Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]        Rudi Table

[JOGOO LA SHAMBA - Moro Jazz Band]

 
Hiloo ulijidai wewe mbabe sana
Leo umepigwa na kijana mdogo
Aibu imekufika
 
Kiko wapi sasa ulichokua ukijidai nacho
Je ungepambana na mimi kaka
Kilema ungekipata
 
Utampiga nani wee kwanza ukini haujakutoka
Wewe uliona wapi Jogoo la shamba likawika mjini
 
Chorus
 
Ulipotoka shamba kuingia mjini mimi nilikuona huwezi kunitisha
 
Oooo gebe na majivuno yako yamekwisha sasa
Heshima iko wapi
 
Kujidai mmbabe na kudharau wenzio leo umefundishwa  
adabu na heshima

Rudi mwanzo  

 

[Morogoro Yapendeza - Moro Jazz Band]


Jamani Morogoro yapendeza ooohhhhhhh
Maji yatiririka milimani ooohhhh,
Mji msafi Moro wapendeza ooooh,
Njoni mjionee Morogoro ooohhh,
 
Rudi mwanzo  

[MSHENGA - Moro Jazz Band]

Kupitapita kwake kunanipa wazimu
Hii ni wiki ya pili ninamuona
Kila mara akipita nyumbani kwangu kuelekea dukani
Sura yake haki jamani na umbo lake kweli vyanisitua
OOOO OOOO  OOOOO
 
Nitamtuma mshenga akaulize wazazi wake
Nimempenda Msichana akikubali tufunge ndoa x2
 
 
Chorus
Sherehe kubwa sana nitaifanya nyumbani
Majibu mazuri nikipata
 
Nadhiri niliyoweka nitaitoa siku hiyo
Hapo nitapokubaliwa

 Rudi mwanzo  

 

[Ukweli Nimepata - Moro Jazz Band]
 
Ukweli nimepata niliyoyasikia sikudanganywa eeee
Kumbe huko Ng'amboni umeshaolewa na mtu mwingine
Nasema nasikitika kwani ulichokifanya ni dhuluma eee
Wazimu si wazimu huku nimebaki nalia moyoni
 
 
Nawaarifu ndugu zangu wote  
Harusi imevunjika jama oooooo
Niliyetaka kumuoa
Amenikatalia bila kosa mwenzenu eee

Tena ufanye hima uwatumie barua wazazi wako eeee
Warudishe mahari yangu ili nipate tafuta mchumba mwingine 

Rudi mwanzo  

 

[TUTAKUJA GOMBANA - Moro Jazz Band] 
 
Sikutilii mashaka Mpenzi wangu
Lakini mimi sitaki uzoeane nae ooo kijana yule eee
Sina imani naye oo kwa mapenzi yetu
Oooo nakusihi
 
Chorus
 
Nina wasiwasi ee rohoni mwangu  
Na yule kijana eeee
Mwisho wako leo ee kusemasema nae
Tutakuja gombana eee

Rudi mwanzo  

 

[Nikupendeje - Moro Jazz] - Ngosha

Nikupendeje ewe wangu ili ujue mimi nakupenda 
Mawazo yangu kila siku juu yako hayaniishi 

Ni vipi sasa ufanyavyo ugomvi kila siku hata mwanzo sijui 

Wanipumbaza ninashindwa la kufanya Mpenzi wangu 

Chorus 
Nikupe nini we mpaka uridhike 
Usiporidhika sasa nifanyeje 
Mwamuzi ni wewe nawewe washindika 

Rudi mwanzo  

 

[MATUSI YA NINI - Moro Jazz Band] - Ngosha


Tulikua na Salumu mpaka kaenda Ahera wala hatukutukanana 

Alipoingia yeye aliyoleta si miziki bali ni matusi 
Mji wa Morogoro ulisifika sana kwa mambo ya miziki 
na nyimbo zenye maana ooo 

Amekuja mchafuzi wa jina la Moro Jazz na Mororgoro nzima 

Chorus 

Huyooo aona kijicho Sululu la chuma liko Imara 
Matusi yake Mjini Morogoro yameleta sifa mbaya 
Sifa ya Moro jazz ni ya Taifa chuki yake ni ya bure 


[Enzi za Moro Jazz na Cuban Marimba. Maneno hayo] 

Rudi mwanzo