka, na Deus Mugunda. solo lilipigwa na Joseph Mulenga,

rtythm na Ally Makunguru pamoja nae Rajab Zahor, bass na Mohamed Mzee,  Emanuel Zagallo alipiga Drums,

Mbaraka Rajab alipiga tumba, Ngoie Mubenga na Ibrahim Mwinchande kwenye trumpet, Saleh Maluu,

Kimeza Abdalah na Majengo Suleiman kwenye Sax.

 

[Skassy]

Salmada wa ubani wa mzizi wa roho

Salmada dawa yangu niuguapo

njoo unitue uzito wa peendoo nimeelemewa nalo moyoni 

nia yangu Salmada tufunge ndoa

ninachosubiri ni siku zitimie

 

watu hutokea mbali mpaka kufikia kupendana

Salmada eh Salma

kikwazo kwa mwanamke huwa na aibu mwanzoni

na mwanamume hachoki kumbembeleza

hadi leo mamaaa ahhh

nimeridhika kwako Salmada eh

kuwa penzi lako ni la kweli na lenye nia

 

[Wote]

nikuonapo huona raha isiyo kifani

mwenyeji wa mwambao na mwingi wa mahaba

nionapo umbile lako damu hunenda kwa kasi

na mapigo ya moyo yasiyo ya kawaida

Salma Salmada mchumba wangu

Salma Salmada mchumba wangu

 

[Wote]

kila shetani na mbuyu wake Salmada usishangae

njoo tujadili mipango ya ndoa yetu

roho itulie Salmada ehh x 3 

 

[Rudi mwanzo]

 

[MSAFIRI - OSS]

Mimi musafiri bado niko njiani,
Sijui lini nitafika ooohh,
Naulizia watu kule ninakokwenda,
Naambiwa bado ni mbali


Mwili umechoka, maungo yameregea,
Kweli lakini nitajitahidi,
Mpaka nifike kule ninakokweda
Mungu wa miujiza niangazie mwanga oooh

Rudi mwanzo

[DUNIA MSONGAMANO – OSS]


AAhhhh DUNIA MSONGAMANO
Mawazo yamenijia leo,
Ya Mzee wangu alokuwa akisema,
Dunia ni msongamano wa watu wenye akili tofauti,
Ukitaka kuishi vema lazima uwe na utulivu,

Ukitaka kuishi vema fikiri kabla ya kujibu,
Jifunze kwa walimwengu, na walimwengu wajifunze kwako,
Dunia ni kuona mambo,
Na halafu kuyasahau


Kibwagizo:

Dunia msongamano,
Kasema baba,
Nimeyaona leo nakubali mie,

Wengine hupendelea kufurahia,
Wanaposiikia fulani kafa,
Kufa kwa binadamu hupangwa na Mungu,
Namuomba Mwenye Enzi anipe maisha eeh 

Rudi mwanzo

[MANYARA - OSS]

 
Manyara mpenzi wangu nakuomba rudisha mapenzi kama zamani.
Najuta makosa sijui kwa nini hutani kunisikia ooh,
 
 
Kibwagizo:
 
Yoyoyo ooh Manyara mpenzi wangu,
Mie wako ooh nakufa niko hai,
Nimekoma kweli  
Kwa kweli nimeipataa
Nitajitahidi sasa Manyara mpenzi wangu.  
Manyara Manyara wangu mama nakuomba sana!
 
Gitaa la nyuzi dazeni kama kawaida lilikuwa linakung`utwa na Maestrim Nddala Kasheba.

Rudi mwanzo

[Salehe – OSS]
 
Mpenzi nakuwaza mwana mama,
La kufanya sina nasubiri barua nyingine,
Anuani yako,  
Mpenzi Salehe kwa herufi kubwa
 
Barua yako ya mwisho kutoka Unguja,
Ilikuwa ya Novemba mwaka jana mama,
Nilipokea kutoka kwa dada Fatuma,
 
Chorus:
 
Mategemeo yangu ni kukuona Salehe,

Mpenzi Salehe okoa Roho yangu

Usiku mchana nasubiri Barua yako….Salehe

Mbona kimya mpenzi waniumiza,
Salehe mi na wewe mpaka kufa,
Nakuomba unikumbuke japo kwa barua Salehe.

 
Lini utarudi mpenzi Salehe,
Roho yangu ipate tulia Salehe,
Salehe mi na wewe mpaka kufa,  
Nakuomba unikumbuke kwa barua  

Rudi mwanzo

[Marashi Ya Pemba – OSS]

 
Alfajiri upepo wa Bahari umenijia,
Nikaona nyota ya kanda ya Mashariki,
Kuishi visiwani mama,  
Kuna utamu wake,
Mafia , Pemba , Zanzibar visiwa vya kwetu eeh x2
 
( Gitaaa zito la kutisha na vyombo murua)
 
Siku nitafika Pemba, ni siku nitatamani eeh x2
Nitembeze sehemu zote hadi mwisho eeeh,
Kuishi visiwani mama eeh,
Kuna utamu wake,
Mafia ,Pemba, Zanzibar visiwa vya kwetu eeh.
 
 
Kibwagizo:
 
Wala sitabaki nakwenda Pemba  
Ndege inaruka
 
Nasikia ni kuzuri,
Jioni kuna upepo,
Upepo unanukiaaa,
Marashi ya karafuu,
 
Nipae angani ,
Nikatishe bahari,
Juu kwa juu nipae,
Halafu nitue Pemba,
Marashi nikoge ,
Pemba ooh , Pemba ooh  
 
Wala sitabaki nakwenda Pemba ndege inaruka  
 
Marashi ya Pemba, Pemba karafuu

Rudi mwanzo

[AJALI YA AMINANI - OSS] 
 
(Skassy)
ilikuwa saa mbili usiku
ndipo ajali ilipotokea
na kupoteza maisha ya mke wangu
baada ya kuishi nae miaka kumi na saba
na watoto sita kaniachia
pengo lisilozibika na mzigo mkubwa
Aminani Mandari kaniachia
yauweee Aminani, yauweee Aminani  
 
(rudia mwanzo)
 
(wote) kibwagizo
mola iweke pema peponi roho yake
Aminani Mandari mpenzi sito msahau x 2
 
(Bushoke)
sikitiko hapo wenetu aliwaacha bado wadogo
Mwajabu na hamida ehh
waniulizapo baba wapi mama
waonapo wenzao
wanapolaki mama zaoo
watokapo kazini
huita mamaaa
baba wapi mama  
 
(wote) kibwagizo
 
(Bushoke) rudia

Rudi mwanzo

[Umbea - OSS] - Mtukwao

 
Tunapogombana mimi na wewe,
Sababu ya maneno ya watu,
Tunapokuwa mimi na wewe ,
Hakuna kinachotugombanisha,
Lakini utokapo kwenda mjini,
Unarudi na maneno chungu mzima,
 
 
We mpenzi wangu,
Sijui ni kwa nini,
Wewe huwa ni mwepesi,
Kuwasikiliza na kuamini
 
 
Kibwagizo;  
 
Aaaah, Sikia mama,
Usifuate ya watu,
Umbea utaaaa vunja ndoa yetu

 


[SHIDA - OSS] - Mtukwao
 
Shida nilikupenda,
Wazazi wanaelewa hivyo,
Ulipojua nakupenda,
Ukaanza kunitesa,
Nikirudi nyumbani nakukuta umelewa,
Usiku unapoingia,
Maneno ya maudhi tu,
Kiasi naomba,
Usiwepo huu usiku,
Nimekosa nini iiiih,
Mbona wanitesa x2
 
 
Kibwagizo:
 
Walimwengu nifahamisheni,
[Nifanyeje niishi naye Shida]
Walimwengu nifahamisheni
Nifanyeje niishi naye Shida,x2
 
Ana wivu kupindukia,
[Nimejitahidi nimechoka]x2
 
 
OOoooh Pole kaka Muddy eeehx3
 
Ushauri unao mwenyewe eeeeh eeeeeh eeeeh,
Kusuka au kunyoax3
Kusuka au kunyoa aaahaa,aaaahx3
 
 
Walimwengu nifahamisheni .......

 

[Matatizo Yamenikuta - OSS] - Mtukwao
 
Matatizo yanakukuta,
Utalia na nani,
Tulishakwambia mengi hukutaka kutusikiax2
 
Utatesa familia yako kwa kujali anasa,
Kutwa kwenye mitaa,
Nyumbani huonekani x2
 
Na sasa kazi umefukuzwa,
Wabaki wahangaika,
Na wala hata huna la kufanyax2
 
Utatesa familia yako,.......
 
Kazini uliongoza,
Kwa utovu wa nidhamu,
Kwa kweli sasa familia yako haina mapenzi nawe x2
 
Utatesa familia yako.....
 
 
Kibwagizo:
 
Huna hata la kutuambia,
Isihaka x4
 
Makosa uliyokuwa ukiyafanya Isihaka,
Hata kodi ya nyumba ulishindwa kulipa x2  
 
Huna hata la kutuambia.....
 
Marafiki sasa wakuonapo hugeuza sura zao, Na yote tuliyokuambia unayaona sasax2
 
Huna hata la kutuambia.....

 

 [KIPIPA AYUBU - OSS] - Uzegeni

(

solo chini yake Mulenga rythim anapiga Ally Makunguru bass anapiga 

Charles Ngosha, safu inayosimama mbele kuweka sauti ipo chini ya 

Maalim Gurumo, Bichuka, Kasambula, Akida, wakishirikiana na kundi 

zima la wana OSS.
)
 
nakushauri kipipa Ayubu eh  
kuendeleza shughuli alizokuachia mzee wako
jiepushe na tabia ya vijana wa leo  
hawafikirii maisha ya baadae  
kuweka mbele mambo ya raha nyingi X 2
 
(wote) kibwagizo
tunza rasilimali usitetereke
ndio msingi wa maisha kipipa
tunza rasilimali usitetereka ........ kweli nakwambia
ndio msingi wa maisha kipipa ... kweli kipipa
 
(Bichuka)
katika hiyo miradi fikiria ufugaji
usisahau shamba ....... la kilimoo
ni viwanda vya kudumu Ayubu ehh
ndio viwanda vya kudumu kipipa eh  
 
(wote) kibwagizo