Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Kupatwa Kwa Mwezi - Mwenge Jazz Band]

 

Kupatwa kwa mwezi si kiama eeeh mama,

Wala ufukara si kilema ooh mamaaah

 

 

Nilipokuwa na mali nyingi oooh mamaaa

Aliniona kama Mungu wa pili aah mama

 

 

Kuachishwa kazi kwangu kumesababisha tuachane mama

Ohh Mungu,

Mama yako kaondoka bila kudai talaka mama eeeh

Nifanyeje eeeh

Kama mimi nimekosa na mtoto kakosa nini

Masikini eeee,

 

 

Unapolia mwanangu na kumwita mama yako

Njoo mama, njoo mama,

Mimi baba yako unanikumbusha mama yako

 

Nyamaza kulia mama oooh mama

Dunia duara mama ooh mama

Yalopangwana Mungu binadamu hawezi kuyapangua

 

Ingawa mama yako amekuacha eeh bado mdogo

 

Nyamaza kulia mama ,ooh mama

Dunia duara ..

 

Rudi Mwenge

[Rehema - Mwenge Jazz Band] 

[Wote]

Rehema mama oo nakupenda mama ee

Kuachana nawe sitoweza nielewe mpenzi ee

 

[Mmoja]

Ingawa huniamini mama eee

Nakuomba Rey wangu ee tu tuyatunze maisha Rey

 

[Wote]

Rehema mama..... 

Rudi Mwenge

[USIKU WA GIZA NENE - Mwenge Jazz Band] - Uzegeni

 
nashangaa nilikuwa nae asubuhi tu
nikimtayayishia chai awahi kaziniii
na watito wake James John na Bahati
aliwapa pesa za matumizi ya shuleniii x 2
 
nimepata habari baba James amefariki jamaniii ehh  
ninashangazwa na habari hizoo  
moyo waniuma na nguvu mwilini sina
 
pole mama James usilalamike sana jirani oh
kwani matatizo yameumbwa duniani ihh
likikukosa leo la kesho linakungoja
na kazi yake mola haina makosa ehhhhhh
 
(wote) Kibwagizo
umeniacha kwenye usiku wa giza neneee
na mvua kubwa ya mawe yenye radi zenye hasira
 
Naelewa kulia sana ni kumkufuru mwenyezi munguu  
naelewa kulalamika ni kulaani matendo yakeee  
nitawalea vipi James na John yoo .. yoyoyoyooo
 
(wote) kibwagizo
 
unakumbukwa sana na ndugu zako .... lala salama
unakumbukwa sana na jirani zako ....... lala salama
ingawa umetutoka kimwili fikra na vitendo vyako bado tunavyo
 
(wote) kibwagizo
 
nakuombea mola akulaze peponi ..... lala salama
nakuombea mola akulaze peponi ...... lala salama
ingawa umetutoka kimwili fikra na vitendo vyako bado tunavyoo
 
(wote) kibwagizo

 Rudi Mwenge

[Nipeleke  - Mwenge Jazz Band] - tizedboy 


Nipeleke ewe Bwana nipeleke
Nikawaone Vijana wa Paselepa
Kwani Vijana hao wananivutia sana
Kwani mitindo yao ni ya kitamaduni
 
Nina hamu ya kuwaona vijana hao  
Mara mbili kwa Wiki sio vibaya Mume wangu  
Aiyoyoyoyoyo aiyo tafadhali  
Aiyo tafadhali aiyo nipeleke leo aiyo  

Rudi Mwenge