Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]    Rudi Table

 

[KASHALA  -  Maquis du Zaire]


Kasha, Kashala sikilliza nikueleze ,
Mimi nateseka shauri yako bibi,
Ungenieleza mapema,
.............


Sikutegemea Kashala,
Kama ungeweza kunivalia ngozi ya nyoka,
Kwa jinsi mimi nilivyokuamini wewe,
Na matokeo yake ukaniweka kwenye janga

Kibwagizo:

Kashala yoyoyo,
Nini hayo yote mama,
Ni tamaa ya kupata pesa kwa haraka yoyooo x2


Mapesa hayachumwi kwa haraka Kashala,
Mapenzi hayawi hivyo,
Hebu jishauri mwenyewe! x2

Huku wataka na kule wataka,
Dunia ya leo nenda polepole x2  

[Rudi mwanzo]

 

[Makumbele Part One- Maquis du Zaire]

 

[Wote]

Makumbele nimevumilia mengi

Sijakutendea kosa mpenzi ee

Nimevumilia mengi mpenzi wangu baba watoto Makumbele

(repeat)

 

Lakini leo nimefika mwisho

Kwa kweli mpenzi si kawaida yako

(repeat 2 lines)

 

Nitarudi kwa baba na mama

Mawazo yangu yote ni kwa watoto Makumbele

 

Mazowea pia yana tabu yake

Nitajitahidi mpenzi nitayasahau

(repeat 2 lines)

 

Aaa Vumbi.....

(repeat all from beginning)

 

(Chorus)

 

[Wote]

Rudi ee rudi ee rudi mama watoto

Umetoroka nyumbani bila taarifa yoyote mama

(repeat 2 lines)

 

Kama nilikukosea ungesubiri mpenzi eee

Kama nilikukosea naomba msamaha

 

[Wote]

Rudi ee rudi ee rudi mama watoto..........

[Rudi mwanzo]

 

[Makumbele II - Maquis du Zaire]

Makumbele nilikupenda mimi  ulishawishiwa na nani bwana,  

Nilipoamua kwenda kwetu nimefikia ukingoni bwana.   

Nilipoamua kuondoka nyumbani kwako,  

Uamuzi wangu mpenzi jamani eeeh  

Nimevumilia lakini sasa nashindwa  

Bora lawama mpenzi kuliko fedheha!!   

 

Kibwagizo:   

Anayenipotosha mimi ni yuleyule msichana wa Ilala mama  

Kanifilisi hadi nimeuza nyumba  

Kasababisha mimi kufukuzwa kazi x2    

Makumbele nilivumilia mengi baba,  

Nilikushauri hukutaka kusikia  

Sasa wahangaika mpenzi Makumbele   

 

Kibwagizo:   

Anayenipotosha mimi..........    Vumbi, vumbi, butabashiii, batumbaaaeeeh

[Rudi mwanzo]

 

[Mabruki - Maquis du Zaire]

 

Mabruki nasikitika mwenendo wako eee... mama aaa

Tabia na vitendo vyako vyanikera babu wee ....Sheri eee

Kinachokuangaisha utakuja juta baadaye ......mama aaa .....Sheri eee

 

We baba muzima popote waitwa mzee wa kutumia

Sifa gani bwana nieleze!

Miaka kumi ya kazi hata musingi huna

Mimi Arafa nasononeka iyolele

 

(repeat from start)

 

(Chorus)

 

[Wote]

Mabruki jaribu kutenganisha maisha mume wangu

Bila kujihadhari babu eee utakuja juta dunia hii

Tazama tunavyoishi jamani shida na shida

Sasa tunao watoto wanne nyumba bado tunapanga

Mimi Arafa nikuelewe vipi bwana wee

 

(repeat chorus)

 

Ulipewa mkopo kazini hapo hapo ukajitangazia kuwa wewe ni KIMWAGA!

Starehe na starehe

(repeat )

 

[Wote]

Mabruki jaribu kutenganisha maisha mume wangu..............

 

(cheza kwa maringo)

[Rudi mwanzo]

 

[Mfaume - Maquis du Zaire]

Ewe Mufaume umefika nyumbani kwetu,
Mimi bado nasomaaa,
Ukanieleza kwamba tufunge pingu za maisha pamoja,
Nikakueleza subiri,
Nikimaliza shule ewe Mufaume,
Kwa kuwa siwezi kuolewa bado ningali mwanafunzi ooh x2


Kibwagizo:

Chuki ya nini kwa wazazi wangu we Mufaume,
SIjakukataaa eeeh papa,
Nimekueleza subiri nikimaliza shule,
Nitakujibu eeeeh papa x2

Rudi mwanzo  

[MAISHA NI SAFARI NDEFU -  Maquis du Zaire]  

Kweli maisha ni safari ndeeefu eeeh x2
Ambayo haina mwisho eeeh,
Mwisho wake ni kifoo ehe,
Mwisho wake ni kifoooooo,
Mwisho wa maisha ni kifo eeh x2


Kibwagizo:


Nimebaaaki na kuanza kuwaza eeh,
Kuanzia utoto wangu,
Wakati bado niko nyumbani,
Ninalelewa bado na wazazi ,
Na sasa nimekua ,
Nimejitoa kwa wazazi,
Naanza kujitegemea,
Kweli maisha kumbe taaabu,
Kweli maisha kumbe taaabu,
Mwisho wake ni kifoo,


Mwisho wake ni kifooooooooo,
Mwisho wa maisha ni kifooo eeh

Rudi mwanzo  

[Tusijuwane Mpaka Milele - Maquis du Zaire]

Sina tena hamu nawe
Tangu ile siku
Nilipofahamu
Tabia yako....haina ujamaa
Tusijuwane....mpaka milele

Rudi mwanzo  

[Usiku Wa Jana - Maquis du Zaire]

 

Usiku wa jana sikulala,
Nasikia moyo oooh unauma,
Wasiwasi mwingi roho inauma,
Kumbe ilikuwa utabiri,
Wa njama za majirani ooh mama,
Wanasema naringa oooh sana,
Tulia kabisa oooh mama. x2


Kibwagizo:

Kwa maneno ya chuki wamenizungaka oooh,

[Bure ooh, bure oooh, bure ooh]

Wamenichukuza mabaya badala ya mema ooh,

[Bure ooh, bure ooh , bure oooh]

Na chuki badala ya upendo wangu,
Nilikuwa na utu kwao mama,
Wanionapo hutikisa vichwa vyao,
Wamenivika laana kama kanzu,
Ikawaingia mioyoni mwao x2

Kaaazi yangu kweli oooh, iyolele,
Na matatizo yote Mungu anajua,

Ubaya na wema wangu wote iyolele,
Ndio umeniponza,

Machozi yanidondoka iyolele,
Nakosa hata la kufanya.

Kusemasema sikuzoea iyo mama,
Yote kwa Mungu baba eeeh x2

Rudi mwanzo  

 
[ZOWA - Maquis du zaire]
 
Zowa ooo ooo ooo
Zowa we Mpenzi wangu
Kwanini leo umeniacha sina kosa nililofanya
Zowa eeee tulia Mama
 
Zowa fikiri kwanza tulikotoka
Mpaka sasa ni miaka mingi
Zowa eeee sikia Mama
 
Chorus
Sitaki mimi matata
Sitaki mimi kusemasema
Nimekupenda wewe tu kwa nini huelewi
Imekua kama bahati kukupata wewe Zowa
Tulia tuzae watoto
Usifuate ya walisema watakupoteza
Kipenzi changu eee Mama eee Mama eeee
 
  Telemuka telemuka chekee chekeecha
Chekeecha Mama, aa cheza kwa maringo
 
Rudi mwanzo  

 

[BAHARIA - Maquis du Zair]

 

Mimi kazi yangu baharia  Mwaka mmoja au miwili niko ndani ya bahari  

Nakubali shida na matatizo 

Yote juu ya watoto wangu 

Yote hayo juu ya kupenda familia yangu eeeh  

Likizo napata  Narudi nyumbani  Nakuta mama watoto  Ametoroka jamaniiii  

Naingia ndani ya nyumba yanguuu  Naona giza  Nitoke nje nitizame juu 

Naona jua na mwezi  Vinakutana leeeeeoooo   

Mama naliaaaaaa  Mizimu ya mababu  Njooni leeeo naumia  yoo lele naumia.   

 

(Churus) 

 Kumwacha muke wangu  Nashindwa kweli mama 

Watoto kuwalea na mama wa kambo  Siwezi kweli mama 

Malezi mema ya watoto ni kuwalea baba na mama yoyoooo  

Maungo yamenilegea juu yake yeye  Na kazi bado kwisha  Sijui nitafanya nini yoyooo   

 

Kumwacha muke wangu......   Kuondoka kwangu safarini  

Tuliagana salama nayeeee  Ahadi tukapeana mashahidi malaika mamaaaaa   

Nilimwamini yeye leo kanigeuka tena  Mizimu ya mababu sijui la kufanya kweliiiiii   

Kumwacha muke wangu.........   

Chekeee, chekecha, cheza kwa maringo , 

cheza ukijidai, maimai maaaa,abatumbaeeee ( Huyo ni mzee Mwema Mudjanga)  

 

Rudi mwanzo

 

[TAFADHALI - Marquis du Zaire]

 

Tafadhali, usiwe na hasira,  usiwe na wivu na kujiumiza bwana wee (x2)   

Nilipokuona nilivyofurahiiii na kukuita sheri eeeh  Mpenzi wanguuu , 

Ukajifanya husikiiii  Uliongeza mwendo kwa kasi kama treni eeeh  

Masikini mie machozi yananidondoka eehhh  Bwana we,

Bwana we nimekukosea nini?   Niko chini ya miguu yako, 

Napiga magoti mbele yako......

 

Tafadhali naomba nambie unasumbuliwa na nini? 

Tafadhali naomba nambie ulichonacho moyoni

Akili haifanyi kazi kwa kuwa wewe unaumiaaaa,aaah maua eeeh 

Nipe ruksa kukutuliza ,  nikupoze moyo wako, 

Sina furaha machozi yanidondoka ohhh  

 

Rudi mwanzo

 

[ANJELUU -  Maquis du Zaire]
 
Mapenzi gani yanizungusha barabara  
Yote nakuwa kama kichaa
Nazunguka uchochoroni kote kumtafuta Angeluu yeyeee
Nachoka nakaa chini nakumbuka siku alhamisi tulipokutana mimi naye
 
Usiku wa jana sikulalaa yooo
Nageuka geuka namuwaza yooo
Mbu wananiuza sisikii yooo
Ninachotaka kuona ni Angeluu yeeee
 
Jamani sasa Anjeluu anasema anataka kukata tamaa
Haki ya Mungu nitampatia kisu akate tamaaa
Kweli kweli mimi nitampatia panga akate tama
 
 
Ni wangu eeeeh Anjeluu
Ni wangu maamaa
 
Sogea karibu mpenzi wangu eeeh  
 
Ni wangu eeeh ..
Naomba tuoane mutoto wa mamaaaa eeh
Ni wangu eeh  
Mama sogea karibu nitulize nikate kiu Anjeluu
Ni wangu eeeh 
Mimi naye, naye Kasongo naye , wangu  eeeeeh  
Ni wangu eeee

 

Rudi mwanzo

 

 

[Makumbele Part Two - Maquis du Zaire] 

 

Makumbele nilikupenda mimi  ulishawishiwa na nani bwana,  

Nilipoamua kwenda kwetu nimefikia ukingoni bwana.   

Nilipoamua kuondoka nyumbani kwako,  uamuzi wangu mpenzi jamani eeeh  

Nimevumilia lakini sasa nashindwa  Bora lawama mpenzi kuliko fedheha!!   

 

(Chorus)

 Anayenipotosha mimi ni yuleyule msichana wa Ilala mama  

Kanifilisi hadi nimeuza nyumba  

Kasababisha mimi kufukuzwa kazi (x2)   

Makumbele nilivumilia mengi baba,  

Nilikushauri hukutaka kusikia  S

asa wahangaika mpenzi Makumbele   

 

Anayenipotosha mimi..........    

Vumbi, vumbi, butabashiii, batumbaaaeeeh

 

Rudi mwanzo

 

[Nasononeka - Maquis du Zaire]

 

Mimi  nalia nalia sana, mpaka machozi yamenikauka ooo

Dhambi gani mimi nimefanya ambayo Mungu hawezi kunisamehe ee

Mume wangu akipata MSHAHARA, mimi na watoto wangu tunafunga Ramadhani yooo

 

Miaka 25 mimi nipo bado kijana mdogo

Ninavaaa magauni yenye viraka vya kubandika bandika kama mtu aliyefiwa ooo iyooo

Nikienda kwa wazazi wangu wananirudisha

Wanasema kwamba hatuwezi kukulisha wewe na watoto wako....

Ikiwa mumeo hana uwezo iyooo

(repeat from Miaka 25...)

 

(Chorus)

[Wote]

Nataka kucheka sina mbavu yooo

Moyo wangu unasononeka kwa mume iyooo

Uamukapo asubuhi hajali chai yooo

Kazi yake kaka kunywa pombe iyyoo

Wenzio hunywa mutori wa moto iyooo

Kazi kaka kudowea pombe iyoo

 

[Mmoja]

Nikisema nicheke ni mume wangu wangu mwenyewe

Aibu na mambo yote yatanizengea miye yooo

DOTI MBILI za kanga sasa mwaka wa SABA!

Sokoni mie peku peku VIATU kwangu sivijui

 

[Wote]

Nataka kucheka sina mbavu yooo .........

 

[Mmoja]

Nasononeka nasikitika mama  nalia yooo

Mimi kuolewa inakuwa kama utumwa baba aaa

Wazee wa baraza naomba ushauri jamani eee

Mumukanye baba watoto labda atawasikia aaa

 

[Wote]

Nataka kucheka sina mbavu yooo ............

[Rudi mwanzo]

 

[LUTA - MAQUIS ORIGINAL]

 

[Wote]

Mpenzi Luta nasikitika sherii!ehee!

Yoyoyo kuishi tena na wewe

Mama yo vituko vyako vimezidi !

Vimenichosha oo mupenzi!

Nashindwa hata la kufanya

 

Nilikuwa nikikuonya hukutaka kunisikia!

Najuta yoyoyoo! Kuishi nawe

Masikini miye mamaaaa kwa kweli sina raha

 

(repeat from beginning)

 

Sasa umeipatapata iyo mama Luta !

Tazama sasa maisha yako yamebadilika!

Ubishi wako mpenzi wangu ukweli umekuponza

Hukutaka kusikia cha mume!

Sasa yamekukuta

Dunia ya leo Luta! nenda pole pole

 

Luta ehee!mpenzi wangu maaaaama x 3

 

Rudi mwanzo

 

[KALUBANDIKA- Marques]

 

[Wote]

Kama wewe ulinipenda

Kwa nini kunidanganya bwana wee

Kujibandika madaraka siyo yako bwana wee we

Unadhurura mchana kutwa

Kupita kuranda randa mitaani

Kumbe hukuwa na uwezo kwa nini kunidanganya

Nikuelewe vipi?

Babu eee uaminifu wako uko wapi ?mamaaa

 

(Chorus)

[Wote]

Usinione BWEGE mamaaa.....Kalubandika eee

Kwa kukubali mwito wako Kalubandika ee

Hayo yote ni matatizo ya dunia mama aa

 

[Mmoja wao]

Akiingia kwenye baa kazi yake kuomba bia

Hana hata aibu sigara pia anaomba

Mitaani na kwenye masoko

Hujitangazia kuwa yeye ni MKURUGENZI wa kampuni fulani

Kumbe sio hivyooooo

 

[Wote]

Usinione BWEGE mamaaa.....Kalubandika eee

Kwa kukubali mwito wako Kalubandika ee

Hayo yote ni matatizo ya dunia mama aa

 

[Mmoja wao tena]

Nilitaka kujitumbukiza ndani ya moto ee mama

Kumbe bwana yule hana KITANDA wala SHUKA

Pa kulala hana, analala kwenye STENDI ya Basi!

Pa kulala hana, analala kwenye KITUO cha UDA! Kalubandika yeyeee

Wacha vituko we bwana

 

[Wote]

Usinione BWEGE mamaaa.....Kalubandika eee.........

 

Rudi mwanzo

 

[Ngalula - Maquis du Zaire]

 

[Wote]

Kinachonifanya nishindwe kuamua eee mama ee

Eee najua mwenyewe

Eeeee maaaamaa

 

Pamoja na vituko vyake mama eee

Bado namuhitaji maishani ee

Eeeee najua ee Ngalula

Eee nimemuzoea ee

Shanganga Ngalula , Ngalula ....

Ananielewa vizuri mamaye kuliko mutu yoyote maaaamaa

Shida na raha zangu Ngalula anazielewa ee

Jamani Ngalula  nimemusamehe mama

Jamani Ngalula  nitamvumilia nione mwisho wake eeee mamamama......

(repeat from start)

 

(Chorus)

 

[Wote]

Ngalula mama Ngalula wangu mamaye

Ngalula mama ziba masikio

Ngalula mama Ngalula wangu mamaye

Ni maji ya moto yatapoa mama....

 

(repeat chorus )

 

Eeee....yewala...

Eeee....yewala....

Vumbi, Vumbi eee

Sendema, Sendema, Sendemaaaaaaa

 

[Rudi mwanzo]

 

[Umalize Mambo - Maquis du Zaire ]

Anasema ulie umalize mambo ooo

Yeko baba, yeko analia sana Kassongo

 Anasema ulie mama ulie mama....

[Rudi mwanzo]

 

[KAZI NI UHAI - Maquis du Zaire]

Wakati nilipokuwa mdogo, nilikuwa mdogo,

Sikuwa najali shida, wala raha,

Nilikuwa nategemea, wazazi wangu,

Sasa nimekuwa , 

Naanza kuona shida duniani

 

Ahh kuepuka siwezi,

Sina la kufanya mziki ni kazi,

 

Msinicheke eeeh msinicheke,

Ndivyo mambo yanavyoenda, msinicheke,

Leo kwangu ,kesho kwako

Aaaa mwenzangu, siwezi,

Sina la kusema, muziki ni kazi

 

Kazi ni uhai kwa kila binadamu oooh yayayaaa,

Kutoka enzi na enzi za mababu zetu jamani eeeh ,

Hata baba Mungu pia aliumba dunia,

Binadamu na viumbe vingine alifanya kazi.

 

[Mzee Mwema Mudjanga]

Cheke chekeeeee, cheke chekechaaaa,

Telemuka, telemuka telemuka

[Rudi mwanzo]

[Sea Wa Nibalo -  Maquis]

 

Sea wa Nibalo ye yeye ye Sea

Sea nipo wako, Sea yeye yeye Sea

 

Wenye kusema sema ooo Sea....

 

(baadaye anasema)

Hata mvua ikinyesha Sea yoyoyo Sea

Lazima tutoke leo, Sea yoyoyo Sea

Tuonyeshe mapenzi yetu...ya ukweli sea

 

Hata wabaya wetu wabaki na aibu

 

[Wandugu Muwe Na Huruma – Maquis du Zaire]

 

Nasema sina ndugu wa kuweza kunisaidia

Nikifa leo na kesho maiti ya kwangu ni bure

Itatupwa kama mbwa na kuyasahau palepalex2

 

 

Wandugu mue na huruma

Wandugu mue na huruma

Mateso ya kwangu ni yako

Tafadhali tupendane

[Rudi mwanzo]

[Malokele – Maquis du Zaire]

 

Malokele yeyeyeye Malokele

EEEE...

Sikiliza mama aaaaa

Mambo-ya-umbeya sikuyazowea naona bora nikueleze

Iyeee Malokeleee

 

 

[Mmoja]Epukana na vikundi

[Wote]Malokelee Mama

[Mmoja]Hayo ndio wameyazowea

[Wote]Malokele mama....  

***********

[KLARA – Maquis]

 

(Chorus)

[Wote]

Klara e mama sikujua kama utanikataa ee

Klara ye mama

 

[Mmoja]

Mla nawe si mfa nawe mpenzi mama naamini

Utanikumbuka Klara ee

 

[Wote]

Ye ye ye ye ye utanikumbuka Klara e.....  

****************

[I love you – Maquis du Zaire]

 

Najua ee ukeli unaumiza eee

Najua eee ukweli unaumiza mama

Najua ee ukweli unaumiza ee Mama aa aaa Mama aaaa

 

 

(Assosa)

 

Huwezi kuamini lakini uongo wako Mama

Hunifanya nilie ee wangu eee

Hivyo ni kwa sababu nakupenda sana Mama

Kama huamini nitazame macho kwa macho

Utayaona Leilah wangu

 

I love you I love you i love you Ilove you Mamaa

 

(Parashi)

Watu wanatusemasema eti hujaridhika na maisha

Lakini naamini ni mimi pekee aliye moyoni mwako 

eee Mama eeee

Leo nakuomba utamke kwa roho moja

I love I live you Baby

 

(Assosa)

Unaniumiza wakati husemi ukweli Mamaa

Usiku unakua wapi wakati ukweli ninao

Mara nyingi usiku silali nawaza sijui uko wapi

Kama huamini nitazame macho kwa macho utayaona

Leilah Baby Ilove I love you Baby

[Rudi mwanzo]

[Tulipopatana Mimi Nawe – Maquis du Zaire]

 

Tulipopatana mimi nawe,

Hatukuwa na mashahidi, inakuwaje sasa mapenzi yamepiga hatua watuingiliex2

Ninaposema mupenzi wangu eeeh,

Unisikie,

Nasema tena mupenzi wangu eeeh,

Unisikie

Ninachotaka mimi nawe,

Tuishi mama kama zamani eeh,x2

Masakamalembe alifika nyumbani eeeh

Kukupasha mambo ninayofanya,

 

Anachotaka mimi nawe,

Ahakikishe tumeachana x2

[Rudi mwanzo]

 [Aurelia – Maquis du Zaire]

Tutasema tutagombana bure

Mambo ya unyumba usiingilie

Wakielewana tutabaki na aibu mama
Wakipatana tutabaki na aibu mamaaa

[Rudi mwanzo]

[DOUBLE DOUBLE – Maquis du Zaire]

Jamani kweli mi nahaingaika hospitali zote nimemaliza sipati nafuuu  
( Gitaaa la nguvu kutoka kwa Nguza Viking )
Nimejaribu hata mitishamba bila mafanikio,
Ugonjwa wa moyo!
 
 
Mapenzi yamenizidia,
Mganga ni yule ninayempenda,
Nifanye nini naye hapendeki!
 
 
Naomba radhi mpenzi kama nimekosea,
Nitavumilia yote sababu nakupenda,
Nawe yatakufika!
 
 
Kibwagizo:
 
Naanza kuona Double Double,
 
Mpenzi wangu nasikitika
 
Naanza kuona Double Double,
 
Yote bure , yote bure,
 
Naanza kuona Duble Duble
 
Double Double  : Naanza kuona Duble Duble

[Rudi mwanzo]

[SAFARI YETU MBEYA – Maquis du Zaire]

 
Safari yetu Mbeeeya,
Tulifurahi saana,
Wakazi wote Mbeeeya,
Walitushangiliiiia,
 
Sikukuu  ya wakulima Sabasaba oooh x2
 
Kusema kweli nduuugu,
Hatuwezi kusahau (yoyoyoooo)
Kutushughulikia kama familia yenu,
 
Sikukuu ya wakulima Sabasaba ooh x2
 
Cheke chekeeeee, cheke chekecha,
Teremuka, teremuka,
Tusangalai,
Maimaima,
 
Cheza kwa maringo, cheza kwa madaha, cheza ukijidai

[Rudi mwanzo]

 

[Maburuki – Maquis du Zaire]

 

Maburuki nasikitika mwenendo wako ee Mama aaa

Tabia na vitendo vyako vyanikera Babu ee cherie ee

 

Kinachokuhangaisha utakujajuta baadae Mama aa

Cherie ee

 

We Baba mzima popote waitwa Mzee wa kutumia

Sifa gani Bwana nieleze

Miaka kumi ya kazi hata msingi huna Mimi Arafa nasononeka iyo lelel x2

   

Chorus

Maburuki jaribu kurekebisha maisha Mume wangu

Bila kujihadhari Babu wee utakujajuta dunia hii

Tizama tunavyoishi jamani shida na shida

Sasa tunao watoto wanne bado tunapanga

Mimi Arafa nikuelewe vipi aeee

 Ulipewa mkopo kazini hapohapo ukajitangazia

Kwamba wewe ni Kimwaga Starehe na starehe x2  

Sanifu, sanifu ,cheza kwa maringo,cheza kwa madaha

Rudi mwanzo  

[Sumu Ya Mapenzi – Maquis]

 Ufitinaaaaa na upelelezi ni sumu ya mapeenzi,
Ufitina naaa, na upelelezi ni sumu ya mapeeenzi,
 
Tumependana wenyewe bila ninyi kujua,
Sasa mwajua mwaanza kuleta matatizo,
 
Mimi kupendwa na yeye ooohhhh,  
Ninyi mwakerwa na nini ihhhhh,
 
Yeye kanipenda,  
Nami nampenda,
 
Ninyi mwakerwa na nini iiihhhh

Rudi mwanzo  

 

[SARA – Maquis du Zaire]

 

Kinachonisumbua ni mapenzi

Kukuwaza Sarah

Ugonjwa huu huponywa na yuleyule

Aliye moyoni mwako Mama

 

Fanya hima Mpenzi uniokoe

Usingizi huwa sipati

Hata kwa vidonge silali

Dawa ni mapenzi

 

(Chorus)

Hawaende hivyo usiwe hivyo Mama

Unikumbuke ingawa kidogo eee

Kunjua uso wako Mama

Cheka kidogo Mpenzi Sarah

Rudi mwanzo  

[TULIPOANZA MIMI NA YEYE - Marquiz du Zaire]  
 
Tulipoanza mimi na yeeeyee
Sikutegemea kama mambo yatakuwa mazuri eeeh  
Sababu mutu mwenyewe  
Alikuwa maarufu sana aaaahaaa
 
Sasa ikaja,
Tena cheo jamani,
Ndio nazidi,
 kusonga mbele,
Sikutegemea,
 mambo yeeee, niko wa kwanza aahaaaa
 

usinione hivi mwenzangu lolo
kweli nimetoka mbali sana
wakati mwengine niache nipo hai
shida zikaanza
mawazo yananituma niishi pekee ah aha aha


Tuombe Mungu atupe  
Tupendane iyoleeeeeeee,
Mvumilivu hula mbivu yeye,aahaaa iyooooooo
 
 
Kibwagizo:
 
Jamani leo ni kama ndoto,
Yuko mikononi mwangu eeeh  
Iyoyo iyoyo iyo,
Yuko mikononi jamani x2
 
Mwenzenu hata habari sina eeeh  
SIjui kama ninaye,
Iyoyo, iyoyoo iyo
Sijui kama ninaye,
 
Nimetoka naye mbali eeeh iyo
Nimetoka naye kwetu iyoyo iyoyox2
 
Jamani leo ni kama ndoto.. 

Rudi mwanzo  

[UBA -  Maquis du zaire]
 
(Assosa)
Leo nasema Uba wangu mie
Vituko vyako Uba vimenichosha Uba
Nisingekua mvumilivu Uba
Tungekua tumeisha achana
 
Majirani Uba wananita mi mpumbavu
Uliumwa Uba nikajitolea Uba
Nikahangaika Uba kwa mara ya kwanza maishani
Uba wangu mie pesa ni matokeo
 
Chorus
Ona sasa Uba eee Uba wangu mie
Aibu imetupata wote Uba eee Uba wangu mie
 
Bobo Sukari)
Nilifanya makosa Mama kukupenda wewe
Leo niko lwangu Mama naona chamtemakuni
Shukrani ya punda Mama ni mateke Uba wangu
 
(wote)
Ona sasa Uba eee Uba wangu mie
Aibu imetupata wote Uba ee Uba wangu mie
 
(Parashi)
Nisingelikua mvumilivu hatungeliishi Uba
Uba pesa ni matokeo nakuelenza Mpenzi ee
Kitu nakuomba oo nisikilize kwa makini Uba
Angalia sasa Uba tumepata aibu Ubaaa
 
(Wote)
Ona sasa Uba ee Uba wangu mie
Aibu imetupata wote Uba ee Uba wangu mie
 
(Assosa)
Kwa Heri Uba ,Uba ee
Iko siku utanikumbuka tena Uba
 
Ona sasa Ubaa eee Uba wangu..................
   
(Hii ni version ya pili maana ya kwanza aliimba Adios na siyo 

Bobo na solo lilipigwa na Nguza lakini hii ni Mbwana Cox)

Rudi mwanzo  

 

 

[Wanakudanganya  -  Maquis du Zaire] 

(Chorus) 
Mama yoo yo yooo
Mama yoo yoo yyoooo
Wanakudanganya Mpenzi utakujajuta baadaye
Wanakudanganya Mamaa
Walimwengu hawataki kuona
Sisi tunaishi kwa amani na upendo
 
Wanakudanganya Mamaaaa

Rudi mwanzo  

   
[
MANENO YAKO -  Maquis du Zaire]
 
Maneno yako yote nimeyapokea
Yako moyoni mwangu  
Nimeyapokea kwa roho moja
 

Uko hapa moyoni mwangu
Mpenzi wangu macho yameona wengi  
Lakini ni wewe pekee ninayekupenda
 
Uondokapo kwenda kazini
Wasiwasi kwangu hunijia
Kama utarudi salama na Mungu yuko nawe
Daima nitakupenda

Roho yangu nimekuachia wewe,
Nguvu zangu zote ni kwaaako,
Hakuna kilichokuwa na thamani kwangu ila wewe.
Ninapokuona au nisikiapo sauti yako,
Furaha hujaa moyoni. 
 
Maneno yako yote
 
 
Ze zi, ze zi , zembwelaaaa
 
Rudi mwanzo  

 

[Kaiba - Maquis du Zaire]

 (Utunzi wake Kalala Assosa)

Unachoshangaa sasa ni nini wee Babu
Au unafikiri sio mimi kunitamani tena
Basi mimi ni yuleyule Kaiba
Uliyekua unanitelekeza na kunifukuza
Kwa kashfa usiku mwingi mvua ikininyeshea
Bila huruma Mama mama
 
Usishangae Babu mimi leo nimependeza
Hii ni kazi nzuri ya mwenzzio Babu kanithamini
Basi mimi ni yuleyule Kaiba
Uliyekua unanitelekeza na kunifukuza
Kwa kashfa usiku mwingi mvua ikininyeshea
Bila huruma Mama Mama
 
Chorus
Hata hivyo Mama ngoya
Kwa kweli dunia kabla hujafa haujaumbika
Namshukuru Mungu umeniacha salama
Mama ngoya ngoya mi Kaiba nimetulia x2
 
(Halafu anakuja Mbwana Cox na solo moto kabisa )

 Rudi mwanzo  

[MIMI NALIA(Nasononeka) - Maquis du Zaire]

 Mimi nalia nalia sana.

Hata machozi yamenikauka eeeh,

Dhambi gani mimi niliyofanya,

Ambayo Mungu hawezi kunisamehe,

Mume wangu akipata mshahara,

Mimi na watoto wangu tunafunga Ramadhani eeeh x2

 

Miaka ishirini na tano mimi niko bado kijana mdogo ,

Ninavaa gauni yenye viraka vya kubandika bandika 

Kama mutu aliyefiwa  oooh iyoooooo,

  

Nikienda kwa wazazi wangu,

Wananirudishaaaa,

Wanasema kwamba hatuwezi kukulisha 

Wewe na watoto waaakooo,

Ikiwa mumeo ana uwezo oooh iyooooooo.

 

Kibwagizo:

Nataka kucheka sina mbavu yooo ( mi nalia)

Moyo wangu unasononeka ,

kwa mume iyoooo ( kwa mume)

..........kwa kulia chai chai eeeh,

Kazi kaka kudoea pombe iyooo,

Wenzio hunywa mutori wa moto iyoo

Kazi kaka kudoea pombe iyooo,

 

Nikisema nichekeeee,

Ni mume wangu mwenyewe,

Aibu na mambo yote ataniachia miyeee eeh,

Doti mbili za khanga sasa mwaka wa sabaaaa,

Sokoni mie pekupeku viatu kwangu sivijuiiii

 

Kibwagizo:

 

Nataka kucheka sina mbavu yoyooo

 

Nasononeka nasikitika mama nalia yooo (pole)

Mimi kuolewa inakuwa kama utumwa jama ooh,

Wazee wa baraza naomba ushauri jamani, eeh 

Mumkanye baba watoto labda atawasikiaa 

Nataka kucheka sina mbavu ooh

  Ogelea , ogelea piga mbizi, 

Mimi na yuleeeee,

Ogelea ,ogelea piga mbizi

 Rudi mwanzo  

[SOPHIA – Maquis du Zaire]

 
Mimi leo mama yako ewe Sophia,
Pamoja na baba yako tunakukalisha chini,
Tupate kuusia dunia hii ni ngumu,
 
 
Usiende mbio mbio kukimbilia mlio,
Kumbe kule hukujua wendako kuna kilio,
Tutapatwa na huzuri watu wakikusikia
 
 
Kibwagizo:
 
Hata ukiwa na cheo,
Kazini kwako wakisema,
Huo ni wito wa wazazi wako,
Kama utawabishia utaumia!x2
 
Sophia eeh mama, eeeh mama epukax2 

Rudi mwanzo

 

[Jane - Maquis du Zaire]

 

(Tabia Mwanjelwa.)
 
Jane mimi nahangaika,
Juu yako kwa maisha yako,
Hebu nieleze ni mtu gani anayekudanganya? x2
 
Jane siku hizi maisha ni magumu sana,
Jitizame jirekebishe,
Maama kwa maisha yako,
Mimi mama yako na hawa majirani sielewani nao,
Mimi mama yako nimekwisha zeeka!
 
 
Kibwagizo:  
 
Asiyefunzwa na mama
[Ewe Jane]
Asiyefunzwa na mama
[Hufunzwa na dunia Jane]
Asiyefunzwa na mama
[Jirekebishe]
 
 
Jirekebisheeeeeeeeeh, jirekebishe Jane!x3

 

Rudi mwanzo

 

[Juu Ya Nini - Maquis du Zaire]


Juu ya nini eee?
Juu ya nini unanificha ukweli wako?
 
Sababu ya nini eee?
Sababu ya nini unanificha uhakika wako
 
Oo nalia mama, o nifanye nini
Oo nasikitika aiyooo

Rudi mwanzo

 

[Umekwama Leo Umekwama - Maquis du Zaire]
 
Ujanja wako umekwisha,
Utaja kuwakosa wawili kijasho kitakutoka leo,
Na ukumbuke ulikotoka ni penzi nimekupa. x2
 
 
Kumbuka umaarufu wako,
Sababu yangu mimi mama,
Leo hii unapendeza, unatia na vidudu,
Lakini kama ulivyofanya sio hasara kwangu mimi ,
Na uchague mmoja wetu kati ya mimi na wewe x2
 

Rudi mwanzo

 
 
[KIONGO - Maquis du Zaire] 
 
Kiongo Mama njoo mbona umeadimika
Kiongo nakuhitaji Mama wangu wa maisha
Sina habari napata uko wapi Mama aaa
Nasengi yo nyota bolingo ................. ........
Sina ubaya na wewe samahani Mama Kiongo
 
 
 
Chorus
Napata tabu Mama
    KIONGO
Mapenzi yamenihangaisha
   KIONGO
Penda akupendae
   KIONGO
Karibu wangu Mama
 
     KIONGO
Nakuomba radhi mwenye makosa husamehewa
 
     [Rudia chorus]

 

Rudi mwanzo

 
[USLA- Maquis du Zaire] 
 
Chorus
 
[Assosa]
Mimi na wewe Mama
 
[wote]
Oooo Usla wangu Mimi
 
[Assosa]
Yote ukitaka tuyamalize
 
[wote]
Tutayamaliza lakini letu liwe moja
 
[Assosa]
Yote hayo Mama
[wote]
Tutayamaliza lakini letu liwe moja

 

Rudi mwanzo

 

[Minou - Maquis du Zaire]


[Assosa]
Wewe ndio ulianza kunitaka eti tuachane
Nilikubembeleza usiku mzima
Ubadilishe uamuzi wako Mama
Nimekuzoea ee hukutaka kunisikia
Ukanihukumu bila hatia
Ukanitangazia ubaya ulivyotaka we Minou ee Minou ee
Ooo Minou eee Kamsuti eee
 
Ona sasa wivu wako mwenzangu mie masikini
Nilijua eee waliokudanganya wako wapi
Wamekuacha huna pa kuanzia
Dunia ya leo matata ee Minou ee Minou eee
Eee Minou ee Kamsuti eee  
 
Chorus
Eee Mama ee maombi yako yamenifikia
Asante sana kwa kunikumbuka
 
Eee Mama ee uwezo wa kukusaidia sina tena
Yaliyobaki yangu macho ee
Nina mzigo mkubwa nyumbani
Eee Mama ee Mama eee  

Rudi mwanzo

[Salimia - Maquis du Zaire] 
 
[Assosa]
Kufika kwako kwetu Salimia kumezua jambo
Baba kavunjika mguu katumbukia shimoni
Alipokua anakukimbiza yo yo yo
 
 
[Wote]
Mpenzi nashindwa aaaa sijui niamue lipi
Kukupenda bado nakupenda aaa
Lakini Baba yangu mie sobongo
 
 
[Assosa]
Yo yo ona sasa Mpenzi Salimia
Haraka yako Mpenzi ni mimi sasa naumia
Baba Hospitali anateseka
Wewe upande mapenzi yananisumbua
Nifanye sasa nini yo yo yo Salimia Mama
 
  [rudia wote]
 
 
Chorus
Angalia kukosa kwa imani yako kwangu
Nilikuambia usifike nyumbani kwanza
Niachie mwenyewe Salimia
Nitajieleza kwa wazazi wangu
Hukutaka kunisikia Salimia
Matokeo yake Baba kabaki kilema
Mimi na wewe oo Salimia
Naona basi tena
(sahau dozen,solo limepigwa na Kivukutu sio mchezo}
 
Sendema camarade Sendema
Sendema cherie Sendema
 
 
Chini ya mti chini ya mwembe washawasha

Rudi mwanzo

 

[Wimbo - Maquis du Zaire] - Ngosha

 
Nimechoka Bwana nimechoka
 
Nimeamua nirudi kwa Baba na Mama
 
Nikatulie nyumbani
 
Chorus
 
Ulikua unalewa eeee
Nyumbani kwako huonekani
Pesa za chakula ee Bwana
Naombaomba kwa majirani
Wazee walikuweka chini Bwana  
Hukutaka kuwasikia eee
Sasa leo wajuta eee
Sasa leo wajuta

 

[TIPWATIPWA - Maquis du Zaire] - Ngosha
 
Tipwa Tipwa hebu amka unieleze kweli
Ndoto za siku hizi zanitia wasiwasi iiiii
 
Sasa ni mara ya tatu hunijia ndoto
Watoto wamekonda kwanini
 
Mume kafukuzwa kazi kwa ajili ya anasa Tipwa Tipwa
............. ...... ...... ........  itakua vipi mimi Joha

 

 

[Monimambo - Maquis du Zaire] - Mtukwao
 
Barua yangu natuma kwa kaka aaah Monimambo oooh,
Ufikirie,  
Mimi niko nyumbani bado nasoma,
Wajua nabaki na mama,
Mbali uliko,
Baba kafariki mwezi wa saba,
Aaaah Monimambo oooh.
 
 
Fikiria we ni mtoto wa kwanza,
Kwa baba na mama,
Twakutegemea,
Kwa nini hutaki kurudi nyumbani,
Kumuona mama jinsi alivyo,
Haya maisha wapata leo yatoka wapi?
Kama si wazee,
Ooooh Monimambo.
 
 
Kibwagizo:
 
Sasa ni miaka minne hata barua ewe kaka,
Kwa nini Monimambo wakua hivyo ewe kaka,
Fikiria mzazi wako, ndio baraka kwako Monimambo.
 
 
Jirekebishe kaka,  
Na starehe za huko mjini,
Mama analia kweli eeeh , Monimambo rudi nyumbani
 
 
Sasa ni miaka minne....

 

[SUMU YA MAPENZI - Maquis du Zaire] - Ngosha
 
Ufitina na upelelezi ni sumu ya mapenzi
Ufitina na upelelezi ni sumu ya mapenzi
 
Mimi kupenwa na yeye
Nyinyi mwakerwa na nini ee ee ee ee
 
Tumependana wenyewe bila nyinyi kujua
Sasa mwaona mwaanza leta matatizo
Mimi kupenwa na yeye
Nyinyi mwakerwa na nini
 
Amenipenda nami nampenda
Nyinyi mwakerwa na nini eee eeee eee
Amenipenda nami nampenda
Nyinyi mwakerwa na nini eee eee eee
 
Nasi twazidi kuimarisha mapenzi yetu
Duniani tumekuja wawiliwawili
Kusaaidiana ndio raha ya dunia
Nyinyi mwakerwa na nini eee ee eee ee
Amenipenda nami nampenda
Nyinyi mwakerwa na nini

 

 

[NAJUA UTANIKUMBUKA - Maquis du Zaire] - Mtukwao
 
Mwenzenu nimeduwaaaa,
Nashindwa niseme nini,
Mume kaniacha kwao kijijini kaenda mjini kutafuta kazi eeeh,
 
 
Kufika mjini kapata kazi,
Akanisahau,
Mimi na watoto nabaki nahaingaika eeeh,
Kumbe dunia hadaaaaa,
Jama eeeh,
Nashindwa hata la kufanya miee,mamaeee
 
Waume wa leo hawaaaminike tena eeeh,
mama eeeeh,
Kumbe dunia hadaaaaaaa,
Jama eeeh
 
Kibwagizo:
 
Najua utanikumbuka eeeeh mama eeeh,
Siku nyingi tuliishi nawe mpenzi eeeh,x3
 
 
Matatizo yote niliyavumilia maama eeeh,
Nyumbani kwangu wote yote wanajua mama eeeh
Tuliiishi kwa taabu,
Kula kwa taabu,
Kulala lkwa taabu,
Yote nilivumilia aaaah mama eeeeeeh
 
Najua utanikumbuka eeeh....

 

 

[NILIPOKUA MDOGO - Maquis du Zaire] - Ngosha

 
Wakati nilikua mdogo nilikua mdogo
Sikua najali shida wala raha
Nilikua nategemea wazazi wangu
Sasa nimekua naona shida nyingi duniani
Aaaa kuepuka siwezi aaa kuepuka siwezi
 
Usinicheke usiniiicheke ndivyo mambo yanavyoenda
Usinicheke leo kwangu kesho kwako
Aaa mwenzangu sina la kusema sina la kufanya
Msingi ni kazi
 
    [rudia]
 
Kazi ni uhai kwa kila Binadamu oo ya yaa
Kutoka enzi na enzi ya Mababu zetu jamani eee
Hata Baba Mungu aliumba dunia
Binadamu na viumbe vingine alifanya kazi
 
    [rudia]
 
Zembwela,zembwela..............