Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]    Rudi Table

 

 

[Barua Toka Kwa Mama - Mlimani Park Orchestra]

 

[Wote]

Mama eee o mamaaa

Salamu zako nimezipata

Ninashukuru kwa kunikumbuka

Ingawa barua uliyonitumia inanitia uchungu

Tabu na mateso unayoyapata yananiumiza roho

Kwa kuwa baba hayuko nawe

Na mimi Mwanao niko mbali nawe

(repeat x 3)

Mama eee.....

 

(Chorus)

 

[Wote]

Ayeee eee mama ooo

Jaribuni kuyasuluhisha mambo hayo

 

[Ngurumo]

Kutengana kwenu kunanipa wasi wasi mwanenu

 

[Wote]

Sina kaka sina dada kwa hiyo naomba

Muishi kama vile mwanzo

 

[Ngurumo]

Ningali mdogo nahitaji msaada wenu wazazi wangu...

 

[Wote]

Ayeee eee mama ooo......

 

Mama eee.....

[Rudi mwanzo]

[Kasim - Mlimani Park Orchestra]

 

[Wote]

Ndugu Kasimu we unayafanyaje sasa maisha ya watoto

Ulipokuwa huna kazi Kasimu we ulikuwa hutoki

Sasa umepata kazi ndugu yangu ee nyumbani huonekani

(repeat x 3)

 

(Chorus)

[Wote]

Unapokuwa huna pesa nyumbani hutoki

Mwisho wa mwezi unapofika Kasimu huonekani

 

[Ngurumo]

Unapotoka kazini unapitia kwenye baa

Unapokuta marafiki unaagiza LETE KAMA TULIVYO!

 

[Ngurumo]

Unaporudi nyumbani umelewa kibao

Unamwambia mama watoto PESA ZOTE ZIMEIBIWA!

 

[Wote]

Unapokuwa huna pesa nyumbani hutoki

Mwisho wa mwezi unapofika Kasimu huonekani

 

[Ngurumo]

Unapotoka kazini unapitia kwenye baa

Unapokaribishwa kiti unaagiza nyingine KEEP CHANGE mama ee

 

[Wote]

Unapokuwa huna pesa nyumbani hutoki

Mwisho wa mwezi unapofika Kasimu huonekani

 

[Ngurumo]

Unaporudi nyumbani umelewa HOI

Unamwambia mama watoto PESA ZOTE ZIMEIBIWA!

 

[Wote]

Unapokuwa huna pesa nyumbani hutoki

Mwisho wa mwezi unapofika Kasimu huonekani

 

[Ngurumo]

Unapotoka kazini unapitia kwenye baa

Unapokaribishwa kiti unaagiza LETE SANDUKU MOJA

 

[Wote]

Unapokuwa huna pesa nyumbani hutoki

Mwisho wa mwezi unapofika Kasimu huonekani

 

[Ngurumo]

Unapotoka kazini unapitia kwenye baa

Unapokaribishwa kiti unaagiza LETE SANDUKU MOJA

 

(Kasim wa kustarehe utaua watoto.....)

[Vyombo]

 

[Wote]

Unapokuwa huna pesa nyumbani hutoki

Mwisho wa mwezi unapofika Kasimu huonekani

 

[Ngurumo]

Unapotoka kazini unapitia kwenye baa

Unapokuta marafiki ukiigiza MOJA MOTO MOJA BARIDI!!

 

[Rudi mwanzo]

 

[Celina - Mlimani Park Orchestra]

 

[Wote]

Najua najua una mawazo

Lakini tutafanyaje ikiwa wazazi wako wameamua hivyo

Nia yangu na madhumuni yangu ......

Ilikuwa tufunge ndoa na tuishi sote kama mke na mume Celina

 

Nimejitahidi kadili ya uwezo wangu

Wazazi wako wameniwekea vikwazo vingi.....

(Repeat x 3)

 

Nimejitahidi kadili ya uwezo wangu

Wazazi wako wameniwekea vikwazo vingi.....

[Ngurumo]

Celina aaaa.......

 

(Chorus)

[Wote]

Oo Celina piga konde moyo oo Celina......

Oo Celina utafanikiwa oo Celina......

(repeat)

 

[Ngurumo]

Na kwa sababu imekuwa hivyo Celina aa

Sioni haja ya kutaka UJIUE kwa ajili yangu ...

 

[Wote]

Oo Celina piga konde moyo oo Celina......

Oo Celina utafanikiwa oo Celina......

 

[Ngurumo]

Na kwa sababu imekuwa hivyo Celina aa

Sioni haja ya kutaka UJICHINJE kwa ajili yangu ...

 

[Rudi mwanzo]

 

[NEEMA -  MLIMANI PARK]

 

Usipate taabu  u Neema, uliyoyafanya sio mageni hapa Duani ehee!Neema!

Ikiwa kupendana mama ,Wapo waliopendana kama watoto mapacha! Neema!

Ikiwa ni mapenzi ii Bibi wapo waliopendana kama kumbi kumbiNeema!

 

Kumbi kumbi ooooh! 

Wanapendana sana hata wakati wa kutembea utawaona ! bibi mbele bwana nyuma!

Lakini sio ajabu kwani hata wao hutokea wakati wakakosa kuelewana

Tena kwa kiapo oo Neema, sembuse mimi na wewe

 

Ingawa roho iliuma, ooh mamaa uliponiezea  

kwamba bwana uliyezaa naye yupooo  

kwa hiyo nisije nyumbani kwako, hata kazini nisikufuate  

Hata kusalimiana na mimi hutaki  japo twafahamiana eee   

Hata shemeji zako Kitimtim na Ngule niliwatuma  waje wakupe salam zangu bibieeee   

 

(CHORUS)

Oh!Neema Oh Mpenzi Maua!

Oh!Neema Oh Mpenzi upepo!

Sina neno mimi, kwa kuwa najua huyo ni mzazi mwenzako.....penzi upepo!

 

[Chidumule]

Ipo siku ehe nitakuja kwa wazazi wako o Neema

Nilete barua ya uchumba mie oo..

Tufunge ndoa na wewe.....penzi upepo....

 

Rudi mwanzo

 

 

[GAMA - Mlimani]

 

Afadhali pia ungenieleza makosa niliyokutenda yoo we Gama

Kabla hujaamua kuniachaaaaa

Ulilazwa hospitali miezi mitatu, miezi sita masomoni yote nimevumilia eee

 

Unataka upendwe vipi yooo we kaka?

Unataka upendwe vipi yooo we GAMA

 

(Chorus)

[Wote]Naomba unisamehe we kaka

[Mmoja] Nani atawaelea

[Wote]Naomba unihurumie  we kaka

 

Rudi mwanzo

 

[Christina Bundala - Mlimani(Max Bushoke)]

 

Ama kweli penzi jamani halikadiriki

Hata ulipime na mzani gani

[Benno Villa]

 

Nililichezea kamari pendo lake Christina

Na kujisahau kama lingenifaa na kudumu maishani mwangu x2

 

[(wote]

Nililichezea kamari pendo lake na kuuza utu wangu

Kwa wasio thamini penzi wala kujua maana ya kupendwa

 

[Ngurumo]

Kwa kweli Mpenzi Christina leo naomba unisamehe 

Nitunze uniongoze kwenye penzi lako la haki

(Rudi wote)

 

[Ngurumo]

Nilihadaishwa na anasa za dunia

Kwa kweli Binadamu hujifunza kutokana na makosa

 

Rudi mwanzo

 

[Hata Mwezi Bado - Mlimani]

 

(Chorus )

Hata mwezi bado oooo, tangu tuoane ee

Kelele kila siku ndani ya nyumba yetu mama

(Benno VILLA) 

Ninaporudi kazini majirani huzima redio

Ili wasikize tunavyogombana

Wametupachika majina wewe Pwagu na mimi Pwaguzi 

Kwa vile imekua ni mazoea

Ingawa nimekuoa kwa pesa na pendo langu ee

Tabia zako zimenishinda ooo nasikitika

 

(Chorus )

Hata mwezi bado oooo..........

 

Ulikua utunzi wake CHIDUMULE COSMAS

 

Rudi mwanzo

 

[MAMA FELLY - MLIMANI]

 

Nina langu jambo linalonikera moyoni
Kidogo, kidogo...................


Nimevumilia lakini roho inauma aa
Umeanza kwa ndugu zako
Kuyafikisha malalamiko yako
Eti nina mpango wa kuoa mke mwingine
Wazo hilo sina mama
 
Lakini leo naona kama una lako jambo........

(Chorus)

Tumetoka mbali eeee Mama Felly ooo

Yatupasa tukumbuke kulea watoto

Ili nao wajidai mbele ya wenzao

Baba yetu na Mama wapo kama sisi tunavyosema......

 

[Chidumule]

Kumbuka furaha ya watoto ni fahari kwa wazazi ee

Kumbuka furaha ya Doto na Kulwa  fahari kwetu mama

Tukitengana ....tutawapa ukiwa bure

Tukitengana nawe tutawapa mateso watoto wetu

 

Rudi mwanzo

[Maudhi Nyumbani - Mlimani]
 
 
[Wote]
 
Maudhi maudhi ya kila siku eee
 
Hayo mimi sintoweza aaa  
 
Ni vigumu kukubali umekosa aa
 
 
Ingawa dharau na maudhi mengi
 
Bora tujiulize tunatoka wapi tunakwenda wapi sasa aaaaa
 
Suala kubwa kwetu ni watoto
 
Ikiwa tutakosana watakwenda wapi ee?
 
Ikiwa tutakosana watakwenda wapi , wazazi wao ni sisi
 
Yafaa tujirekebishe.................!
 
(repeat x 3)
 
 
 
(Chorus)
 
 [Wote]
 
Poa ewe kipenzi changu nimekusikia
 
Naahidi mbele yako nitajirekebisha
 
 
[Ngurumo]
 
Kwa kweli mpenzi tunayofanya janatuabisha
 
Tunapogombana watu hujaa tele nyumbani....!
 
 
[Wote]
 
Poa ewe kpenzi changu nimekusikia
 
Naahidi mbele yako nitajirekebisha
 
 
[Ngurumo]
 
Kutukanana mbele za watu si jambo jema
 
Kuna hatari ya kuwafundisha watoto tabia mbaya
 
 
[Wote]
 
Poa ewe kipenzi changu nimekusikia

Naahidi mbele yako nitajirekebisha

[Rudi mwanzo]

 

[Aziza(Uzuri i Shani) - Mlimani Park Orchestra]

Nasikitika aaaa, kubadili mawazo yako wewe
Kijana nakuonea huruma (........)

Kijana una umbo la kupendeza
MREFU MNENE na MWANYA wa wastani

Aziza uzuri si shani,
Uzuri wa mtu ni tabia njema

(kila nikiuimba kinanijia kipande kingine sijui ni cha huu wimbo Aziza au vipi)

Aaaaa mimi .....
Najuta najuta sana
Ningeyajua hayo oooo
Nisingekubali kamwe

Kitu gani...mimi nimefanya
Hadi umetafuta BWANA mwingine?

Aaa mimi ....
Najuta najuta sana........

[Rudi mwanzo]

[NDOA YA LAZIMA - Mlimani Park Orchestra]

(Utunzi wake Cosmas Chidumule, kuimbwa naye pamoja na Fresh Jumbe, Benno Villa, Lubua, na Bushoke, solo limepigwa na Michael Billali, Rythim na Huruka Uvuruge, bass chini yake Julius Mzeru na kushirikisha sqadi zima la wana Sikinde ngoma ya ukae. Kibao hiki kimetiwa muziki na King Michael Enock )


(Fresh Jumbe)
mke mlionichagulia enyi wazaziii
oneni sasa sielewani nae vyema
ndani ya nyumbaa x 2

(wote)
kama mtakumbuka vizuri
wazazi wangu
nilichukia sana
wakati ule
na sababu kubwa hasa nilimkataa mke huyu
ambaye mlinichagulia nyiee

(Fresh Jumbe)
mkazidi kunisisitizia kwamba
mwanetu eh muoe mchumba huyu
ana tabia nzurii

(wote)
kama mtakumbuka vizuri
wazazi wangu
nilichukia sana
wakati ule
na sababu kubwa hasa nilimkataa mke huyu
ambaye mlinichagulia nyie

(wote) kibwagizo
sasa mnayaona wazee..... .... wazeee
mambo anayofanya mke huyu ..... mke huyu
anafikia hata kudharau wewe mama mzaziii

(Chidumule)
na wageni wafikapo hapa nyumbani kwetuuu
anaanza kununa bila sababu
na vituko vingi na hivi na vile
nashindwa kuelezea ni aibu kwa wazeeee

(wote) kibwagizo

(Chidumule) rudia

[Rudi mwanzo]

[Nawashukuru Wazazi - Mlimani Park Orchestra]


[Bichuka] 

Nimeishi na wazazi wangu nikiwa bado mwanafunzii 

Sukuwahi kuishi peke yangu bila kuwa na wazazi wangu 

Baada ya kumaliza masomo nilipata kaziiii 

Wazazi wangu walinihusia jinsi ya kuishi na walimwengu  

 

[Wote]

Ya kuwa niwe na heshima kwa mkubwa na mdogo 

Hayo ndio mafanikio ya maisha yangu ya baadae  

 

(Chorus)

[Wote]
Nawashukuru wazazi wangu wakati wowote
Ushauri wao umeniletea mafanikio mema
Sasa naishi...na watu vizuri
Sasa naishi...na watu vizuri eee mama

[Mmoja]
Huku nilipo wazazi wangu sina ndugu
Lakini kutokana na usia wenu wazazi wangu
Najiona kama, nipo nyumbani
Najiona kamaaaa nipo nyumbani ee mama

[Rudi mwanzo]

[Kugombana Sipendelei - Mlimani]

 (COSMAS)

Ingawa tumezoeana rafiki yangu ooo oooo oooo

Lakini itabidi toka leo tuyapunguze matembezi ya pamoja

 Unajua toka siku ile ulipogombana na shemeji

Kwa ajili ya kuchelewa kurudi nyumbani

Lawama nyingi nilizipata

Kua mimi ni Mwalimu wako

(WOTE)

 Kugombana kila siku hata mimi sipendelei

(Ngurumo)

Rudi nyumbani mapema uwaone watoto

Kugombana kila siku hata mimi sipendelei

 (Ngurumo)

Tafadhali nakuomba usimnyanyase mkeo

 Kugombana kila siku hata mimi sipendelei  

[Rudi mwanzo]

 

[TALAKA REJEA - Mlimani(DEDE)]

Ulinisaliti kwa talaka rejea

Bila aibu ulininyang'anya nguo mbele za watu

Huku ukitoa kashfa....nikajifunze kwa wazazi wangu!

Leo unaniambia nirejee kwako, ulivyonisaliti umesahau...

Mpenzi eeeee AKHERI nipate tabu kuliko kurejea kwako 

 

(Chorus)

Nakuambia mimi sikutaki tena .....siwezi (x2)

Abeli Bathazar ooo jama.....siwezi

Mwanaibu Rahimu naye pia jama.....siwezi

Bichuka kaka ooo DEDE.....siwezi

Shabani DEDE ooo DEDE siwezi

 

Nakuambia mimi sikutaki tena .....siwezi (x2)..... 

 

[Rudi mwanzo] 

[USITUMIE PESA(Kama Fimbo) - Mlimani Park(Cosmas Chidumule)]

COSMAS...

Sikusimuliwa haya ninayoyasema

Nimekusikia mwenyewe ukimsimanga yule Msichana

Eti kwa nini amempenda mtu kama Chidumule

Kwanza fukara sina nyumba wala gari 

(Kwanza fukara sina mbele wala nyuma)

Nitampa nini eee huyo Bibi jamani oooox2

 (Ngurumo& hamisi)

Ameshasema hakutaki kaa chonjo

Ameshasema hakutaki kaa chonjo

(COSMAS)

Lazima katika mapenzi kamwe hakuna

Na penzi la pesa duniani hakuna

Kwani hata kobe ana mpenzi wake

Na kamwe hajui pesa oo Mama ninasema

 

Unamponda yule kijana ili Bibi akuthamini wewe

Ukimpenda Msichana sema nae polepole

Kamwe hakuna haja ya kumkashifu kijana mwenzio

 

(Ngurumo& Hamisi)

Ameshasema hakutaki kaa chonjo

Ameshasema hakutaki kaa chonjo

 

CHORUS

Usitumie pesa kama fimbo Kaka

Mambo ya  kutaka taka makubaliano

Hapo ndipo pesa huwa na thamanix2

 

(COSMAS)

Ikiwa mapenzi mpaka Bibi akupende

Hata kama fundi wa kuhonga mpaka Bibi akubali

 

(WOTE)

Usitumie pesa kama fimbo Kaka

Mambo ya pesa yataka makubaliano

Hapo ndipo pesa huwa na thamani

 

(COSMAS)

Ikiwa mapenzi mpaka Bibi akupende

Hata kama Mzee Kimwaga lakini kwa mipango

 

(WOTE)

Usitumie pesa kama fimbo Kaka

Mambo ya pesa yataka makubaliano

Hapo ndipo pesa huwa na thamani

 

(COSMAS)

Ceci amesema Cosmas mpaka kufa

Nami nasema Ceci wangu wa kufa na kuzikana

 

(WOTE)

Usitumie pesa kama fimbo Kaka

Mambo ya pesa yataka makubaliano

Hapo ndipo pesa huwa na thamani

 

(COSMAS)

Hata njiwa ana mpenzi wake kwenye tundu

Ingawa njiwa hajui noti wala shilingi

 

USITUMIE PESA......................... 

  [Rudi mwanzo]

 

[VISA  - Mlimani Park Orchestra]

(Kibao kimetungwa na Hasan Rehani Bichuka kuimbwa nae pamoja na Cosmas Chidumule,

Maalim Kinyasi, Muhidin Gurumo; solo lilipigwa na Joseph Mulenga; rythim na Abdalah Gama;

na bass limepigwa na Computer Mwanyiro) 

(wote)
ohh ohhooo ohoo ohh dear
ohoo ohoo ohoo ohh dear
limekuwa ni jambo lisilotegemewa na wengiiii
haswa kwa wanao tufahamu na wetu wazazi pia
imekuwa ni jambo lisilotegemewa na wengiii
hasa kwa wanaotufahamu na wetu wazazi pia
 
(Bichuka)
lakini kwangu  
imekuwa si jambo la ugeni
wala kushangaza  
wala kushitusha


mimi ni amba eee nimeishi nawe siku nyingi
wengineo ni vigumu kufahamu yetu tofauti
penzi ni kusikilizana
si kama hili la sisi ........ Mulenga ohh
 
(wote) kibwagizo
visa vituko na dharau dada
na mengi ................

bila idadi nimevumilia x 2
 

(BIchuka)
kama mapenzi yaua  
kufa sioni muhani muhari eeeh
 
(wote) kibwagizo
 
(Bichuka)
leo nimefika kikomo  
naufunga mdomo wanguu ahhh
 
(wote) Kibwagizo
 
(Bichuka)
usiponipenda wewee
wenzio wanitafuta
 
(wote) kibwagizo

 [Rudi mwanzo]

[KATA YA MAJI UKWENI - Mlimani Park Orchestra

 

Naelewa thamani ya penzi kati yangu nawe Nuruu,

Ndio maana ninasema siwezi kukuacha (x 2)  

 

[Wote]

Waliona mimi kuwa na wewe ni miujiza kwao walimwengu

Ndio maana lilikwakera penzi letu  

 

[Bushoke]

lilipowakera walitafuta kila njia, ili kulivuruga na wewe ulikubali na siku ikawadia Ohh ...

 kwa kuninyima hata tone la maaaji wakati nina kiu, wakati nina kiu        nina kiu  

 

[wote] 

Waliona mimi kuwa na wewe ni miujiza kwao walimwngu

Nndio maana liliwakera penzi letu   

 

[wote]

Siwezi, siwezi kutoa nadhiri japo wametima kulivuruga penzi letu, 

Japo wametimiza kulivuruga penzi letu siweeezi   

 

[Benno Villa]

Kama wametimiza hiloo lakini nakataaa ahadi yao, 

Ya kuninyima hata tone la maji wakati nina kiu .............. nina kiu  

Nia yao nikose mpenzi wa kunituliza   

 

[Wote]

Siwezi kutoa nadhiri......   

 

[Bushoke]

Mkasaa huuu nikueleza kiundani .......

taratibu  unafanana na hadithi ya mchumbia 

Aliyepewa kata ya maji ukweni.......... kata ya maji ukweni  

Baada ya kunywa funda tatu za majii,  

kanyang'anywa kata mdomoni  kabaki na kiu yake jama oh  

 

[Wote]

Siwezi kutoa nadhiri......

 

Rudi mwanzo

[TAXI DRIVER -  Mlimani Park Orchestra]

Taxiiii! taxiii!
 
Mama Jacqueline ninajua ni nini kinachokunyima raha,
Ahhh mama Jacqueline,
Ninajua ni nini kinachokukondesha,
Ninajua ni nini kinachokukondeshax2
 
 
Maamaa Jacqueline usisahau kuwa kazi yangu ni taxi driver
 
Usisahau abiria si wa aina moja  eeh (mama watoto)
Awe mwanamke , awe mwanamume  
wote ni abiria wangu eeeh
Mimi ni taxi driver!
 
 
Kazi yangu mimi mwenzio isiwe sababu au kisingiziooo
Kuwa hii siyo taxi bali ni gari ya kubeba vimada,
 
 
Usisahau abiria wangu si wa aina moja ..

Rudi mwanzo

[CLARA Mlimani Park Orchestra]

 
Ninajua mwenzangu karibuni utatoka hospitalini,
Utokapo tafadhali,
Fika mjini umtafute mpaka umuoneee,
Mchumba wangu Clara, mchumba wangu Clara x2
 
 
Kibwagizo:  
 
Nyumbani anakoishi,
Ni Msimbazi kota,
Ukimuona mpe salamu nyingi sana,
Mueleze mchumba wako Kitwana,
Anakusalimuuuu
 
Kama hajasikia eeehx2  
Ajali  iliyonipata,
Nimekuwa kilema,
Na kilema isiwe kisingizio cha kukosa kuja kuniona,
 
Tafadhali ukimuona muulize kama kweli Clara yuko radhi,
Niteseke hospitali eeh,
Kwa maradhi bila kunijulia hali,
Kwa maradhi bila kunijulia hali ( oooh mama najuta )

Rudi mwanzo  

[Shemeji Yangu Issa - Mlimani Park Orchestra]

 
Shemeji yangu leo mbona u-mkimya
Na huku umejiinamia
Kwani si kawaida yako kuwa hivyo
Leo Kuna nini hapa nyumbani
 
(Sista kwa huzuni anajibu.......lakini yamenitoka.Baadaye anasema hivi)
 
Vitendo alivyofanya kaka yako Issa
Ni vya huzuni na ni vya kusikitisha
(Sijui alifanya nini huyu Njemba)
 
(Chorus)
[Wote]
 
Mnatusema sisi wanawake wabaya
Mnatusema sis wanawake wabaya
 
[Mmoja]
Kama mimi ndio ningefanya hivyo
Sijui ingekuwaje .......Shemeji yangu Issa....a
 
[Wote]
Mnatusema sisi.........

Rudi mwanzo  

 

[HISTORIA YA KWELI YA MWANADAMU - Mlimani Park Orchestra]

( Sikinde na kibao Historia ya kweli ya mwanadamu, 

utunzi wake Bichuka, kuimbwa nae pamoja na Hussein Jumbe, 

Francis (Nassir) Lubua, Benno Villa, na Max Bushoke, 

solo lilipigwa na Henry Mkanyia, sec solo na Kassimu Rashidi, 

rythim na Huruka Uvuruge, bass na dogodogo)

historia ya kweli ya mwanadamu

ndio kiumbe wa kwanza ulimwenguni

historia ya kweli ya mwanadamu

ndio kiumbe wa kwanza ulimwenguni

(wote) Kibwagizo

kapewa akili ili afikirie

hatimaye kuyaendeleza maisha yeke x 2

(Bichuka)

mwenyezi mola kaumba

watu tofauti

wapo makatili

na wenye huruma

ili tuje tupendane jamani

na tushirikiane sote kwa pamoja

(wote) kibwagizo

(Bushoke)

binadamu fikiria kwa makini

ongeza juhudi katika kazi yako

maendeleo hutokana na juhudi zako

usichoke kujifunza

kwani elimu ni bahari ..... mwanadamu

(wote) kibwagizo

[DUNIANI KUNA MAMBO - Mlimani Park Orchestra] 

 

(Utunzi wake Suleimani Mwanyiro, kuimbwa na Bichuka, 

Muhidini Gurumo, Cosmas Chidumule, solo lilipigwa na Joseph Mulenga, 

sec solo na Abel Baltazar, rythim na Mwanyiro bass katika wimbo huu wa 

mahadhi ya reggae lilipigwa na Abdalah Gama ambaye walikuwa na kawaida 

ya kubadilishana magitaa na rafikiye Mwanyiro)

(Bichuka)

duniani kuna mambo

unapokuwa u-mkimya

wanakufuata fuata na maneno

ili wao wakupe sifa mbaya

hata ukifanya jambo zuri

wao wanalikashifuu

kwa vile wamezoe kusema ehh waseme mwisho watachoka X 2

(wote) Kibwagizo

waache waseme

mwisho watachoka .... mwisho watachoka

ngoma ya sikinde tunaindeleza

(Gurumo)

walimwengu tuacheni

maneno maneno ..... ohh maneno

tutizame dunia hii

inavyokwendaa... mbele

(wote) kibwagizo

(Gurumo)

kutetana tetana hakuna maana yeyote

nawaombeni walimwengu

tushirikiane jamani ih ih

(wote) kibwagizo

[Usisikie La Kuambiwa - Mlimani Park Orchestra] 

(Chorus)

[Wote]

Sio wivu mke wangu eee naona uchungu kusikia

Maneno kwa majirani mimi nina wasiwasi

[Mmoja (DEDE?)]

Wasiwasi wako mke wangu(x2)

Usisikie la kuambiwa mpaka uone mwenyewe eee

[Wote]

Mmmmm Kama ni wasiwasi haya

Eeeee kama ni wasi wasi hayaaaaaaaa

Linalosemwa na watu mwisho wake huonekana

Sio wivu mke ..........

[Rudi mwanzo]

 

[TELEGRAM - Mlimani Park Orchestra]

 

Kaka naijibu telegram,  Niliyoipata kutoka kwa mkeo oooh  

Anaomba ushauri wangu  

Kwa kuwa maelewano yenu ndani ya nyumba  Yamekuwa madogooo

 

[Chidumule]

Nakuomba heri itawale shari  

Mkumbushane hisani msameheane,  mkumbushane hisani msameheaneeeee  

Kama wazaziii......   

 

(Chorus)  

 

[Wote]

Katika majibu niliyotumaNimemuusia mkeooo (atakonda bure mtoto wa watu),  

Kama ameazimia kutorudi nyuma kimapenzi  

Avumilieeee   

 

 

[Chidumule]

Ninakuusia mimi , Mke ndani ya nyumba  

Hapigwi kwa fimbo au makofi  

Hupigwa kwa upande wa khanga  

Kwani mkeo ni pambo la nyumba   

 

[Wote]

Katika majibu niliyotuma......

 

[Chidumule]

Sasa wewe kaka yangu  Sisemi mengi mie  

Ila nakukumbusha kuwa  Adabu dhahabu  

Na starehe ni pambo la wakati   

 

[Wote]

Katika majibu niliyotuma....... 

 

Rudi mwanzo  

 

 

[Conjesta - Mlimani Park Orchestra]

 

(Kibao hiki kimetungwa nae Fresh mwana wa Jumbe, 

kuimbwa nae akishirikiana na Benno Villa, cosmas Chidumule, 

na Francis Lubua solo limepigwa na Michael Billal, 

rythim Huruka Uvuruge na bass limepigwa na John Ngosha, 

tumba kama kawaida zimepigwa na Jamwaka, 

trumpet zikiwa mikonomi mwa Machaku, bwana Ibrahim Mwinchande, 

midomo ya bata ilipulizwa nae Joseph Benard akishirikiana na 

King Michael Enock, drums chini ya Chipembele Saidi 

fundi mitambo akiwa marehemu Hezron Mwampulo)

 

[Jumbe]  

Nimetembea pande nyingi za dunia  mashariki na magharibi ihii jamani eh  

Nikatifuta mpenzi mwenye busara  ili kujenga mapenzi ya kweli  

Na sasa kwako mpenzi nimefikia ukingoni eh  

Sitegemei kupenda mwengine tena zadi yako we CONJESTA  

Na sasa kwako mpenzi nimefikia ukingoni eh  

sitegemei kupenda mwengine tena zaidi yako we CONJESTA   

(solo ya Bilal)   

 

(Chorus)

 

[Wote]

Mtoto mwenye imani Conjesta nimeamua kukupenda wewe pekee duniani (x 2

 

[Benno Villa]

Mapenzi mazito sioni mwengine wala sisikii la yeyote yule ila ni weeee   

 

[Wote]

Mtoto mwenye imani Conjesta nimeamua kukupenda wewe pekee duniani (x 2

 

[Jumbe]

Macho yanguuu na masikio yangu, mawazo yangu yote ni kwako weeee   

 

[Wote]

Mtoto mwenye imani Conjesta nimeamua kukupenda wewe pekee duniani (x 2

 

Rudi mwanzo

 

 

[HIBA - Mlimani Park Orcchestra]

 

(Utunzi ni wake Marehemu Mharami Saidi, 

kuimbwa na Hasan Rehani Bichuka (sterio) 

akishirikiana na kundi zima la wana ngoma ya ukae, 

Muharami mwenyewe akipiga gitaa la rythim na 

Abdallah Gama katika wimbo huu ndio alipiga bass 

nadhani alibeba mikoba yote ya kaka yake Mwanyiro ipasavyo. 

 

[Bichuka]

Hiiba nimelibeba pendo lakoo kama mwana na mbelekoooo  

Hiiba nimelibeba pendo lakoo kama mwana na mbeleko  

Nina maana kukwambia mchana usiku silali natafuta pesaa  (x2)

 

Ili tuishi vizuri na kujenga familia bora yenye thamani na penzi (x2)

Hiiba imekuaje mpenzi mbona umebadilika aha ah  

Hiiba imekuaje mpenzi mbona umebadilika   aaaaaah

 

(sauti ya midomo ya bata kutoka kwa King Michael Enock)   

 

(Aa Hiba, Hiba, Hiba, nimekukosea nini mpaka kufika kunikataa Hiba)

 

[Bichuka]

Ili tuishi vizuri na kujenga familia bora yenye thamani na penziii

Hiiba imekuaje mpenzi mbona umebadilika  aaaaa 

 

[Wote]  

Hiba oh Hiba imekuaje Hiba  Hiba oh Hiba nieleze leo (x 2)

 

[Bichuka]

Badiliko la pendo lako lanitia wasiwasi  

kipi nilo kuudhi yoo oh Hiba  

(repeat) 

 

Ninapokuuliza wewe unanunanuna  

Ninapokuuliza hiitikii hata kidogo Hiba  

Ninapokuuliza hutaki kusema nami Hiba  

 

Unanisikitisha sana unapokataa kula nami Hiba   

 

[Wote]  

Hiba oh Hiba imekuaje Hiba  Hiba oh Hiba nieleze leo (x 2)

 

Rudi mwanzo  

 

[Sauda - Mlimani park Orchestra]

 

[Prelude Bichuka]

Haaaya......Sauda .....oo...nisikilize...dada

 

[Bichuka]

Tangu tuwe wapenzi tumependana kikweli pendo letu la moyoni ee

Mioyo yetu tusibadili wangu kipenzi dada tuepuke ushauri eee

Na mahasidi wa penzi o sauda

Wa mahasidi wa penzi dada Sauda

Na mahasidi wa penzi o sauda

Wa mahasidi wa penzi dada Sauda

(repeat)

 

[Wote]

Sauda oooo mamaaaa

Sauda oooo mamaaaa

(repeat)

 

(Chorus)

 

[Wote]

MV Mapenzi Meli ya wapendanao

Moyo kama Bahari Manahodha mimi na Wewe

(repeat)

 

[Ngurumo]

Duniani kuna mengi sawasawa na Bahari

Kuna Papa na Nyangumi tena wale wa hatari.....e e

Hawapendi kuiona Meli yetu baharini

Watafanya kila njia kuifupisha/(waifupishe) Safari

 

[Wote]

MV Mapenzi Meli ya wapendanao.........

 

Rudi mwanzo

 

 

[Hapendeki - Mlimani Park Orchestra]

 

[Wote]

Hapendeki umekuwa mtoto wa kutanga tanga hovyo wee Hapendeki(x2)

Umekimbia kwenu Kijijini ukaenda Mjini kutafuta kazi

Kazi ulipoipata hukuwakumbuka Baba na Mama Hapendeki

Sasa kazi umefukuzwa......

 

(Chorus)

 

[Wote]

Umekuwa mtoto wa kutanga tanga hovyo Hapendeki wee Hapendeki

 

[Mmoja miondoko ya ku-rap]

Wee Hapendeki rudi nyumbani....ndio Baba

Na hizi pesa nyingine nenda kanunue Unga na Dagaa huko uwapeleke wazazi

Utakuja kamatwa hapa na NguvuKazi upelekwe Manza

Na hali kwenu hapa hapa Kisijo 

Mwaka wa nane hujarudi nyumbani Hapendeki

 

[Wote]

Umekuwa mtoto wa kutanga tanga hovyo Hapendeki wee Hapendeki

 

[Mmoja miondoko ya ku-rap]

Wee Hapendeki rudi nyumbani....ndio Baba

Na hizi pesa nyingine nenda kanunue Unga na Dagaa huko uwapeleke wazazi

Utakuja kamatwa hapa na NguvuKazi upelekwe Singida

Na hali kwenu hapa hapa Mbagala 

Mwaka wa nane hujarudi nyumbani Hapendeki

 

[Wote]

Umekuwa mtoto wa kutanga tanga hovyo Hapendeki wee Hapendeki

 

[Bichuka kwa huzuni anaingia]

Ulipopata kazi uliwasahau wazazi

Wanapata uchungu kusikia unapata matatizo

(repeat)

 

Fanya rudi nyumbani eeee Hapendeki ooo

Fanya urudi ooo Hapendeki mama 

 

Fanya urudi nyumbani eeee Hapendeki ooo

Fanya urudi ee Hapendeki oo kaka 

 

[Wote]

Umekuwa mtoto wa kutanga tanga hovyo Hapendeki wee Hapendeki

 

Rudi mwanzo

 

 

[MWANETU KAZA MOYO - Mlimani Park Orchestra]

 

MWANETU KAZA MOYO ni utunzi wake Chidumule, 

solo lilipigwa na Abel Baltazar, rythim na Abdallah Gama 

na bass chini yake Computer Mwanyiro, 

huku trumphet zikipulizwa na Boniface Kachale.

 

[Wote]

 

Nimekubali maneno yenu wazazi wangu

Kuwa uzuri wa mtu sio Sura ni tabia

Yule mume niliyemkubali kanishinda hila

Nipomuulizapo hunijibu:

Wewe ni mama wa ndani tu 

Una shida gani?

Na kila kitu ninakutimizia

 

Hata kama mimi ni mama wa ndani tu jama ee 

Sio arudi saa kumi za usiku

Kwa hiyo wazazi wangu ......

Tabia hizo zimenishinda ni bora nirudi kwetu

(repeat)

 

(Chorus)

 

[Wote]

Mwanetu kaza moyo uishi na mumeo....mumeo huyo

Ni wewe mwenyewe uliyempenda

 

[Chidumule]

Tulikufahamisha mapema 

Kuwa mchumba wako ni mlevi ...mlevi

Hukutaka kutusikia....hukutaka kutusikia

 

Leo umeyaona mwenyewe ee...mwanetu eee

Nenda kwa wazazi wake mumeo ukwaeleze

 

[Wote]

Mwanetu kaza moyo uishi na mumeo....mumeo huyo

Ni wewe mwenyewe uliyempenda

 

Nenda, nenda kule

Nenda, nenda kule

Aa dogo......

Siki siki sikinde....

 

Rudi mwanzo  

 

 

[TUAMINIANE - Mlimani Park Orchestra]

Wasiwasi wako wa nini eee bwana  

Naona sasa huna imani nami  

Kila unaporudi kazini weeewee  

Unaniuliza maswali meeengi   

Eti nijieleze nilikuwa wapi ,  

Wakati wewe mwenyewe uliniacha nyumbani,  

Na pia hupendi niwatembelee ndugu zangu ,  

Hata maelewano yetu sasa ya taabu,(x2)   

 

(Chorus)

 

[Wote]

Tumekwisha kuwa watu wazima sasa  

Nakutafadhalisha tuaminiane aaeeh (x2)  

 

Najiona sasa sina raha mimi eeeh  

Kunisema sema kila siku bwana eeeeh  

 

Mapenzi ya kuchungana kwa kweli sio mema  

Nakusihi sana sasa tuaminiane   

Tumekwisha kuwa  watu wazima sasa 

 

Najiona sasa sina raha mimi eeeh  

Nitokapo unanipeleleza  

 

Mapenzi ya kuchungana kwa kweli sio mema  

Nakusihi sana sasa tuaminiane   

Tumekwisha kuwa

 

Ukarimu wako nauthamini eeeh  

Penzi letu pia naliheshimu  

Endapo huniamini basi (basi) 

 Iliyobaki kila unapokwenda aaaah tuwe sote (x2)  

 

Temekwisha kuwa ........  

 

Rudi mwanzo  

 

[Ubaya Uliuanza Zamani - Mlimani]

Ubaya uliuanza zamani wakati ningali mdogo

Na  haya unayoyafanya kaka

Si mageni hapa Ulimwenguni

Kaa chini ufanye uteuzi ni lipi la kufanya

Kwani ubaya haulipwi

Na pia wema hauozi  x2

 Ubaya uliuanza zamani

Wakati ningali mdogo

 

(Ngurumo)

Mambo unayoyafanya huko uliko nimeyasikia

 

Ubaya uliuanza zamani

Wakati ningali mdogo

 

(Ngurumo)

Sifahamu lengo lako tueleze tunachogombania

Ubaya uliuanza zamani 

Wakati ningali mdogo

(Ngurumo)

Kama ni kipato chatokana na juhudi zangu

UBAYA ULIUANZA ZAMANI

WAKATI NINGALI MDOGO 

[Rudi mwanzo]

[Ufukara Jeraha La Ulimwengu - Mlimani]

 Siioni raha ya dunia aaa, Roho inaninyong'onyea

Naomba fikra zinitoke nisipatwe na mfadhaiko wa akili mama aa kwa mawazo

Kuwa fukara sikupenda ....

Kwa nini iwe sababu ninakataliwa nisimuowe binti tajiri

Ama kweli ufukara jeraha la ulimwengu mama...

Jeraha la ulimwengu mama aaa

(Chorus)

[Wote]Kwa kauli yangu ya ukiwa siwalaumu enyi wakwe

[Mmoja]Siwalaumu enyi wakwe, siwalaumu enyi wakwe

[Wote]Kwa kauli  yangu ya ukiwa siwalaumu enyi wakwe

[Mmoja]Ninailaumu roho yangu kwa kumpenda binti tajiri

Nabaki na majonzi moyoni najisikitikia.....

[Wote]Kwa kauli yangu ya ukiwa siwalaumu enyi wakwe

[Rudi mwanzo]

[Naomi - Mlimani]

(kibao kilitungwa naye Max Bushoke kuimbwa naye pamoja na Fresh Jumbe,

Hussein Jume, Francis Lubua, Benno Villa Anthony, solo gitaa likiwa limepigwa na Henry Mkanyia, secondsolo na Michael Bilal, gitaa la kati gitaa, likiwa limepigwa na Huruka Uvuruge na gitaa zito la bass likiwa limeungurumishwa na Ngosha akishirikiana na Dogodogo. Drums zimekumutwa nae Habib Abbass aka Jeff kama mtakumbuka katika wimbo huu zimekumutwa barabara. tumba zimepigwa nae bwana Ally Jamwaka. Mchanganyiko wa vyombo umefanywa na King Michael Enock, hii ni kwa ufupi tu.

 (wote)

Tunzo gani jamani, nimpatie naomi nauliza eh ... x 2

kwa busara na uvumilivu alionienzi mimi,

nauliza eh .... x 2

 

(Fresh jumbe)

Kama ua lililofumba mpaka kuchanua, penzi lilianza na vikwazo chungumzima eh.....

na bahari iliyokina mawimbi yake makubwa matatizo na mateso Naomi yalimkutaaa eh ........

watu wabaya na wafitini wao hawakuridhia kwa vishawishi vidogo Naomi walimuingiiaa eh .......

kanipenda nami nampendaa.....

 

(wote)

ndio mana Naomi aliviruka vikwazoo eh ...

 

(jumbe)

Kanipenda nami nampendaaa ......

 

(wote) 

hadi hii leo penzi letu ni moja eh ...

 

(kibwagizo)

tunzo gani jamani nimpatie Naomi naulizaa eh ...

kwa busara na uvumilivu alionienzi mimi naulizaa eh ...

nauliza....

 

(Wote)

Penzi pevu la naomi ni fundisho maradufu, 

kwa wale wapendanao wasirubuniwe,

penzi pevu la naomi ni fundisho maradufu,

kwa wale wapendanao wasirubuniweee ...

 

(Fresh Jumbe)

tabia zake Naomi ni tabia tunzo la mwenye uzima,

uzuri wake naomi ni kama ua lipambalo nyumba,

busara zake naomi ningome isiyovunjika,

wanastahili sifa waliomzaa na kumlea eh eh ....

 

(wote) 

penzi pevu la Naomi ni fundisho maradufu kwa wale wapendao wasirubuniwe x 2

 

(Bushoke)

Enyi mliowazuri msikose msimamo

msijivunie uzuri na kuharibu tabia

acheni kuzurura ovyo leo huku kesho kule

hakuna atayekubali mapenzi ya kuchangiaaaaa ....

 

(wote)

penzi pevu la naomi ni fundisho maradufu kwa wale wapendanao wasirubuniwe x 2

 

(Bushoke)

We Naomi, we Naoooomi

penzi letu Naomi limekuwa kama chunusi ilowiva x 2

lahitaji kutumbuliwa ah 

na vidole viwili vyenye upeeendo we Naooomi

 

(wote)

penzi pevu la naomi ni fundisho maradufu kwa wale wapendao wasirubuniwe x 2 

 [Rudi mwanzo]

 

[Sitachoka Kukuambia  - Mlimani]

Sitachoka kukuambia hata kama tumeachana

Wafitini hawachoki kuwagombanisha wapendanao

Mengi walikueleza na wewe,

Hukuyachunguza,

Wanasema ati mume gani,

Anayekuweka kama pazia,

Kuolewa ni utumwa na tena ni kunyimwa starehe

Hebu tazama sisi wenzako tunavyoyaponda maisha

Ulipoanza shawishika

Ukaanza dai talaka

Nami nikakuruhusu bora wende ukaishi salama.....

(Chorus)

Ilikubidi ufikiri ndipo uamue, bora pazia kuliko bendara kufuata upepoooo

[Wote]

Sasa tazama umecheza PATA POTEA

Bora  PAZIA kuliko bendera kufuata upepo ooo

[Mmoja]

Ninapopata habari zako nakusikitikiaaaa

Kutwa uko kwenye mabaa na kuranda randa na njia

[Wote]

Sasa tazama umecheza PATA POTEA...........  

[Mmoja]

Mara leo Manzese na kesho upo Kinondoni,

Unajivunjia hadhi na heshima yako bure!

Sasa tazama umecheza PATA POTEA,  

Pole mkuu mwenzangu kwa yote yanayokufikaaa

[Rudi mwanzo]

[NALALA KWA TAABU - Mlimani Park Orchestra]

(Utunzi wake Cosmas Chidumule)

 

[Bichuka]

Mwenzenu uh usiku huwa silali nateseka 

Usingizi kweli sipati nabaki nahangaika

Kuyasema yote ninayaona siwezi

Yasije yakaleta udadisi kwa watu buree

Shahidi yangu ni mama watoto yee anajua 

 

[Wote]

kwani huwa aniona ninavyohangaikaaa

 

(rudia kuanzia mwanzo)

 

[Wote] Kibwagizo

naalala kwa tabu mie oh

walisema watu lisemwalo kama halipo laja (x 2)

 

[Chidumule]

ingekuwa ni ndoto wala mimi nisingejali ohh

ninawaelezea enyi walimwengu muyajua mateso yangu

 

(Kibwagizo)

 

[Chidumule]

uwaonao wazuri na wabaya ni hao hao ..... ndio bwana

amini usiamini kukuchekea sio kufurahi nawe kakaa

 

[Rudi mwanzo]

[MNANIONYESHA NJIA YA KWETU - Mlimani Park Orchestra]

(King Enoch na C. Chidumule)

Mnanionyesha njia ya kwetu

Huku mnanisimanga kua sina changu tena wala faida kwenu x2  

Hata tanga halijaishaa mnaanza kugawana mali

Ya Marehemu Mume wangu ee 

Ninapouliza yamekuaje jibu ni kwamba mnagawana mali ya mwaanenu x2  

Mbona mmesahau ya kua mali hiyo haswa ni ya watoto

Na msimamizi ni mimi Mama yao ambae leo mnanikana x2

  

Chorus

Kama ni mila tuache ooo ooo tuache kwa sababu

Madhara yake ni makubwa

(Bichuka)

Mlikua mkiniita Mkwe  ooo Wengine Shemeji

Wengine wifi ee lakini hayo mmeyasahau

Kama ni msiba ni wa kwetu sote

(Wote)

Kama ni mila tuache oo oo tuache kwa sababu madhara yake ni makubwa

(Bichuka)

Wengine huniita Shemeji

Wengine huniita wifi

Wengine huniita Shangazi

 [Wote]

 Madhara yake makubwa

[Rudi mwanzo

[Mtoto Akililia Wembe Mpe Mlimani Park Orchestra]

Cosmas--

Mtoto akililia wembe wacha umkate

Atapopata kidonda ndipo atapouogopa

Dada yetu wewe ulishaolewa lakini kwa tamaa yako

Ulikubali kuacha watoto wako ukaivuruga na ndoa yako

Kwenda kuishi na Bwana mwingine eeee

 

 

Vimekukuta vya kukukuta mwenyewe umetutangazia

Majuto ni mjukuu tukusaidie nini sema

 

Nduguzo tulikuasa na mapema kua huyo Bwana mdanganyifu

Hodari sana wa kuoa na kuacha ukatuona sisi watu fitina

Tunakuonea gere umpata Bwana mwenye pesa oooo

 

(wote)

Atakujengea nyumba

Atakununulia gari eee

Sasa unajuta

 

(chorus)

Usilie eee usilie dada

Unalia nini nawe ulisema umempata Bwana

Ataekufaa maishani mwako hello Dada hello Sister

 

(cosmas)

 

Sisi tulijua nyumba hiyo ni chambo tu

Sio kwako peke yako dada eee  

Hata hao walioolewa kabla yako wakaachika

Tunawaona mitaani kila siku  

Tunapanda nao UDA na Daladala ee

Hakuna hata kibanda walichoambulia

 

Pole dada uliyataka mwenyewe

 

 

(wote)

Usiliee  usilie dada

Unalia nini nawe ulisema umempata Bwana

Atakaekufaa maishani mwako

Hello dada hello Sister  

[Rudi mwanzo]

 

[TUFURAHI NA WANA SIKINDE Mlimani Park Orchestra]

 

Tufurahi leo , tufurahi na wana SIkinde,

Tucheze leo, ngoma ya ukae x2 

 

[Wote]kibwagizo

Ukitaka kufurahi (yoyooo) 

Kila jumamosi ( na sikinde)

Njoo uburudike na wana sikinde oyeee x2

 

 

[Bichuka]

Abeli, Mulenga, Omari na Gama ah 

George Kessy, Mwanyiro, Habibu, Machaaku x 2

 

[Wote]kibwagizo

 

[Bichuka]

Bichuka, Gurumo, Cosmas, Hamisi

Bwana Ibrahimu, Boni, Juma Townn x 2

 

[Wote]kibwagizo

 

[Bichuka]

King Enock .... ah ticha

Thomas, samweli, Joseph Benard,

Juma na Kitwana x 2

 

[Bichuka]

Hayo ndio majina ya wana Sikinde ...... oyeee

tucheze leo ndoma ya ukae

 

[Wote]Kibwagizo

 

solo la mulenga kisha sax tamuu ya Michael Enock

 

[Rudi mwanzo]

[MV MAPENZI II -  Mlimani Park Orchestra]
 
Pooooooooooooooooo,poooooooooooo
 
EEE bwana unanisikia, ndio nakusikia,Eeh endelea,  
tulipokuwa tukisafiri, Tulikutana na dhoruba,  
Eeh ,  
mawimbi yalikuwa makali sana, Eeh na bahati mbaya 
nakusikia endelea.
nahodha alikuwa muoga, akajitosa baharini
kajitosa baharini

Ndio kajitosa baharini
Lakini mabaharia kwa ushirikiano wao safari inaendelea..
 
Poooooooooo,poooooooo
 
Kuchafuka kwa bahari sio mwisho wa safari nasema,
Meli yetu ilipokumbwa na dhoruba,
Nahodha kajitosa baharini eeeeh  
 
Wale papa na nyangumi,  
Wenye uchu, wamemmeza oooh masikini x2
 
MV mapenzi meli ya wapendanao
Bendera inapepea  
Safari yaendelea x2
 
Mabaharia wenye upendo wameikabili dhoruba,
Ushirikiano na bidii
Ndio silaha yetu ya ukweli eeeh
 
Na upendo si sawa na roho
Utaona kisebusebu na kiroho papo.
 
MV mapenzi .
 
 
Rudi mwanzo  

[PATA POTEA - Mlimani Park Orchestra]
Sijui unakwenda wapi mama watoto
....................
Ni bure na unaondoka
.....
 
Kibwagizo:
 
Ohh imekuwa vigumu kwangu kusema ondoka
Na sasa ninakuambia 'ondoooka'
 
Ohhh nilicheza pata potea, ooh potea
Nlicheza pata potea , pata potea!
 

Rudi mwanzo  

 

[Penzi - Mlimani]
 
Penzi ni kati yake mke mume
 
Na hustawi kwenye Mahaba aa
 
 
Penzi ni kileo cha fikara
 
Wala usione ajabu nikipeeenda
 
 
Uliponikubalia tuwe mke na mume
 
Nilitamani Dunia isimame hata kwa sekunde moja
 
Ili niione nuru ya mapenzi yako
 
Na roho yangu iwe radhi kuwa huru

 
(Chorus)
 
  [Wote]
 
Penzi letu liwe moja
 
Lenye dhiki na faraja
 
Tukiishi vizuri ni Taji kwa wapendanao
 
 
Iliyobaki tusaidiane tulindiane heshima
 
Tuipende familia
 
Ndio kustawisha pendo

Rudi mwanzo  

[EDITA - Mlimani Park Orchestra]

Utunzi wake Hassan Rehani Bichuka na muziki kutiwa nae King Michael Enock, 

solo limepigwana Joseph Mulenga aka spoiler, rythim na Muharami Saidi bass chini yake 

Mwanyiro na sauti kali kabisa inayosikika katika wimbo huu ni ya 

Hamisi Juma aka Maalim Kinyasi.
 

(Bichuka)
kipenzi changu Edita sikia nikupe undani niliokuwa nao
kusema kweli nimechoshwa na tabia yakoo
ni siku nyingi nimeelzwa mengi niliyapuuza
nilijua ni fitina za majirani tu
wanataka kututenganishaa
 
(wote)
lakini leo nimeamini
kipenzi Edita methali ya kiswahili yasema kwamba
lisemwalo lipo
 
(sax ya Enock)
 
(wote)
nikitoka kazini sikukuti
nikuulizapo ulikuwa wapi
nilikuwa kwa shangazi Kariakoo
kumbe una wako wa pembeni kipenzi Edita
hukuridhika mpaka ulipomleta kwangu
wakati sipo nipo kazini
waweza kuchukua kila chako wende zako kipenzi Edita
 
(wote rudia)

Rudi mwanzo  

 
[USILIE - Mlimani Park Orchestra] 


Usilie eeeh dada  
Unalia nini nawe ulisema
Umempata bwana atayekufaa maishani mwako,
 haloo dada, haloo sister
 
Atakujengea nyumba, atakununulia gari eeeh,  
sasa unajuta
 
Hayo ndio watu husema  
Huku tamu na kule tamu
Sasa umebakia pachungu
 
Kibwagizo:  
 
Umebaki kuwagombanisha wenzio na waume zao
Ati wanamfuata mzazai mwenzio mama (uongo)
 
Ulipokuwa ukitumia pesa za mumeo kumstarehesha bwana
Tulikuonya mama hizo bia zitakuponza kweli
 
Umebaki..
 

Mashati na suruali za mumeo ulimpa yule kijana
Report Police Mama, umesema nguo zimeibiwa kwenye kamba

Tulikuonya mama hukutaka kutusikia kwelil
 
Umebaki

Rudi mwanzo  

[Halima - Mlimani Park orchestra]
 
Nilikaaa na Halima
Kwa muda wa siku nyingi ee
Kumbe ana mpenzi asinieleze
 
Mapenzi yaliponizidi nilinunua alichokitaka

Vitu nilivyonunua alipeleka kwa ndugu zake

Majirani walineleza mengi kuniambiaa

Sikuamini nilijua ni fitina tuu

Nilipoyachunguza

Kweli halima amenitumiaaa

ahh mara tukafarakana

(Chorus)
 
[Wote]
Halima alikwenda kumweleza mume wake
Nilkuwa namshawishi na vivutio  ili tuishi naye ee
 

[Mmoja]

Na kujitoa kila mara akipita kila mtaa kama 

MATANGAZO YA BIASHARA Halima maama eee

(x2)

Halima maama eee

[Wote]
Halima alikwenda.....

Rudi mwanzo  

 

[ISHI NA MKEO VYEMA NYUMBANI Mlimani Park Orchestra]

(Kibao kiliimbwa nae Hasan Rehani Bichuka, Chidumule, Gurumo, Maalim Kinyasi.

Solo na Abel Baltazar, Ogan ikipigwa na George Kessy Omojo, konga na Juma Town)


(Bichuka)
kwa macho nimechunguza haya ninayoyasema
na kisha nikapeleleza
ushahidi kuupata
leo mwanangu ninakuusia
hili nililonalo
kwa kuwa umekwisha kuwa na sasa umeoa

hasira nyingi ikiwa
ndani ya mioyo yenu
ikiuka kumoyo
huleta hasara
msikae vibaya ndani ya nyumba yenuu

(wote)
ishi na mkeo vyema nyumbani eh
jaribu kuvumilia
hasira muipinguze wanaa

(wote) kibwagizo
japokuwa mwagombana eh
punguza zako hasira x 2

(Bichuka)
talaka ya hasira ni mbaya sana eh
usimpe talaka subiri japo kwa mwaka hiyaaaaa

(wote) kibwagizo

(Gurumo)
kama hataki kujirekebisha
ni bora andika talaka ......... aende kwao

(wote) kibwagizo

 Rudi mwanzo

[Maneno na Wewe - Mlimani Park Orchestra] 
 
Kuna maneno nataka kusema na wewe kidogo aa
 
Ingawa nimeyasikia kwa watu walio pembeni
 
Lakini huenda yakawa na ukweli ndani
 
Kwa sababu niliowasikia ni watu wanaokufahamu bibi
 
(Chorus)

[Wote]
Watu wanasema mimi siwezi kuishi na wewe
Ingawa tumezaa
 
[Mmoja]
Kumbuka hapo zamani walitucheka
Sasa wanataka kututenganisha.....mama watoto 

 

[Mmoja tena]

Sikiliza mama watoto usinione ninahangaikaaaaa

Ninatafuta pesa

[Wote]
Watu wanasema mimi siwezi kuishi na wewe.........

[Rudi mwanzo]

 
[Hana Wema - Mlimali Park Orchestra] 
 
 
(Chorus)
 
Hana wema usimwone kucheka ooo
 
Mtendee la muhimu hataridhika
 
Apita hakusalimu moyoni kakasirika

[Rudi mwanzo]

 

[Hiba - Mlimani Park Orchestra] - Mtukwao
 
Hiiba nimelibeba pendo lako kama mwana na mbeleko,x2
Ili tuishi vizuri na kujenga familia bora, yenye thamani na pendooo, x2
 
Hiiba, imekuwaje mpenzi, mbona umebadilika aaaah,aaah
Hiiba, imekuwaje mpenzi, mbona umebadika
 
 
Kibwagizo:
 
 
Badiliko la pendo lako lanitia wasiwasi,
Lipi nililokuudhi ooh,ooh, iyo,
 
 
Ninapokuuliza wewe unanuna nunaaaa,
Ninapokuuliza hutaki kusema nami Hiba,
Ninapokuuliza hunisikii hata kidogo Hiba,
Unanisikitisha sana unapokataa kula nami Hiba
 
Hiba ooh, Hiba, [OOH MAMA]
Imekuwaje Hiba,
Hiba ooh Hiba, nieleze leo [nakupenda sana Hiba] x2
 
 
Badiliko la pendo lako.... 

[Rudi mwanzo]

[Mwanisengenya Bure - Mlimani Park Orchestra] - Mtukwao
 
Mwanisengenya bure, bwanaaa aah
Mwanisengenya bure, bwanaa aaaha,
 
Ae mnaniteta na kunisuta,
Ae mnanisengenya bure,
Aaa eeeh na mimi sijali tena sina hofu,
Mtasema mtachoka Zubeda nakwambia.
 
Hatua uliyochukua, ya kumueleza mke wangu,
Kuwa sina kitu,
Najivuna sana,
Sina umbo la kupendeza,
Wala sihitajiki,
Si urafiki tena ila,  
Ni uadui huo.
 
 
Aeeh mnanisengenya bure,
Aeeh mnaniteta na kunisuta,  
Mwisho wake mtachoka Zubeda na kwambia,
 
 
Kila nipitapo,
Mnaseeema,  
Na kusononeka,
Lipi nililokuudhi,
Au imekuwa vibaya,
Mimi kukupenda,
Na wewe kunipenda mimi,
Zubeda rafiki yangu,
 
 
Aeee mnanisengenya burea.....

[Rudi mwanzo]

[Nyimbo Unknown - Mlimani Park Orchestra] - tizedboy
 
[Bichuka]
(.......)
Utaona wanaume wengine huwapa Talaka wake zao
Huku bado wanawapenda
Mke akisharudi nyumbani kwao
Bwana anakwenda kubembeleza....
 
[Wote]
Baba na aina Mama nisameheni sana
NAMRUDIA MKE wangu talaka hiyo siitambui!
 
[Bichuka]
Akiaambiwa aangukie anatoa pesa nyingi....chuma ulete
Akiaambiwa aangukie yoooo anatoa pesa nyingi
 
Kuliko ile MAHARI aliyotoa
Kuliko ile MAHARI aliyotoaaaaaaaa.....
 
kusikilizana ndaniya nyumba eee
Ndio vizuri ii
Jamani eee, yeyeyeye
Hasira za nini eee, yeyeyeyeye 

[Rudi mwanzo]

 
[Weekend - Mlimani Park Orchestra] - tizedboy
 
Baba naomba ruhusa leo Weekend iiii
Niende kwa Wana-Mlimani
Kwani kwa mitindo yao
Waweza kucheza mwanzo hadi mwisho
Bila kuchoka aaa...............
 
(Chorus)
[Wote]
Ahsante sana Mwanangu kwa ombi lako
Sikukatazi kwenda kwani nafahamu
Kuwa siku za Weekend ni siku za furaha Mwanangu
 
[Mmoja]
Ila tu Mwanangu ninachokusihi
Unapokwenda kutembea tafadhali
Usisahau kurudia Nyumbani mamaa
 
[Wote]
Ahsante sana Mwanangu..... 

[Rudi mwanzo]

[Wimbo - Mlimani Park Orchestra] - Mtukwao
..........
Kaza roho nduguuuu,
Kwa yote yaliyokupata,
Kwa sababu ya kupenda.
 
 
Ukutanapo na mwenzio tabasamu [halooo]
Mfariji roho oooh,
Ukiweza,
Ukae ukielewa,
Kupenda sio ndoto,
Ya usiku mmooooja,
Ya usiku mmoja kaka eeeh
 
Wajue penzi ni donda la rohoni,
Lakini usichukie eeeh
 
[Kupenda ninakokupenda]
 
Wajua penzi ni donda la rohoni,
Lakini usichukie eeeh 

[Rudi mwanzo]

[KIU YA JIBU - Mlimani Park Orchestra] - Uzegeni
 

(Kibao hiki kimetungwa na Max Bushoke, kumbwa nae akishirikiana na Benno Villa Anthony,

 Fresh Jumbe, Hussein Jumbe na Fransis (NAssir) Lubua, solo limepigwa na Michael Billali, 

Rythim na Huruka Uvuruge bass chini yake Disfa (dogodogo))

 
(Bushoke)
kiu ya jibu ehh mama
kiu ya jibu ehh mama
kiu ya jibu jamani ndio inusumbuayooo
 
tafadhali nijibu jibu ambalo litanirudishia furahaaaa
ili roho yangu iweze tulia
iwe kama usiku wa mwezi mpevu
unaofarijiwa na nyotaaa
na nyotaa ah .. na nyota
 
(wote)
nilipatapo jibu nasema sito kusumbua
kumbuka hakuna binadamu duniani  
asiyejua
kutafadhalishwaaa au kutafadhalisha x 2
 
naatafuta kulala duniani
nimeechoka kulala macho na kulala macho
na kuota ndoto za Alinachaaaaa
 
(wote) rudia
 
(solo la Billal)
 
(wote) Kibwagizo
tafadhali nijibu nielewe ..... elewe
kwa sababu jibu ndilo litanihakikishia ..... mpenzi eh
umeipokea samahani yangu ewe NDUA
 
(Fresh Jumbe)
naomba uwe umeridhika kuliachia
penzi letu lichanue upya kama uaridiii
ili mahaba yatujae rohoni
tuwe kama vipepeo wanaobembelezana ... wanaobembelezana
 
(wote) kibwagizo
 
(Fresh Jumbe) rudia
 

[Rudi mwanzo]

[SOFIA - Mlimani Park Orchestra] - Uzegeni
 
(BIchuka)
Ewe Safi sikia ninayokwambia
siku nyingi tumeishi mimi na wewe
wewe ndiwe ua langu la moyoni
mengi tumeona tusibabaike
 
ewe safi elewa ninayokwambia
siku nyingi tumeishi mimi na wewe  
wewe ndiwe ua langu la moyoni  
mengi tumeona tusibabaike
 
trumpet murua
 
(wote)
kuvumiliana wajibu katika nyumba
ingawa kutenda kosa huwa vibaya
vibaya zaidi kurudia makosa
tuzidi kusikizana tuwe pamoja x 2
 
(Wote) kibwagizo
yoyoooooo Safiiiiiiiiiiiiiiii x 2
 
(Bushoke)
acha waseme seme safiiiiiiiiii
 
(wote) kibwagizo
 
(Bushoke)
mimi nawe tuyazibe masikio
 
(wote) kibwagizo
 
(Bushoke)
tumetoka mbali mimi na weeeeee
 
(wote)kibwagizo
 
(Bushoke)
tujiepushe na watu fitina
 
(wote) kibwagizo
 
(Bushoke)
we Safi we Safi we Safiiiiiiii
 
(wote) kibwagizo
 
(Bushoke)
we Safi we Safi Safi wangu
 
(wote) kibwagizo 

[Rudi mwanzo]

[Barua Kutoka Kwa Mama II - Mlimani Park Orchestra] - Ngosha
 
Ugomvi wa Baba na Mama siwezi kuingilia kwa sababu
Ndio ninaowategemea
Ingawa Rafiki zangu wananilaumu
Eti siwajali wazazi wangu
Tena ............. ...................
 
Sio kweli mimi nasema leo Nitawaeleza
 
Nakumbuka siku za nyuma

Nilipopokea barua kutoka kwa Mama

Akinipa malalamiko yake
 
Kwa uchungu niliijibu barua ya Mama
Ya kwamba nitajaribu kuyasuluhisha
Lakini ......... ........  .........
 
Chorus
Hata kama Baba ndio mwenye kosa
Nifanye nini
 
Hata kama Mama ndio mwenye kosa nifanye nini mie
Nisijekosa radhi ya Baba
Nisijekosa radhi ya Mama
 
[cosmas]
Matatizo kila mtu anayo
Mengine hufanana na mengine hutofautiana
Hebu jamani niambieni mie nifanye nini
Nisije nikachanganyikiwa
 
[rudia chorus]
 
[Cosmas]
Naepuka lawama naepuka lawama
Mimi sio mtoto wa upande mmoja

Nisimame upande gani mwenzenu
Hebu jamani nisaidieni
Nisije kosa RADHI ya Baba au Mama
Kwani wazazi ndio kitu cha kwanza elewa e
Ninayosema


[Cosmas]
naepuka lawama, naepuka lawama
kwani mimi sio mtoto wa upande mmoja
nisimame upande gani mwenzenu
hebu jamani nipeni busara zenu nifanye nini miee
nisije nikaharibikiwa
kwani duniani wazazindiyo kitu cha kwanza elewa ee
ninayosemaa eeee

[Rudi mwanzo]

[KHADIJA - Mlimani Park Orchestra] - Mtukwao
  
Nakupenda sana sherieee,
Si kwa uzuri tu ulionao,
Hata tabia zako kwa kweli ni za kuridhisha!
 
Khadija eeeh, we Khadija wa moyooo,
Nakuombea salama,
Asante sana, nasema kwa tabia zako!x2
 
Kibwagizo:
 
Tabia zako dada ni za kuridhisha,
Nikikukosa nitapata wapi mwingine,
 
Nakuomba mwana kaaa,
Utulie,
 
Tabia zako dada ni za kuridhisha,
Nikikukosa nitapata wapi mwingine,
Usidanganyike na mambo ya mjinix2

[Rudi mwanzo]

 

[KAUKA NIKUVAE - Mlimani Park Orchestra] - Uzegeni

(wote) 
mumewangu katafute kazi 
naona tabu zinatuzidi 
maisha yetu yakiwa hivi bila ya kibarua 
tutazidi kutesekaaaaaaaaaa 

onaaa hata hawa ndugu zetu 
hawafiki kwetu 
kwa vile hatuna kitu mume wangu ehhhhhhhhh 

onaaaa hata hawa ndugu zetu hawafiki kwetu 
kwa vile hatuna kitu mume wangu ehhhhhhh 

(wote) kibwagizo 
ohoo katafute kazi kwa juhudi na maarifaa X 2 

(Bichuka) 
naona aibu watoto viraka vimewajaa 
kama matangazo gazetini nawe kazi hunaaa 

(wote) kibwagizo 

(Bichuka) 
naona aibu kuvaa kauka nikuvae 
kwa jumbe kuna ngoma ... ngoma ya msondo 

(wote) kibwagizo 

(Bichuka) 
naona aibu kuvaa kauka nikuvae 
kwa jumbe kuna ngoma .. Bichu ... ngoma ya msondo 

(wote) kibwagizo 

[Rudi mwanzo]

 

[Mume Wangu Jeri - Mlimani Park Orchestra] - tizedboy

[Mume Wangu Jeri - Mlimani Park Orchestra] 

[Mmoja H. Rehani] 

Mume wangu Jeri kusema kweli 
Nimechoshwa na visa vyako 
Sitovumilia kamwe kutokana na Mwenendo wako 
Nashindwa aaa 

[Wote] 
Kila nitakalosema kwako ni baya 
Kila nitakachofanya kwako ni kibaya 
Juzi juzi ulinipiga kukuomba utulie nyumbani! 

Sijui tuishi vipi 
Raha ya Mume ni kusikilizana 
Ningechoshwa pengine 
Kama hatukuelewana ni kazi bure...... 

(Chorus)

[Wote]
Ahe ahe mke wangu eheeee 
Ohoo ohoo mke wangu eheeee 

[Bichuka]
Kutokana maneno ulionelezaaaa X 2 
Nimesikia kwa makini ohhooo 
Nakuomba radhi unisamehe 
Kwa yote niliokukosea 
Nitajireke........ nitajirekebishaa 

[Wote]
Ahe ahe mke wangu eheeee 
Ohoo ohoo mke wangu eheeee 

[Rudi mwanzo]