Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]    Rudi Table

 

[I want To Go Home - Matimila(Dr. Remmy Ongala)]

 

[Remmy]

Narudi nyumbani yooo

Narudi nyumbani

Eeeee nyumbani.....

Nilipoamua nirudi nyumbani

Nyumbani  ni nyumbani  hata kukiwa kubaya au kuzuri

Nyumbani kwako  ni nyumbani eee...nyumbani

 

Narudi Songea ooo

Narudi Matimila

Narudi Narimo

Ooooooo narudi nyumbani

Narudi Pilamio ooooo eee

Narudi Ungonini

Wangani wote mjiunge walongo vangu(Kikabila sikipati vizuri hapa)

 

Eeee nyumbani.....

 

[Wote]

I want to go home

I need to go back ho

I need to go back home

The place that is our home

Good or bad still home

(repeat x 3)

 

[Remmy tena]

Narudi nyumbani yooo

Narudi nyumbani

Eeeee narudi Majimaji

Narudi Afrika eee( x 2)

Narudi Nigeria

Eee narudi Ghana

Yooho narudi Kenya eee

Yoo narudi Uganda

Eeee narudi Gabon

Yooho narudi Congo

Eeee narudi Zaire eee

Yooho narudi Burundi

Narudi Rwanda

Narudi Majimaji

Nakwenda kula likono na la nyungu

Eee narudi Zambia

Narudi Zimbabwe

Narudi Botswana

Narudi Afrika ya Kusini

Mandela narudi nyumbani eee

Mwinyi weee narudi Tanzania

Eee narudi Tz ooo

Maricela ooo narudi nyumbani

Maricela ooo narudi nyumbani ooo

Murema narudi nyumbani

Baba Murema narudi nyumbani

Kawawa narudi nyumbani.........Salamwela eee

Kamwenye ee narudi nyumbani

Nyerere narudi nyumbani oooo x2

(kinaendele kiloingala hapa sikipati)

 

[Wote]

I want to go home

I need to go back home

I need to go back home

The place that is our home

Good or bad still home

(repeat x 3) .........

 

[Rudi mwanzo]

 

[NALILIA MTOTO - Matimila]

Nakulilia Mola wangu weee,
Nakuwaza Mola wangu wee,
Yalonipata makubwa naona balaa,
Wala hamu sina x2

Wenzangu wana watoto,
Mimi sina hata wa dawa eeeh,
Niwatumapo wana wa wenzangu,
Mama zao hunisimanga x2

Nalia nasikitika bahati sina,
Kwa waganga wa kila namna nimefika ni bure tuuuu,
Hospitali za kila namna nimekenda ni bure tuuuu,
Mola nimemuomba na sadaka nimetoa ni bure tuuuu,

Mola, Mola, Molaaa eeeh,
Mola eeeh nataka mtoto,

Mola Mola, Molaa eeh,
Mola eeh, nalilia mtoto

Mtoto angelikuwa ni nguo ningenunua,
Mtoto ni mtoto kwa mama hakui,
Hata angelikuwa kilema au mbaya kama Remmy ni mtoto tu!

Mola Mola, Mola eeeh....

[Rudi mwanzo]

 

[Mariamu - Matimila]

  (Remmy)

ataka yote akosa yote

apita ahangaika asijue la kufanya ... asijue la kufanya

mshika mawili yote yamponyoka 

apita akebakeba asijiue la kujitetea

mmmhhh mapenzi yawaka moto

naitika nilikukosea sasa nihurumie

si ninafikiri zaidi kuliko wewe

nakonda kama mnazi kwa mapenzi nilionayo

nilalapo nakuota mchana kutwa sili

moyo wanichechemea mwili damu hukauka

penzii eh ..... mmmh penzi eh x 2

 

nasumbuka kwako unionavyo moyo wangu

wewe ndio dawa yangu

Maraimu wangu 

Tanga mbali

waja leo wondoka leoo

waja leo warudi leo

 

Mariamu bibi

mwenzenu sina pumuzi kujizuwia siwezi ohhh

mwanaume barabara kazi ya mume kwa mke

neno ya mke chumvi kwa mumewe

neno ya muke kachumbari kwa mumewe

penzi oh penzi likamung'uma he heh heh

 

likamung'uma hen heh heh .... mmhhhh

mdundiko, mdundiko ........ waaaaaa

mdundiko ...... waaaa

[Rudi mwanzo]

 

[Tembea Ujionee - Matimila]
 
Tembea ujionee usingoje kuambiwa
 
Tembea tembea tembea kaka tembea ndugu uu
 

[Rudi mwanzo]

 

[MWANAIDI - Matimila]

 

(Kibao MWANAIDI kilipigwa na wana Matimila enzi hizo.

Sauti ni za Skassy Kasambula, Kyanga Songa, Fan fan na solo

ni la Batii Osenga bila kumsahau Mbwana Cox katika rythim)

 

nimetokea kumpenda binti Mwanaidi

nimeridhishwa na tabia yake

nikaamua tufunge nae pingu za maisha

urithi ulioacha baba niliutumia

ili kuneemesha ukoo wake

nilianza kuuza mifugo 

hatimaye shamba

ili kumtosholeza mahitaji yake ehhh

 

baada ya miezi michache nikapata barua kutoka kwa Mwanaidi

..... .. kuwa yeye hanitaki tena 

tena hawezi kuolewa na mimi 

 

(wote)

mimi najuta eh najuta mama

gharama nilizogharamia

ameona bure 

sijui la kufanya .. nasikitika oh

sababu yako ....... Mwanaidi x 3 

 

[Rudi mwanzo]

 

[Mwanza - Matimila] 
 
Mwanza oooh Mwanza eeeh,
Mwanza mji mzuri eeh,
Mwanza nitarudi Mwanza,
Mwanza nitakuja tena! x2
 
Mji wa Mwanza umezungukwa na milima ya mawe,
Milima ya alimasi,
Milima ya dhahabu,
 
 
Mji wa Mwanza umezungukwa na Lake Victoria,
Lenye maji bariiiidi,
Na samaki watamu wazuri,
Mwanza ooh,
 
Nalia Mwanza,
Wakazi wa Mwanza ni Wasukuma ooh,
Kabila Wasukuma,
Sukuma waaa!
Sukuma waaa!
 
 
Kutoka Mwanza tulielekea Bukoba,
Bukoba tulipokewa vizuri eeh,
Matoke kwa wingi,
 
Wakazi wa Bukoba wanasema Kihaya,
Mwabonaki waitu,
Mmmmh waitu eeeh
 
 
Mwanza oooh Mwanza eeeh
......

[Rudi mwanzo]

[Barafu Ya Moyo(Wangu)  - Matimila]  

Mpenzi wangu uu mama
Mpenzi wa moyo
Mpenzi wangu uu mama
Mpenzi wa moyo
 
Mpenzi wangu uu mama
Barafu ya moyo
Mpenzi wangu uu mama
Mpenzi wa moyo
 
Huko uliko mama unisikie
Mawazo yangu mama uyapatee
 
Mpenzi wangu........

Nakumbuka sana,
Pendo lako,
Nakumbuka sana,  
Pendo lako,
 
Huzuni tele kutwa nawaza,
Kutwa nawaza ,
Kuwa mbalimbali nawe,

Huzuni tele kutwa nawaza,
Kutwa nawaza ,
Kosa gani nilofanya,

Yelele , yelele, yelele

Mpenzi wangu mama........

[Rudi mwanzo]

 

 

[Kidogo Kidogo - Matimila] – tizedboy

 
Kidogo kidogo bwana wewe eeeeee
Kidogo kidogo baba
Kidogo kidogo
Pole pole
Pole pole mume wangu wee
 
Saa nane za usiku bwana wewe watoka wapi?
Saa nane za usiku mume wangu nambieeeee
 
Kama ni marumba, mbona peke yako?
Kama ni maraha, ulikuwa na nani bwana
 
Pole pole
Pole pole mume wangu wee
 
Nikikuulliza ulikuwa wapi Bazo
Nikikuuuliza unatoka wapi mume wangu baba watoto?
Wanijia juu kwa mateke na mangumi(x2)
Haina ujanja hiyo
Haina dawa
Haina Kinga
Haina sindano.....WAFWA
 
(Kilingala kikali kinafuata hapa)
 
Kamolewa eeee....
Kamolewa nalewa pombe

 

 

[Kifo Kifo - Matimila] - tizedboy
 
Kifo o kifo nilikuwa na mpenzi wangu
Ameniaga kwenda ng´ambo
Kifo umemchukua.........
 
Kifo umemchukua Chinyama Chiaza
Mlezi wa Maquis
 
Kifo umemchukua Mbaraka Mwinshehe
Mbaraka Mwinshehe alifahamika sana
Katika fani ya Muziki
Hata Zaire wanafahamu Mbaraka Mwinshehe
 
Kifo ungekuwa (....)
Kifo ningekupa Pesa.......
Kusudi niishi milele

[Kidogo Kidogo - Matimila] - tizedboy

 

Kidogo kidogo bwana wewe eeeeee

Kidogo kidogo baba

Kidogo kidogo

Pole pole

Pole pole mume wangu wee

 

Saa nane za usiku bwana wewe watoka wapi?

Saa nane za usiku mume wangu nambieeeee

 

Kama ni marumba, mbona peke yako?

Kama ni maraha, ulikuwa na nani bwana

 

Pole pole

Pole pole mume wangu wee

 

Nikikuulliza ulikuwa wapi Bazo

Nikikuuuliza unatoka wapi mume wangu baba watoto?

Wanijia juu kwa mateke na mangumi(x2)

Haina ujanja hiyo

Haina dawa

Haina Kinga

Haina sindano.....WAFWA

 

(Kilingala kikali kinafuata hapa)

 

Kamolewa eeee....

Kamolewa nalewa pombe

 

[Nchi Yetu - Matimila] - tizedboy

 

 

Nchi yetu ni  ya kwanza katika Afrika....Afrika

Nchi yetu ni kwanza katika Afrika kwa umoja

Nchi yetu Tanzania ni ya kwanza katika Afrika

Nchi yetu Tanzania ni ya kwanza katika Afrika

Nchi yetu ni ya kwanza katika Afrika namba one

Tanzania ni ya kwanza katika Afrika namba one

Tanzania ni ya kwanza katika Afrika hakuna mama

Tanzania ni ya kwanza katika Afrika kwwa upendo

Nchi yetu…..

Raisi wetu Ali Hassani Mwinyi

Twawapa pongezi viongozi wote

Kwa kazi kubwa mnayofanya

Kuleta umoja Tanzania…….

Tanzania, Tanzania, Tanzania, Tanzania

 

[Tuishi Pamoja - Matimila] - tizedboy

 

Bwana mdogo sogea nikutume hehe

Sogea nikutume yeyeyeye

Bwana mdogo sogea nikutume…..

 

Hee young brother come close to me

I need you come close to me Brother

I want you to take my greetings back home

Tell Mother and Father that I am still sweating in Town

 

Life in town means more money

If you don’t have money you will suffer

If no money you will never sleep

If no money you can  never eat

 

You wont even wash your clothes

 

Everbody needs money

Everybody needs more money

 

Kweli pesa pesa aaa yaaa

 

Pesa  pesa kweli inaleta balaa

Mama nalia miyeeee

Kurudi nyumbani mama tunaona haya

Mikono mitupu Mama tutarudi vipi

Tumepoteza miaka mingi mjini Darisalama

Kweli pesa pesa inaleta mambo

Kweli pesa pesa inapeleka watu jela

 

Life without money….bila ya pesa ee

No respect

 

 

 

[Kidogo Kidogo - Matimila] - tizedboy

 

Kidogo kidogo bwana wewe eeeeee

Kidogo kidogo baba

Kidogo kidogo

Pole pole

Pole pole mume wangu wee

 

Saa nane za usiku bwana wewe watoka wapi?

Saa nane za usiku mume wangu nambieeeee

 

Kama ni marumba, mbona peke yako?

Kama ni maraha, ulikuwa na nani bwana

 

Pole pole

Pole pole mume wangu wee

 

Nikikuulliza ulikuwa wapi Bazo

Nikikuuuliza unatoka wapi mume wangu baba watoto?

Wanijia juu kwa mateke na mangumi(x2)

Haina ujanja hiyo

Haina dawa

Haina Kinga

Haina sindano.....WAFWA

 

(Kilingala kikali kinafuata hapa)

 

Kamolewa eeee....

Kamolewa nalewa pombe

 

 [Masiara Sitaki - Matimila] - tizedboy


Sitaki tatizo nimeamua ni wangu
Yeye ni kipenzi mume mwenzangu nachie
Masiara sitaki nitakupiga MWEREKA