Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]        Rudi Table

 

[Baba Anna - Dar International (Marijani)]

 

Baba Anna eee

Ni lini utarudia nyumbani

Uje uwaone watoto wako

Uje uwaone baba na mama kwenu.......

(repeat)

 

[Marijani]

Najua kazi nyingi zimekuzonga...

Huko uliko nako ni MBALI sana baba Anna eeeee

Hata hivyo ufanye kila njia.....kwani kuna matatizo  matatizo  matatizo kwenu eeee

 

(Chorus)

 

[Wote]

Watoto wako wanakukumbuka...kila siku haweshi kukuuliza

Na mama naye ananung'unika....kwani miaka mingi imepita

Baba amekuwa mtu mzima...hawezi kuhangaika huku na kule

Kwa hiyo bwana ufanye haraka...matatizo yametuzidi mno yooooo

Fanya uje eeee

 

[Marijani]

Leo nasema aaa......mimi naomba.....niko peke yangu.....

Maisha ya tabu.....kila kitu ni pesa.....chakula ni pesa....

Mavazi ni pesa.....ufanye haraka...bwan naomba eee

 

[Wote]Fanya uje eeee

[Rudi mwanzo]

 

 

 

[Zuwena - Dar International (Marijani)]

 

[Marijani]

Ilikuwa asubuhi iii na mapema aaghaaa jua linachomoza aaa

Siku hiyo nilipatwa na msituko usiosemekana aaa

Niliposikia habari kumetokea na ajali ya kutisha aaa

Kwenye daraja la Salenda magari mwili iii yamegonganaaa

 

[Wote]

Yakatangazwa majina ya watu waliokuwamo kwenye ajali hiyoooo

Mmoja wapo kati ya watu hao alikuwamo mpenzi Zuwena

Nikatoka bila kujitambua mikono kichwani huku ninalia

Mbio kwenda Hospitali kwenda kumuona  mpenzi Zuwena

Sijui kama yuko hai au Zuwena amekwisha kufa

Maringo na mikogo yangu kwa siku hiyo vyote vilikwisha

 

[Marijani]

Mammy Zuwena

Ooo mpenzi Zuwenaaaa

 

[Wote]

O mpenzi Zuwena

 

(repeat Wote)

Yakatangazwa majina ya watu............

 

(Chorus)

 

[Wote]

Zuwena ningempata wapi ee

Zuwena mwingine sawa na yeye

Zuwena ningempata wapi ee

Zuwena mwingine sawa na yeye

 

Mtoto aliyeumbika mwenye tabia za kupendeza

Zuwena Zuwena kweli nampenda

 

[Marijani kwa masikitiko makubwa]

Moyo ulianza kutulia kukuta Zuwena  angali mzima

Ingawa ana majeraha mengi haidhuru mradi namuona

Zuwena Zuwena Zuwena mama aa Zuwena bibi iii kweli nampenda

 

[Wote]

Zuwena ningempata wapi ee

Zuwena mwingine sawa na yeye

Zuwena ningempata wapi ee

Zuwena mwingine sawa na yeye

 

Mtoto aliyeumbika mwenye tabia za kupendeza

Zuwena Zuwena kweli nampenda

 

[Marijani kwa masikitiko]

Sijui mimi ningefanya nini kama Zuwena angenitoweka

Tumeishi kwa muda mrefu wote wawili tumezoweana

Zuwena Zuwena Zuwena mama aa Zuwena bibi iii kweli nampenda

 

[Wote]

Zuwena ningempata wapi ee

Zuwena mwingine sawa na yeye.............

[Rudi mwanzo]

 

[Gorgina - Safari Trippers (Marijani)]

 

[Wote]

Ooo Georgina aaa

Siku uliyoondoka uluniacha nalia na machozi

Umekwenda kuishi mbali nami Georgina wa mama aaa

Sipati usingizi nikikumbuka tulivyoishi mimi nawe Georgina aaaa

Ooo Georgina.......

(repeat Wote)

 

(Chorus)

[Wote]

Umeondoka Georgina umeniachia masikitiko

Georgina Georgina oooo

(repeat)

 

[Marijani]

Nauliza Georgina oooo

Ni  lini utarudi? oooooo

Uniondoe wasiwasi...oooooooo

Georgina wa mama aaa

Georgina Georgina oooo

[Rudi mwanzo]

 

[Sauti Yako Nyororo - Safari Trippers(Marijani)]

 

[Wote]

Sauti yako nyororo naipenda unapoimba aa

Inanikumbusha mbali saana....

Hebu we Kaka imbaaa

We hapo uliye mbele .....

Natembea kila siku nakutafuta ulipo sikuoni....

Kwa nini unaniringia?

Nimevumilia sasa ninasema aaa...

 

[Marijani]

Mama na mwana

 

[Wote]

Sauti yako nyororo naipenda unapoimba aa

Inanikumbusha mbali saana....

Hebu we Kaka imbaaa..............

 

(Chorus)

Nakuooona njiani unapita lakini kukuita ninashindwa aaaaa

Naonyesha ishara hunioni!

O Kaka we wanikondesha.....

Sogea karibu yaaangu nikuone utoe sauti yako nipate sikia.....

 

O Kaka wee mwenye sura nzuri

O Kaka wee mwenye sauti njema

O Kaka wee mwenye sura nzuri

O Kaka wee mwenye sauti njema

[Rudi mwanzo]

 

[Matilda - Safari Trippers (Marijani)]

 

[Wote]

Ooo Matilda yoo Matilda tulia mama unisikiee

Mama Matilda sasa tulia umuleee mtoto wako

Matilda  mama ghaagha

Mama Matilda nakuomba nisikie punguza nyendo za usiku na mchana .

Kumuacha mwana pekee anatafuta wapi mamaye hayuko

Na siku nyingine ukalale huko huko

Huna imani matilda utaua

 

Kumuacha mwana peke yake anatafuta wapi mamaye hayupo

Na siku nyingine ukalale huko huko

Huna imani matilda utaua.....

(repeat)

 

(Chorus)

 

[Wote]

Matilda umtunze mwanao kwanza

Uhuni kwako hauna faida Matilda utaua.....

 

[Marijani]

Nakuambia mimi jirani yako Matilda

Naona uchungu aa naona uchungu

 

[Wote]

Matilda umtunze mwanao kwanza

Uhuni kwako hauna faida Matilda utaua......

 

[Marijani]

Matilda mtunze mwanao mama oo

Furaha hazina mwisho utazikuta yee...

 

[Wote]

Matilda umtunze mwanao kwanza

Uhuni kwako hauna faida Matilda utaua........

 

[Marijani]

Matilda mlee mwanao mama aaa

Kuna wenzio wanasaka mwana hawajapata

 

[Wote]

Matilda umtunze mwanao kwanza

Uhuni kwako hauna faida Matilda utaua...

 

[Marijani]

Matilda iyooo  Matilda  aaa ma Matilda  Matilda yoooo

[Rudi mwanzo]

 

[Salama - Safari Trippers (Marijani)]

 

[Marijani]

Kwa jina Salama aaaa, Salama nakuomba Salama nakuita mamaaa

Umenipa majonzi, majonzi yasiyokwisha nifanyeje mwana mamaaa

Kwa jina Salama aaaa, Salama nakuomba Salama nakuita mama aa

Umenipa majonzi, majonzi yasiyokwisha nifanyeje mwana mama aa

 

Tangu utoto tulikuwa wote, tulipendana kama wana mapacha

Tangu utoto tulikuwa wote, tulipendana kama pete na chanda aa

Nawe ulijua kama nakupenda, ukanitoroka bila kuniaga.....

 

Uwapi Salama, Salama nakuomba Salama nakuita mama aa

Uwapi Salama, Salama nakuomba Salama nakuita mama aa

 

O Salama.........

Sikia kilio changu, kilio changu cha  moyoni

Nifanye nini Salama?

Nimebaki kusikitika na KULIA .....oo Salama

 

Mama iyo yelelii uuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuuu......

 

Nikilala naota sura yako

Nikitembea nasikia waniita aaa

Nikilala naota sura yako

Nikitembea nasikia waniita aaa

 

Nageuka sikuoni Salama mama

Nauliza uko wapi Salama mama

 

Nikilala naota sura yako

Nikitembea nasikia waniita aaa

Nikilala naota sura yako

Nikitembea nasikia waniita aaa

 

Nageuka sikuoni Salama mama

Nauliza uko wapi Salama mama

 

Nalia yooo nalia mwana mama

Uwapi Salama, Salama nakuomba Salama nakuita mama aa

Uwapi Salama, Salama nakuomba Salama nakuita mama aa

 

(Chorus)

 

[Wote]

Poa o kaka poa, Poa o kaka poa,poa Salama atakuja

 

[Marijani]

Poa SIWEZI poa mpaka nione Salama

 

[Wote]

Poa o kaka poa, Poa o kaka poa, poa Salama atakuja

 

[Marijani]

Na kula SIWEZI kula mpaka nione Salama

 

[Wote]

Poa o kaka poa, Poa o kaka poa, poa Salama atakuja

 

[Marijani]

Poa ee nalia poa nataka Salama oo mama aaa

 

[Wote]

Poa o kaka poa..........

[Rudi mwanzo]

 

[Mwanameka -Dar International(Marijani)]

 

[Wote]

Kweli penzi eee, penzi lavunja udugu

Watu wakakorofishana, wakakosa kusikilizana

Penzi lavunja unyumba eee, nimeyaona kwa Musa

Mwanameka umeleta maneno, umeuvunja unyumba kwa Musa

 

Mwanameka eeee, Mwanameka jirani yangu

Mimi naona vibaya.......

Umemponza mamaye , umemponza mwenzio

Mwanameka umeleta maneno, umeuvunja unyumba kwa Musa

 

Uliposikia eee, kwamba Musa ameoa

Kaoa mke wa ndoa.......

Musa sasa katulia eee, uhuni kaweka kando

Ukatumia kila uwezo, kuyabadili mawazo ya Musa

 

Watambua eee,ukifusa(?) urembo

Ukazidisha na mapambo, vipini wanja kwa poda eee

Na mwendo wako maringo...

Musa macho yake yameona, na moyo ukaanza sononeka

 

Ukabadili na njia eee. lazima upite kwa Musa

Ukenda sokoni kwa Musa....

Musa amevumilia eee, mwisho kapotea njia

Kakusimamisha bila kutambua, akazungumza neno la mapenzi

 

Ulipopata kauli yake, ukakubali bila kusita

Uliyotaka yamekuwa......

Kazi ikawa ni moja, ni mapenzi motomoto

Umempa pendo lenye huba, maneno matamu kama asali

 

Ukichanganya na urembo wako, Musa kanasa kwenye ulimbo

Akili zake zimemruka...

Kwako wala habanduki, kwa mkewe hakumbuki

Amekwisha ionja asali, anataka kuchonga mzinga

 

Penzi nalo eee, penzi nalo halina siri

Na siri si ya watu wawili...

Mkewe Musa katambua, naye kadai talaka

Hakuliki wala hakulaliki, mpaka Musa katoa talaka

 

Baada ya kisa eeee, Mwanameka umefanya mkasa

Kweli wanisikitisha....

Mara Musa humtaki, hata kumuona hupendi

Jama Musa ameumbuka, kakosa mwana na maji ya moto

 

Kweli penzi eee, penzi lavunja udugu

Watu wakakorofishana, wakakosa kusikilizana

Penzi lavunja unyumba eee, nimeyaona kwa Musa

Mimi sasa nimeshaamini, Ibilisi ya mtu ni mtu

 

(Chorus)

 

[Wote]

Kweli Mwanameka umefanya madhambi makubwa

Mambo ulomfanyia Musa yanasikitisha

Eee Mwanameka mkasa uliofanya ni wa mwaka

Ooo bwana Musa hatokushau mpaka kufa

Tena amekwisha apa mambo ya upuuzi hataki tena

Keshaumwa na nyoka akiona unyasi anashituka

Eee Mwanameka hebu punguza matata

 

[Marijani]

Mwanameka umetuachia hadithi mitaani

Kila mmoja anashangazwa na vitendo vyako

Kila mtu anasimulia mambo yako

Ati watu mama wanasema.......

 

[Wote]

Mgombanishi....

[Marijani]

Kweli watu mama wanasema....

[Wote]

Muhuni

[Marijani]

Ati watu mama wanasema.......

[Wote]

Mdanganyifu

[Marijani]

Kweli kweli kweli Mwanameka....

[Wote]

Umezidi

[Marijani]

Oooooooo Mwanameka

[Wote]

Umezidi

[Marijani]

Mwanameka umetuachia hadithi  mitaani mama aaa

[Wote]

Kweli mwnameka umefanya madhambi makubwa.........

[Rudi mwanzo]

 

[Mayasa - Marijani]

[Marijani pekee]  

Mayasa mbona wanichana mbavu bibiye  

Sura yako mbona sasa imekuwa hivyo  

Nakuuliza mbona hata kunijibu hutaki?  

Umenikasirikia kama mimi ndio nilikutuma   

Sura yako na ulivyokasirika mama eee  

Ndio mimi wazidi kunichana mbavu Mayasa hooo   

 

Dada yako jana alipita kunieleza  

Lakini mimi hata kidogo sikumuamini  

Kanambia ulizidisha tamaa ya urembo  

Mawazo yako uwe mzuri kuliko ulivyoumbwa   

Mayasa tazama sasa ulivyobadilika aaa  

Urembo umekubadilisha sura yako ooo   

 

Nasikia ukachanganya madawa ya nywele  

Ukaona bado na mengine madawa ya ngozi  

Mchana kutwa hubanduki kwenye kioo  

Sujui mama ulitaka uwe sawa na Malaika   

 

Mayasa tizama nywele zilivyoharibika aaa  

Sura yako hapo zamani haikuwa hivyo ooo

   

(Chorus)   

 

[Wote]  

oooo Mayasa, mama Mayasa gha  

Uzuri ni wa kuzaliwa nao ooo   

 

[Marijani]  

Oo Mayasa, mama Mayasa  

Hapo zamani mama ulikuwa mwenye umbo la kupendeza   

 

[Wote]  OO Mayasa, mama ..... 

 

[Marijani tena]   

Oo Mayasa, dada Mayasa aa  

Aliyekuona zamani akikuona sasa atashangaa   

 

[Wote]  OO Mayasa, mama ..... 

 

[Marijani tena]   

Oo Mayasa, mama Mayasa aa  

Tizama sasa mama uzuri wako wa asili wakupotea   

 

[Marijani tena]   

Oo Mayasa, mama Mayasa aa  

Nakuambia mamaa aliyekuumba si mjinga   

 

[Wote]  OO Mayasa, mama ..... 

 

[Rudi mwanzo]

 

[Sababu Ya Mapendo - Dar International(Marijani)]

 

[Wote]

Sio mimi.....ni sababu ya mapendo ooo

[Marijani]

Samahani ewe mama kwa yote nitakayosema aaa

[Wote]

Sio mimi.....ni sababu ya mapendo ooo

[Marijani]

Nakuomba niwie radhi usinikasirikie mama aaa

[Wote]

Sio mimi.....ni sababu ya mapendo ooo

[Marijani]

Ukiwa na kinyongo ooo

Utaniumiza mama

Na maisha yangu....yote yataharibika aaaaa

Tafadhali nakuomba niko chini ya miguu mama aa

[Wote]

Sio mimi.....ni sababu ya mapendo ooo

[Marijani]

Mapendo o mapendo..... oo yamenizidi nguvu mama aa

[Wote]

Sio mimi.....ni sababu ya mapendo ooo

[Marijani]

Najaribu kuepuka na moyo hautaki mama aa

[Wote]

Sio mimi.....ni sababu ya mapendo ooo

[Marijani]

Nasema bila kuficha aa

Walimwengu sikieni

Yule mvulana mimi nimeshampemda

Sioni sisikii mapenzi yamenizidi nguvu mama aa

[Wote]

Sio mimi.....ni sababu ya mapendo ooo

[Marijani]

Nasema bila kuficha aa

Mwingine simtaki tena mama aa

[Wote]

Sio mimi.....ni sababu ya mapendo ooo

[Marijani]

Mnayemtaka nyinyi mbona mimi simpendi jama aa!

[Wote]

Sio mimi.....ni sababu ya mapendo ooo

 

[Marijani]

Mapenzi ni ya moyoni

Si ya kulazimishana

Mnanilazimisha aaa....mume nisiye mpenda

Sababu ye tajiri au ni kitu gani mama aa?

 

[Wote]

Sio mimi.....ni sababu ya mapendo ooo

 

[Marijani]

Kumkosa kijana yule....mimi akheri ya kufa mama aa

 

[Wote]

Sio mimi.....ni sababu ya mapendo ooo

 

[Marijani]

Kuolewa na mwingine.....siwezi kukubali KAMWE eee

 

[Wote]

Sio mimi.....ni sababu ya mapendo ooo

 

[Marijani]

Nimekubali lawama aaa

Na yote yanayosemwa

Si jambo la ajabu.....kwangu mimi kupenda aa

Si mimi wa kwanza....yameanzwa na Adam na Eva aaa

 

[Wote]

Sio mimi.....ni sababu ya mapendo ooo............

 

(Chorus)

 

[Wote]

O jama niacheni e.....mwenzenu nimeshapenda jama

Msinilazimishe! nisiyempenda sababu ya UTAJIRI wake eee

 

O jama niacheni e.....mwenzenu nimeshapenda jama

Mapenzi hayana masikini wala tajiri ni kwa mtu yeyote

 

O jama niacheni e.....mwenzenu nimeshapenda jama

Hata kama MASIKINI mimi niko radhi kuishi naye eee

 

O jama niacheni e.....mwenzenu nimeshapenda jama

Hata kama kwenye PANGO tutakwenda kuishi sote eee

 

O jama niacheni e.....mwenzenu nimeshapenda jama

Walimwengu walikwisha sema KIPENDACHO roho hakina dawa eeee

 

O jama niacheni e.....mwenzenu nimeshapenda jama

Asiyejua kupenda Mungu amsaidie yasimkute eee

(Vyombo.......)

 

[Wote]Nimependa, nimependa

[Marijani]Jama nimependa

[Wote]Nimependa, nimependa

[Marijani]Nikila sioni tamu

[Wote]Nimependa.....

[Marijani]

Sipati usingizi

[Wote]Nimependa

[Marijani]Nalala kwa tabu

[Wote]Nimependa

[Marijani]Nikilala namuota yeye

[Wote]Nimependa

[Marijani]Nikilala namuwaza ye

[Wote]Nimependa.......

[Marijani]Nalia machozi......

[Rudi mwanzo]

 

[Usia Wa Baba - Dar Internationa(Marijani)]

 

[Wote]

Mbona hamuelewani...e nyinyi watoto wangu

Mmekuwa kama si ndugu....ndugu wa damu moja

Kila mtu kashika lake...si kwa uzima wala ugonjwa

Hita nasi wazee wenu....MMETUTUPA aaa

 

Mwaniona Baba yenu pamoja na huyu Mama yenu

Sote tumekwisha zeeka....nguvu hatuna tena

Twahitaji msaada wenu....na ushirikiano wenu

Ili mpate kututunza.....hiyo kawaida

 

Mimi leo natamka...kwa makini msikilize

Kwani nimeshakasirika...mambo mnayofanya

Mjikusanye kwa pamoja...mpate kujirekebisha

Muupate wangu usia....wana mwapotea

(rudia beti ya kwanza)

 

(Chorus)

 

[Wote]

Kweli Baba, kweli Baba

Maneno tumesikia...tunajikusanya tuyazungumze...tutajirekebisha....

Tumekubali makosa....tunakuomba radhi....tutafuata usia wako Baba

 

[Marijani]

Mimi nasema UMOJA aaaa

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Umoja kwenu ni nguvu

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Wanangu shirikianeni

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Utengano ni udhaifu

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Dunia hii ni kubwa

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Ina mema na maovu

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Msipofuata yangu......wenyewe mtayaona baadaye

 

[Wote]

Kweli Baba, kweli Baba.............

 

[Marijani]Nasisitiza heshima

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Heshima ni kitu CHA BURE

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Wanangu nisikilizeni

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Kiburi si maungwana

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Muwaheshimu wakubwa

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Pamoja na wadogo

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]tenda wema uende...usingoje SHUKURANI aaa

 

[Wote]

Kweli Baba, kweli Baba..............

 

[Marijani]Usia jama usia

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Nawausia wanangu

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Msifanye FITINA!

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Kila mtu na bahati yake

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Msikate tamaa

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Riziki yenu kwa Mungu

[Wote]Ndio Baba

[Marijani]Mfanye kazi wote.....matokeo mtayaona baadaye

 

[Wote]

Kweli Baba, kweli Baba..............

[Rudi mwanzo]

 

[Paulina - Dar International(Marijani)]

 

[Marijani]

Tumetoka mbali mimi na wewe mpenzi hebu fikiria..... Paulina

Kwa tabu na raha tumezipata wote hebu fikiria ....Paulina

 

Ona leo, mbona umebadilika...nashangaa

Kosa dogo, kwako linakuwa kubwa...naumia

 

Mwanzoni hukuwa hivyoooooooooo.......

 

(Chorus)

 

[Wote]

Paulina mimi ninakuita

Nimeshayakubali makosa

Njoo mama tulee watoto

 

[Marijani] Mimi naapa...sitorudia tena....

 

[Wote]

Paulina mimi ninakuita...........

 

[Marijani]

Hata majirani wanatucheka

 

[Wote]

Paulina mimi ninakuita..........

 

Rudi mwanzo

 

[Vicky -  Dar International(Marijani)]

 

[Wote]

Vicky mtoto wa mama aaa

Mbona siku hizi umeadimika

Hata kwenye magoma hutaki kufika

Hebu nijulishe Vicky eee Vicky ee

Si kawaida yako Vicky ee Vicky eeee

Naona si bure Vicky eee Vicky eee...una neno

(repeat)

 

[Marijani]

Usinikondeshe bure mwana wa mwenzio

Wakati wewe mwenzangu hata hunijali

Hebu nijulishe Vicky ee Vicky eee...nijue Moja

 

[Wote]

Vicky mtoto wa mama aaa ....

 

[Marijani]

Vicky ungenijulisha mapema.....

Niweze kumtafuta mwingine

Awezaye kulisakata Bomboka

Super Bomboka eee kwa wazee na vijana

 

[Wote]

Vicky mtoto wa mama aaa ........

[Rudi mwanzo]

 

[Lila Ninachoka - Dar International(Marijani)]

 

Ooo Lila nachoka Mama aaa 

Kuvumilia sintoweza 

Tumeishi siku nyingi 

Hata siku moja hukusema ............. 

Niambie ukweli Mama aaa 

OO Lila sasa nachoka Bibi  

 

(Chorus)

OOH Lila niinachooka,  nisamehe mume wangu, 

Hapana hapana mamaaa 

Ningoje kwanza nitubu,  

Ooh binadamu yeyote hukosa 

Ukiniacha nitakwenda wapi, 

Nitasema nini nyumbani kwa wazazi eeeh mama!   

 

Asubuhi nakwenda kazini  unaatoka kunyumba eeh 

Unaacha watoto hata chakula kupika 

Na mlango umefunga eeeh funguo umechukua  

Unalia iiihhhhh oooh ohhh 

Oooh ninachokaaaa (Nisamehe mume wangu)  

Hapana hapana mama

 

Rudi mwanzo

 

 

[CHRISTINA - Dar International(Marijan)]

 

 Asante sana Asante sana Mwana Christina  

Sikutegemea kama utafanya ulivyofanya  

Kunidanganya nakupenda Bwana  

Nami Mwenzio nikakupenda  

Hata Wazazi wakatambua aa kweli kama nakupenda   

Hata posa nilipeleka na mambo yote nikamaliza  

 

Ikabaki tufunge ndoa mi nawe ukanitoroka (x2)  

 

(Chorus)

 

[Marijani]

Ooooo Mama   

 

[Wote]

Christina Mapenzi yako yanipa wazimu   

 

[Marijani]

Na dada   

 

[Wote]

Christina usiku kucha siwezi kulala   

[Marijani]

Mapenzi yako yanipa wazimu usiku kucha siwezi kulala  oo lala   

 

[Wote]

Christina mapenzi yako yanipa wazimu   

 

[Marijani]

Nani aliyekudanganya akabadili mawazo yako Bibi   

 

[Wote]

Christina usiku kucha siwezi kulala   

 

[Marijani]

Jamani   

 

[Wote]Christina mapenzi yako yanipa wazimu  

 

[Marijani]

Tumependana sanasana Mpenzi mpaka sasa kuoana Bibi   

 

[Wote]

Christina usiku kucha siwezi kulala   

Nakonda nakonda Bibie   

Christina usiku kucha siwezi kulala 

 

Rudi mwanzo

 

[MASUDI - Dar International(Marijani)]

 

(Fresh Jumbe alishiriki kikamilifu kabisa katika ukamilishaji wake

 na sauti yake inasikika vyema. Kama kawaida solo limeshikwa na Mahdi Tumbo. 

wimbo huu unasax ambazo zimepigwa vyema kabisa na huyu jamaa 

alikuwa akiitwa Seif sijui aliishia wapi huyu jamaa)

 

[Marijani]

Wanangu mimi nawakumbusha mnapopata rafiki  muangalie vizuri ihhiii ....

wanangu  kuna urafiki mwengine wa kweli  na urafiki mwengine wa kupotezana ... wanangu   

 

[Wote]

Angalia yasije yakawakuta mambo yaliyomkuta  mwenzenu masudiii  

Masudi kapata marafiki oh marafiki wamempotezaaa   

Masudi amehuni nyumbani na vilevile shule  hataki kusoma  

Inapata mwezi wa tatu wazazi wake nyumbani hawajamuona   

Haijulikani analala wapi  wala haijulikani anapokula   

Anapita akizura ovyo wala kazi yeyote hataki kufanya  

Anapenda mambo makubwa wakati yeye mwenyewe lolote hana   

 

Masudi amekuwa hashikiki  wala hana yeyote anayemsikiza   

Wazazi wamesema wamechoka sasa wamebakia wanatizama macho loh   

 

(Chorus)

 

[Wote]

Masudi amekuwa jambazi  ukikutana nae usiku mpitie mbali 

Kama si hivyo, atakudhuru baba

 

[Marijani]

 Anisikitisha kweli anisikitisha kijana Masudiii  

Mambo yake vitendo anavyovitenda mimi haviniridhishii  

 

Masudi amekuwa kwapukwapu  

Mapesa mfukoni kachomoa  

Ukivaa saa nzuri kwapu kwapu  

Vitambaa vya kichwani kwapu kwapu  

Stendi ya basi ndio kwake ......

 

Anisikitisha kweli anisikitisha kijana Masudi  anisikitisha babaa   

 

[Wote]

Masudi amekuwa jambazi  ukikutana nae usiku mpitie mbali 

Kama si hivyo, atakudhuru baba

 

[Fresh Jumbe]

Siku moja alikuwa hana kitu mfukoni  

Akaamua kuvunja nyumba ya watu  

Alikamatwa Masudi akapigwaa karibu ya kufa na sasa amefungwa Masudi   

 

[Wote]

Masudi amekuwa jambazi  ukikutana nae usiku mpitie mbali 

Kama si hivyo, atakudhuru baba......

 

Rudi mwanzo

 

[Ukatini Ni Unyama - Dar International(Marijani)]

 

Kweli dunia ina watu wengi na mambo tofauti

Kuna wakatili na wengine wenye huruma

Kuna wadanganyifu na wapenda haki

 

Watu wengi hupata sifa kwa ukarimu wao

Na wengine hupata sifa kwa ushujaa wao

Wengine hulaanika kwa ukatili na ushenzi wao

(repeat)

 

(Chorus)

 

[Wote]

Kila mtenda wema ee atakumbukwa kwa wema e(x3)

Ukatili, ukatili ni unyama ee (x2)

(repeat)

 

[Marijani]

Mashujaa tutawakumbuka kwa wema ee

Mlokubali kujitoa muhanga ee

(repeat)

 

Kwa ajili ya kutetea haki zetu ee

Kwa ajili ya kutetea utu wetu ee

Afadhali ya kufa kuliko kuonewa ee

Afadhali ya kufa kuliko kunyanyaswa

Mashujaa tutawakumbuka daima ee MILELE......

 

[Wote]

Kila mtenda wema e atakumbukwa .............

 

[Marijani]

Makatili tunawapiga lana ee.......laana kuubwa.....

Watu gani wasio na huruma ee

(repeat)

 

Kuzitoa roho za watu bila sababu ee

Hata watoto wadogo wamekosa  nini ee?

Mtakwenda sema nini mbele ya Mungu ee(x2)

Makatili tunawapiga lana ee....laana kuubwa.....

 

[Wote]

Kila mtenda e atakumbukwa kwa wema.............

 

Rudi Mwanzo

 

 

 

[NAMSAKA MBAYA WANGU - Dar International(Marijani)]

 

( Fresh Jumbe alikuwamo katika sqadi la wana Supa Bomboka Dar International, 

kibao hiki kimetungwa nae Marijani Rajab, kuimbwa nae akishirikiana na

Fresh Jumbe na Benno Villa, solo linapigwa na Mahd Tumbo ambaye alilicharaza barabara)

 

[Marijani]

Nani kaenda kwa mama Maria? ..... 

Mama Maria  na kuzusha maneno ya uongo ....... mama Maria  

 

Kenda kuueka uhasama  kina mtaani kuchukiana oh jamani eh   

 

[Wote]

Hao ndio wenye kukaanga mbuyu  kuwaachi wenye meno watafune (x 2 )

 

[Marijan]

Ilikuwa saa za usiku ...... mama Maria  

Mbaamwezi na nyota zinaangaza ... mama Maria  

Mama Maria kafunga kibwebwe,  kaja nyumbani kwangu kunitukana bila sababu   

 

[Wote]

Hao ndio wenye kukaanga mbuyu  kuwaachia wenye meno watafune (x 2 )

 

[Marijan]

Nikamuuliza ah mama Maria ... mama Maria  

Vipi kutoka kwako kuja nitukana .... mama Maria  

 

Akanambia amepata habari ........ mama Maria  

Ati mimi ndie ninamzuzua mume wake   

 

[Wote]

Hao ndio wenye kukaanga mbuyu  kuwaachia wenye meno watafune (x 2 )

 

[Marijani]

Nikamuelezaa ah mama Maria ...... mama Maria  

Watu fitina walivyo mambo yao ..... mama Maria  

 

Nikaapa kwa jina la Mungu ......... mama Maria 

Kkwamba mumewe sina habari nae hakukubali   

 

[Wote]

Hao ndio wenye kukaanga mbuyu  kuwaachia wenye meno watafune (x 2 )

 

[Marijani]

Nani kaenda kwa mama Maria  na kuzusha maneno ya uongo  

Jamani mimi nikimtambua  itakuwa ama zake ama zangu leo nasema   

 

[Wote]

Hao ndio wenye kukaanga mbuyu  kuwaachia wenye meno watafune (x 2 )

 

(Chorus)

 

[Wote]

Oh oh mama Maria embu punguza hasira  

Namsaka mbaya wangu anayetugombanisha  

Siku nikimuona  mambo tutasawazisha  

Kweli nikimuona oh mambo yatawaka motoo   

 

[Marijan]

Ama kweli walimwengu babaa  hatuna wema wala shukurani hiii  

Ukiiishi na watu vizuri  watafitini ili mugombane jamaa  

Ukiwa huelewani na watu watasema sijui mtu gani  fitina mama oh   

 

[Wote]

Oh oh mama Maria embu punguza hasira

 

[Marijani]

Ukiwa unajimudu kidogo  walimwengu watasema anaringa .... sana  

Ukiwa mwana wa masikini  watakudharau na kukucheka..... kachaacha  

Ama kweli walimwengu jama hatuna wema wala shukurani  fitina mama oh   

 

[Wote]

Oh oh mama Maria embu punguza hasira..........

 

Rudi mwanzo

 

[Dunia Imani Imekwisha - Dar Internationa(Marijani)]

 

(Chorus)

 

[Wote]

Dunia sasa imani imekwisha

Nyoyo za watu zimebadilika

Si wanawake, si wanaume

Sote tunakwenda musomba musomba

Penye watu kumi binaadamu mmoja

 

[Marijani]

Hasa ulaghai ndio umezidi

Watu wamezidi kudhulumiana....

 

[Wote]

Dunia sasa imani imekwisha.........

 

[Marijani]

Bwana Uledi kaachiwa duka

Mwenyewe kaenda Kilwa Kivinje

 

Bwana Uledi kasema sasa watanikoma!

Hasa yule Sauda atanitambua

 

Kapita Sauda kamuhonga Unga

Karudi jioni kapewa Sukari

 

Siku mbili tatu duka limefilisika

Uledi kaiba pesa na vitu vyote kapotea.....!

 

[Wote]

Dunia sasa imani imekwisha.........

 

[Marijani]

Fundi Cherehani kaletewa vitambaa

Mwenyewe kataka suruali tatu

 

Fundi kasema:

[Fundi] " Hewallah vimefika"

 

Wiki imepita mwenyewe kafika

Anauliza:

[Mwenyewe] " Fundi wapi suruali zangu?"

Fundi analia:

[Fundi] Yoyoyoooyo

 

Anaulizwa:

[Mwenyewe] "Fundi walia nini?"

 

Fundi anajibu:

[Fundi] "Ooo zimeibiwa"

 

[Wote]

Dunia sasa imani imekwisha.........

 

 

Rudi mwanzo

 

[UKEWENZA - DAR International]

 

[Marijani]

 Kweli Mama Fatu nilipokuona

Sikuamini macho yangu

Nilikua kama nipo ndotoni,Mama Fatu shoga yangu

Ama kweli hujafa hujaumbika

Naamini ya Walimwengu

Jinsi umbo lako lilivyobadilika ni masikitiko kwangu

 

Hebu nieleze umepatwa na swahibu gani x2

 

[wote]

Yoo ukewenza,kweli ukewenza una mambo

Ama kweli nimeona vituko,mnitizame nilvyokondaSababu ya ukewenza

 

[MARIJANI]

Ukewenza jama sitaki tena sitaki Mama

Tena nimekoma hata kulisikia hilo neno sipendi

Ukewenza ni ufahari kwa Mwanaume kwetu ni tabu

Hata mwanangu Fatu akiposwa na mwenye Mke sikubali

Ukiolewa bora ukute Mke mwenzio mwenye imani

Kama si hivyo ndugu yangu utajuta

Hebu nitizame mwenzio mambo yalonikuta

Ukewenza mimi hapana,mimi hapana,hapana

Ukewenza mimi sitaki jama sitaki

 

(RUDIA WOTE)

 

[MARIJANI]

Ukwenza kweli hatari we Mama

Akina Baba wanatuletea janga

Fahari yao sisi matatizo

 

Rudi mwanzo

 

 

[NDOA YA MATESO - DAR International]

 

[Marijani]

Niulizieni enyi walimwengu

Huyu Mwanaume anavyonitesa

Hii ndio haki au ni mateso(x2)

 

Kanitoa kwetu kwa Baba na Mama

Kwa vigelegele na heshima nyingi

Tizameni sasa anavyonigeuka(x2)

 

Ananipa mateso huku ugenini

Sina hata ndugu wa kunisaidia

Na mimi na watoto jamani tabu gani(x2)

 

Kwani kuolewa ni jambo la ajabu

Au kuolewa ni sawa na utumwa

Kama ndio hivyo mimi nimeshindwa(x2)

 

Natoa ushahidi kwa wewe Mjumbe

Mwambie huyo Bwana anipe talaka yangu

Nisije kuondoka ikawa maneno(x2)

 

[WOTE]

Mambo anayoyafanya ni aibu kusema

Kwa kua leo nina uchungu nitakueleza

Hapa unapotuona hatuna chochote nyumbani

Mume wangu haonekani sijui yuko wapi

 

Anababaishwa na anasa za mjini 

Bibi kanitupa na watoto hawajali

Pesa zake zote zinaishia nje

Kwa makuku ya kukaanga

Mimi na mkate mkavu

 

Nimechoka mimi na Mwanaume mlevi

Heri anipe talaka mimi nirudi kwetu

Sikuzaliwa juu ya miti

Ninako kwetu(x2)  kwa Baba na Mama

 

CHORUS

(WOTE)---Mateso,mateso mateso yamezidi nachoka

(MARIJANI)

Pole Mama kwa tabu unazopata

Lakini kwanza usichukue hatua hiyo mama

Chorus--mateso---------------

 

(MARIJANI)

Mimi na Wazazi wake tutamwita tumkanye

Akirudia mimi nitakua shahidi yako Mama

Mateso.............

Naona vibaya mmeshazaa watoto

Mkitengana mtawapa tabu watoto wenu Mama

Mateso, mateso,mateso yamezidi nachokaa

 

Rudi mwanzo

 

[Pendo - Dar International(Marijani)]

PENDO!(wote)

Pendo !pendo! kulazimishana !

pendo pendo yafaa kulingana!

Marijani:

Uzegeni kamuoza mwanaye kwa baba Hamisi!

Sababu Hamisi hajambo kidogo

Ana nyumba tatu na kiunga cha minazi

PENDO!(wote)

Pendo !pendo! kulazimishana !

pendo pendo yafaa kulingana!..........

 

Rudi mwanzo

 

[Magreti - Safari Trippers(Marijani)]

 

Magreti mama shangazi yako anakuita yooo

Ukamwone mama, mama yako anaumwa sana

Tena Magreti msikize wako shangazi yoo

Anayosema ukipuuza mama yako hutamkuta

Utamlilia nani wakati baba yako naye, ameshakutoka Magreti ii

 

(Chorus)

 

[Wote]

Kukaa kwako mjini faida yake umeiona....iona

Wazazi wako wawili sasa wameshakutoka

 

[Mmoja]

Tazama sasa hali yako imebadilika

Tazama sasa mambo yako yameharibika

 

[Wote]

Kukaa kwako mjini faida yake umeiona....iona

 

[Marijani]

Shangazi yako naye alikusihi sana aaa

Kuja kumwona mama

 

[Wote]

Magreti ukapuuza........

Aaa kukaa kwako mjini faida yake umeiona...iona.....

 

Rudi mwanzo

 

[Rufaa Ya Kifo - Dar International]

Kama ingalikuwaaa, binadamu anakata rufaa ya kifooo,ohhh, 

inapotokeaaaa, mbele ya Mungu na mimi ningekataa rufaaa, 

nirudishiwe wanguuuu niliyempendaaaaa 

hapa duniani lakini ninashindwa sijui nifanyeje

 

 Chorus:

Lakini Mola yeyeyeeee,

Kazi yake haina makosaaa, (kweli haina makosa)

Wala hairekebishwi na binadamu yeyote

 

Yeye ndiye muumbaaaeee, yeye ndiye muwezaaaa

Analotaka amuaaaee, eeeh huwa eee

 

Lakini Mola yeeyee

 

Nalia mimi nalia eehh, huzuni nyingi huzuniii(pole)

 wangu umeondoka umeniacha mkiwa eeh

 

Lakini Mola yeeyee

[Rudi mwanzo]

[Dunia Tambara Bovu - Dar International(Marijani Rajab)]

 Sadiki leo nimerudi kwako

naanguka chini ya miguu yako

nakuomba urudishe moyo wako babaa mpenzi sahau yaliyopita,

shoga zangu ndio walinipoteza sadiki mpaka tukafika kutengana mimi na wee 

Sadiki sadiki oh oh ninakuombaa baaba sadiki sadiki ohoh fanya huruma baaba

 [Rudi mwanzo]

[KUMEKUCHA Dar International(Marijani)]

 

(wote)

kumekucha sasa kumekucha

majogoo vijijini wanawika

na sasa jua mbinguni linatoka 

wazalendo amkeni tufanye kazi sasa x 2

 

oh oh mama ...... twende mbele

oh oh ohooo ..... twende mbele sasa tusonge mbele

kwa majembe mabegani tuende mbele 

na mapanga mikononi tusonge mbele

sote twende vijijini tukalime sasaaa  

*******

 

[SIKITIKO Dar International(Marijani) ]

 

Kweli sikitiko, sikitiko,

Kweli sikitiko linatupata mama,

 

Kusema ukweli tukikumbuka mama,

Na machozi yanatutoka, ( kusema kweli)x

 

Tukiona wale wenzetu wanateseka maaamaa,

Wako katika makucha ya watu weupe wachache,

 

Watu wasiothamini utu wa mtu,

Watu makatili kwa roho za watu

 

Marijani:

 

Wanawaua ndugu zetu kama bila kosa,

Wanawaua ndugu zetu kama wanyama,

Na huku makaburu wanafurahia yoyo

 

 

Witooooooo ( witoooo) ,

 

Afrika lazima tuikomboe 

(Lazima tuikomboe)

Makaburu tukawakatekate mama,

Lazima tuikomboe,

Kwa bunduki na mikuki na mapanga mama 

Lazima tuikomboe,

 

Iyoo mama lazima tuikomboe maama

Lazima tuikomboe  

**************

 

[MWAJUMA - Dar International(Marijani)]


Marijani: Jamani mimi naimba, Naimba na masikitiko
Wote: ( ooh na masikitiko)
Marijani: Anisikitisha Mwajuma alivyo hana mapimo
Wote: Ohhh hana mapimo


Wote: Mwajuma anaelewa ya kwamba,
mumewe kipato chake kidogo
Hivyo inawabidi ya kwamba
Waishi kufuatana na uwezo


Marijani: Lakini sivyo anavyofanya Mwajuma,
Mwajuma hajui kupata wala kukosa
Tamaa nyingi ndio kaweka mbele
Na mambo mengine yamemzidi kimo


Oooh Mwajuma pesa hupatikana kwa taabu,
Oooh Mwajuma pesa hupatikana kwa jasho,

Wote : Wanaishi nyumba ya kupanga,
Kila mwezi ni kodi ya nyumba,
Watoto wanataka matunzo,
Mwajuma wala habari hana,


Marijani: Akili yote kwenye urembo na mapambo,
Kuchunguzana leo mwenzangu kavaa nini,
Akiona mwenziwe leo kapata khanga,
Lazima na yeye akadai khanga,
Hata kama mumewe yuko kwenye muambo,
Atalazimishwa aende akakope,


Kama si hivyo,
Nyumbani hakulaliki,
Malalamiko na maneno chungu teleeeee,


Rudi mwanzo


 

[MANENO MANENO - Safari Trippers(Marijani)]

Aaa Mummy nasikia maneno maneno
Watu wengi wanakusonga na maneno maneno
Ya kukutia uchungu eee eeee usiwajali eee maua

Mimi na wewe tuonyeshe mapenzi ya ukweli
Hao fitina waache na fitina zao ee eee
Waseme wachoke ee ee ee
Mimi ni wako ooo ooo maua

Chorus
Hao hao watu fitina
Hawapendi wawili wakipendana
Kazi yao kubwa maneno ya uongo uongo

Kila kukicha utawaona njiani
Ukiwaonyesha neno dogo kwao ni kubwa
Kazi yao kubwa maneno ya uongo uongo

 

 Rudi mwanzo

[Jina Lako Chakubanga - Marijani]

 

[Marijani]Ulipochaguliwa

[Wote]Kwenda ng'ambo

[Marijani]Mwisho wake bwana

[Wote]Mambo yalikuwia magumu

[Marijani]Mwendo umebadilisha

[Wote]Bega moja umelishusha

 

[Marijani]Jina lako Chakubanga

[Wote]Unajiita John Smith

[Marijani]Mwana vibaya

[Wote]Vibaya mwana vibaya aaaaa

 

(Nimesahau mpangilio lakini baadaye wanaimba maneno kama hivi:)

 

[Marijani]Mama kaondoka

[Wote]Analia mama analia

[Marijani]Anaona uchungu

[Wote]Analia mama analia

 

Rudi mwanzo

 

[Mama Usinung`unike - Dar International(Marijani)]
 
Mama nakuomba, usinung`unike,
Fikiri naye ana matatizo x2
 
Kwa tabia zake dada ninavyomuelewa,
Hawezi kupuuza, shida za wazazi,
Uongo, Uongo x2
 
Kibwagizo:
 
Usiwe na hasira eeeh,
Za haraka haraka,
Na kumlaani mwanao ooh,
Ewe mama ni dhambi x2 

Rudi mwanzo

 

[MAMA Watoto - Dar International(Marijani)] 
 
Mama watoto,
Acha roho mbaya,
Nakusihi mama, nakuomba,
Au kwa sababu wazazi wake, wametoweka,
Si kosa lake mwana hiyo ni kazi ya Molaaa,
Huyu ni mtoto sawa na watoto wako,
Hebu fanya huruma ,usimtese mwana
 
Oh mama watoto, usimtese mwana,
Ohh mama watoto,
 
 
Mama nasema aaah,  
OOhh mama watoto,
Usimtese mwana,
Ohh mama watoto,
 
 
Majirani wanalalamika,
OOh mama watoto ooh
Usimtese mwana,
Ooh mama watoto.
 
 
Kibwagizo:
 
Mama watoto muogope Mungu wako,
Kwa huyo mwana asiye na mama,
yeye hakuomba ila ni kazi yake Mungu,
Kazi ya Mungu haina makosa x2
 
Marijani:
 
Uhai, uhai umeumbwa  
Na kifo vilevile kimeumbwa,
Usisahau na wewe pia ni kiumbe,
iko siku yatakuja kukuta,
 
 
Aiyo aiyo maama,
 
Wote:
 
Mama watoto muogope Mungu wako,
Kwa huyo mwana asiye na mama,
Yeye hakuomba hiyo ni kazi yake Mungu,
Kazi ya Mungu haina makosa.

 

Rudi mwanzo

[SIWEMA I - Dar International(Marijani)] 
 
Siwema, usinipe mateso ya moyo,
Na sasa nimechoka, ukweli nasemaaa aah,
Nia na madhumuni yako,  
nimeshavitambua siwema dada,
Najiepusha nawe, maaamaa ahaaa
 
 
Unajitapa, mbele ya rafiki zako,
Kwamba mimi sina la kusema mbele yako,
Umeniweka kwenye kiganja,
Unalotaka, ndilo ninalofanya,
Sababu wewe ni mzuri sana,
Siwezi kupata mwingine kama wewe,
Siwema dada unajidanganya.
 
 
Kibwagizo:
 
Nimezunguka Tanzania Bara  aaah
Unguja na Pemba nimefika aaah
Nimewaona warembo wenye sifa aa
Wenye kujipamba wakapambika
 
Kwa hiyo unielewe hivyo dada
 
Sibabaishwi na sura aa
Napenda Tabia njema aa
 
Tabia njema ndiyo silaha kwako
 
Sibabaishwi na sura aa
Napenda Tabia njema aa
 
Kila mtu atakupenda dada
 
Sibabaishwi na sura .....
 
Usifikiri mimi limbukeni dada
 
Sibabaishwi na sura aaah
 
Kweli dada, kweli dada,


Sibabaishwi na sura aaah,

Rudi mwanzo


[SIWEMA II(SADIKI) - Dar International(Marijani)] - Mtukwao
 
Sadiki leo ninarudi kwako,
Naanguka chini ya miguu yako,
Shoga zangu ndio walinipoteza,
 
Walinambia tembea uone mambo,
Anakuweka ndani kama pazia,
Mtoroke..........
..................
 
 
Sadiki yooo, sikutamka baba,
Sadiki yooo, fanya huruma baba.

Rudi mwanzo


[Nyota Njema - Dar International(Marijani)] - Muhanga


nyota njema imewaka

mambo yangu yamenyooka

maisha yamebadilika, baada ya dhiki faraja
Lakini bado nashangazwa, jirani yangu kakasirika,  
hata jambo hataki kunipa, sijui nililomkosa
 
anacheka jino pembeee moyoni anasononeka,
kwa nini huyu yupo hivi nami nipo moyo wamuuma.
Alitaka niwe duniii wala nisiwe nathamanii
lakini matakwa yake na jitihada zake hazishindi kudura
pilipili asoilaaa yeye inamuwashia nini?
kupata kwangu au kukosa hakumpunguzii wala hakumwongezei
anasahau hata munguuu baba  kwamba yeye ndiye mtoaji,
Jirani angepewa jukumu la kugawa riziki ingekuwa vipi  
 
Hunichunguza kwamba mimi nakula nini
hunichunguza kwamba mimi navaa nini
kuvaa na kula kwangu wakutakia nini
 
Hata kama nashindia uji wa change

hata nikila kuku kwa biriani haya yote jirani hayakuhusu weee
 
Hata kama mimi ninavaa kaniki, hata kama nikivaa suti yapande tatu

haya yote mwenzangu hayakuhusu weee
 
nilipokuwa sina kitu hata humunijalii, na kazi ninayoifanya haukuithamini,
ulisema eti bure na hangaika, wala sina lolote ninalopata mieee
baada ya dhiki mungu kanikumbuka, sasa mbona jirani wanisakama buree
 
 
ooooo jirani ooooooooooo jirani oooooooo jirani mbona wanionea bureeee
unanisakama bure jirani

Rudi mwanzo

 

[Ndugu Umepotea - Dar Internationa(Marijani)] - tizedboy

 

[Wote]

We kipenzi cha Mama eee

Ewe Ndugu yetu Kitinda-mimba

Hebu tizama unavyofanya Kaka aa

 

Mbona nakuona unapotea

Mama naye mapenzi kazidisha kwako

Hata kukukanya anashindwa

Anakuacha ufanye unavyotaka Mamaa

 

Sasa imebidi nikueleze

Nakuambia kama mimi ni Kaka yako

Ingawa natambua unanidharau

Lakini mimi ndio nimeona Dunia mwanzo

 

[Marijani]Naona unapotea

 

(Chorus)

[Wote]

 

Mzee Saidi ee

Alikuja lalamika haaa eee

Kasikia fununu kwamba unavuruga Nyumba za watu

 

Kaja kutoa onyo

Anasema Kijana ole wako

 

Nasikitishwa sana ndugu yangu kuwaza mambo hayo

Umefanya mambo mengi

Lakini hayo yamezidi kipimo

Mchezo na Nyumba za watu

SAWASAWA KUCHEZA NA MOTO!

 

[Marijani]Wacha wacha mara moja

[Wote]Hatari kubwa

[Marijani]Utapoteza Maisha Baba

[Wote] Hatari kubwa

[Marijani]Wewe ungali Kijana mdogo

[Wote]Hatari kubwa

[Marijani]Hujaiona Dunia baba

[Wote]Hatari kubwa

[Marijani]Chonde chonde nakuomba Baba

[Wote]Hatari kubwa

Rudi mwanzo

 

[Pesa Sabuni Ya Roho - Dar Internationa(Marijani)]  - tizedboy

(.......) 
(Chorus) 
Pesa Pesa, Pesa ndio Sabuni ya Roho 
Mwenye Pesa, mwenye Pesa sio mwenzio 
Nasema............ 

[Marijani] 
Mwenye Pesa akipita watu wote husimama 
Shikamoo Mzee 
Jamani Pesa.......... 

(Chorus) 
Pesa Pesa.......... 

[ Alinacha - Dar International(Marijani)]  - Mtukwao


Alinacha zitakuponza wewe, 
Unawaza pesa, mamilioni, 
Gari kubwa na nyumba nzuri ( ajabu) 
Hata kazi huna! 

Kibwagizo: 

Chanzo cha nyumba nzuri na gari uwe na pesa, 
Sasa pesa utapata wapi bila kazi, 
Fanya kazi ujenge taifa Alinacha ee 

Fanya kazi hiyox4 

Sisi sote tumeumbwa kuhangaika eeeh, 
Hangaika usikate tamaa Mungu anakuona, 
Iko siku utafanikiwa kama wenzio eeh 

Fanya kazi hiyox4