Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

 [Mwanzo]   

[ESTHER - Mbaraka Mwinshehe]  

Sasa nimeshatubu ewe wangu

Sinto weza rudia tena

Tumeamuliwa na wazee wetu

Yamekwisha

Kilichonizuzua siku ile

Mwenyewe nimeshaamua

Ili nikiache kuliki kukuudhi

Nisije nikajuta

Chorus...

Esta wangu sikiliza thamani ya mapenzi ni kusikilizana

Na hii leo ndiyo mwisho wangu niliyotenda kwako

Kweli yanatosha

Yote haya niliyoyafanya yamekuudhi wewe

Samahani sana, mpenzi wangu............

 

[Rudi mwanzo]

 

[Maria - Mbaraka Mwinshehe]

OOO oooo Maria ooo unanipa machungu

Mimi sikutegemea kama iko siku utakuja sema kweli sikutaki

Oooo ooo Maria ooo oo unanipa mateso

Mawazo mengi yatanipa tabu yote wafahamu tulivyozoeana

Jinsi nilivyoamini tutaishi milele mi nawe kitutenganishe kifo

  

(Chorus )

Najua utaondoka mamaa 

Utaniachia machungu ye ye ye

Fikira nyingi zitanipa tabu Maria

 

Kwa ajili ya mazoea nitakonda

Nategemea siku moja utarudi

Umetupa jongoo na mti wake pamoja 

 

[Rudi mwanzo]

 

 

[Sembuli - Mbaraka Mwinshehe]


Oooo Sembuli, ooo sembuli
Baba na mama yake Sembuli

OOOh Sembuli , ooh Sembuli

Kalale vyema ndugu Sembuli

 

[Rudi mwanzo]

 

 

[Shida - Mbaraka Mwinshehe]

Hakuna kitu kibaya sana hapa duniani kama shida
Haichagui mtu siku wala mwaka eee
Shida huja popote tena shida iingiapo bila hodi
Si mkubwa wala mdogo wote shida


Kila siku shida shida haishi mpaka siku ya mwisho ooo
Ooo Shida
tarara rarara tarara tarararara  

 

[Rudi mwanzo]

 

 

[Mashemeji Wangapi - Mbaraka Mwinshehe]

 

Mashemeji wangapi mimi nimechoka

Tena majiuliza sana wanatokea wapi?

Wanitia majonzi nakuwa na wasiwasi

Unaniweka roho juu imani nawe imeshanitoka.....

 

(Chorus)

[Wote]

Naota naota nadanganywa

 

[Mbaraka]

Kila mtu Shemeji hata yule Shemeji

Abdallah pia Shemeji?

Nia afadhali nifungue shule iitwe COLLEGE ya MASHEMEJI!

 

[Wote]

Naota naota nadanganywa.......

 

[Rudi mwanzo]

 

 

[Njooni Mnichukuee Haraka - Mbaraka Mwinshehe]

 

Majirani oneni mateso haya

Kama yeye si ndugu na baba yangu

Anavyonitesa utafikiri mtoto wa Kambo

Baba na mama fanyeni mje mnichukuwe haraka

Ooo ninakonda

 

Njooni mnichukuwe haraka

 

[Mbaraka]Kitanda kipo ananilaza chini

[Wote]Njooni mnichukuwe haraka

 

[Mbaraka]Chakula kipo ananipa makombo

[Wote]Njooni mnichukuwe haraka

 

Rudi mwanzo

 

[Kasema Hakutaki - Mbaraka Mwinshehe]
 
Hakutaki, kasema hakutaki
Amekupasulia wazi msichana
Ikiwa yeye ni wa chini yako ooo
Itakuwaje kumfukuza kazini
Eti kwa sababu hakutakiiiiiiiii!
 
(Chorus)
........
Itakuja leta hekaheka
Tafadhali iii bwana ee utakuja niponza mwokozi nani bwana eee..........

Rudi mwanzo  

 

[Nasikitika - Mbaraka Mwinshehe]

Nalia nasikitika kwani ulichokifanya ni cha dhulumaa ohhhhhh.  

Rudi mwanzo  

 

[Mapenzi Yanitesa - Mbaraka Mwinshehe]

Mapenzi yanitesa
Wazimu wanipata
Kwa kukufikiri wewe
Kama ulivyonigeuka
 
Mimi nashangaa
Najiuliza
Tumeachana lini x2
 
 
Chorus
 
Umeshalikatilii penzi langu bila kosa
Hali mimi bado nakupenda
 
Wazimu tayari sina hata la kufanya
Niko kama Bubu kwa mapenzi

Rudi mwanzo  

 

[Mahari - Mbaraka Mwinshehe]

Wajomba wamechacha wamekuja juu harusini,
Wapi mahari aliyekula hajulikani eeeh,

Wapi mahari mbona sisi hatujapata

Mwali hatoki mpaka sisi tukubali,
Tumekwisha sema bila hivyo hapakaliki eeh
[Rudi mwanzo]

HARUSI IMEVUNJIKA  - Mbaraka Mwinshehe] Ngosha

 
Ukweli nimepata nilyoyasikia sikudanganywa ooo
Kumbe huko Ng'amboni umeshaolewa na mtu mwingine
 
Nasema nasikitika kwani ulichokifanya ni cha dhuluma eee
Wazimu si wazimu huku nimebaki nalia moyoni
 
Sasa ufanye hima uwatumie barua wazazi wako eeee
Warudishe mahari yangu ili nipate tafuta mchumba mwingine
 
Chorus
 
Nawaarifu ndugu zangu wote oooo
Harusi imevunjika jama eeee
 
Niliyetaka kumuoa, amenikatalia bila kosa mwenzenu ooo

 

[Mmoja anaongea]
 
Tulia bwana Mwaruka,
Wako wengi hao,
Utampata mwingine kushinda yeye!
 
Nawaarifu ....
 
Oooo Masika solesole masika x2

[Rudi mwanzo]

[Nirudie Mama - Mbaraka Mwinshehe]  - Ngosha


Kusudi hasa unipoze moyo Mama kwa nini usinirudie 
Ingawa mimi ndio mwenye kosa nakuomba unisamehe x2 

Kukosa kokote ni kwa binadamu mwenyewe watambua Mama 

Lakini haraka urudi nakuomba ili tuwe pamoja 

Chorus 
[wote] 
Haya njoo haya njoo haya njoo Mama 
Haya njoo tuwe pamoja haya njoo Mama 

[Mwinshehe] 
Naapa shahidi naweka sintorudia tena kukuudhi Mpenzi 

[wote] 
Haya njoo haya njoo haya njoo Mama 
Haya njoo tuwe pamoja haya njoo Mama 

[mwinshehe] 
Aheri nikose kingine nikikukosa wewe nitapata kichaa 

[rudia wote] 

[mwinshehe] 

Naapa mbele ya ndugu zangu sintorudia tena kukuudhi Mpenzi 

[wote] 
Haya njoo haya njoo haya njoo Mama 
[Mwnshehe]-I swear Iswear 
[wote] 
Haya njoo tuwe pamoja haya njoo Mama 

[mwinshehe] 
Nikose redio ya sierra nikikukosa wewe nitapata kichaa 
[wote] 
Haya njoo haya njoo haya njoo Mama 
[because of love,because of love] 
Haya njoo tuwe pamoja haya njoo Mama 

[Rudi mwanzo]

 

 

[PUNGUZA HASIRA - Mbaraka Mwinshehe] - Ngosha

Niko tayari kukuangukia cherie kwa kiasi chochote ili turudiane 
Nakuomba machungu yote uyafute nionee huruma kiumbe mwenzio 

Rudisha moyo wako wote machungu yafute kabisa 
Moyo wazidi sononeka Mama hasira punguza 

Chorus 
Nimekubali kosa langu 

Nimekubali kosa langu nimeshatubu sintathubutu kurudia tena x2 

(Mwinshehe) 
Rudisha kabisa moyo wako tukae pamoja 
Sina budi kukuomba radhi Bibi eeee 

(Repeat chorus) 


(Mwnshehe) 
Nikirudia tena nikate mkono 

(Wote) Sintarudia tena 

(Mwinshehe) 
Nikirudia tena nitoe jicho 

(Wote) Sintarudia tena 

(Mwinshehe) 
Ooo Oooo Mama eeeee 

(wote) Sintarudia tena 

[Rudi mwanzo]