[Mwanzo] Rudi Table
Mtoto wa Arusha mama mbona wanipa shida
Mimi ni wako waikana mulu eee
Wache waseme seme watachoka wao
(Chorus)
Mapenzi ya pesa hayadumu Mama
Mapenzi ya roho ni ya maisha
Nimekupenda na wewe umekubali
Ukila kisamvu.......ooooooo
Kaza roho Mama
DAR-ES- SALAAM jiji umbeya mwingi
[Athumani - Makassy]
[Wote]
Athumani eee vipi mambo VALUVALU?
Umenioa bado ningali kijana
Ukipata chungu kipya usitupe cha zamani.........Athumani eee
Athumani eee samaki apishe chambo
Kila apitae Athumani asabahi
Kusema sema sijui kubishana sitaweza........Athumani eee
(repeat x 3)
(Chorus)
[Wote]
Mke wa ne eee.....mke wa ne...
Unkasigo oooh, unkasigooo
Akana ubufi nu bumi,
Atikulonda ukwendenda,
Akamanya kuyelayela,
Atugalile kanunu fijoooooo!
[Umasikini Si Kilema - Makassy]
Umasikini si kilema ni matatizo
Ni matatizo ya Dunia ndugu yangu
Kitu kimoja ninalia watoto wangu...
Wamenikimbia kwa sababu shida nyingi
Kuku anakula sawa na mdomo wake....eee
(Chorus)
Yaliyopita nayo yamepita
Yatayokuja nayo yatapita
Aaaa Aaaa Aaaaaaaaa
[Bomoa(tutajenga Kesho) - Makassy]
Bomoa ee bomoa ee bomoa mama tutajenga kesho
Tutajenga kesho imaaa
[Mmoja]
Nyinyi watoto wazuri wote njooni tucheze leo
Bomoa eee
[Wote]
Bomoa, bomoa, bomoa mama.....
[Siku
Ya Kufa - Makassy Orchestra] - tizedboy
[Prelude
miondoko ya kulonga]
Hii nyimbo ni nyimbo ya ukumbusho
Wa siku ya kuzaliwa na siku ya kufa
Tumetoka kwa udongo....
Tutarudi kwa udongo
[Mwanzo----Remmy]
Mawazo
mawazo ya mutu muzima ee
Kila akikuambia neno usibishe ee
Ila ya muzee ukabisha mwisho utapata tabu
Kuimba tunaimba nashauri musikie
Ila msisahau muziki ya Makassy inawasuhia
Mambo yenye manufaa
Siku
ya kufa siku ya kufa siku ya kufa
wandugu kwaheri
Siku ya kufa nyama ya udongo
Akina Mama kwaheri
Dar Internationale kwa heri
Marquis kwa heri
Supa Afrika kwa heri
Dar es Salaame kwa heri
Piga hodi utafunguliwa ee
Maiti haina rafiki
Mwanamuke muzuri hakosi kasoro ooooo
Mwendo wa chura kuruka ruka e
Mwendo wa bata upande upande
Mwendo wa Jongoo kusua sua e.......atafika tu!
Jongoo mpenda watu e na watu hawamupendi Jongoo oo Jongoo
[Mwanangu Celina
- Makassy Orchestra] - tizedboy
Mwanangu Celina, mbona hutulii
Hali yako eee
Si ya kawaida
Hata chakula huli vizuri
Sababu gani Mwanangu eee
[Mmoja]
Baba nashukuru kuniuliza swali kama hilo
Nilipokuwa Shuleni, uliniambia nimalize kusoma
Masomo nimemaliza
Leo hii ni miaka mitatu
Nitafute Kazi
Hutaki unataka niolewe!
Nimepata ee atayenifaa
Nimempata ee wangu wa milele oooo
Mama mama ma a
[Wote]
Mwanangu Celina.........
[BINADAMU HATOSHEKI
- Makassy Orchestra] - Mtukwao
Kwa vipi atatulia jaaamani,
Ikiwa apatacho hakimtoshi,
Awe ni mwenye mali,
Ataka tena nyingine,
Kulalamika hachoki yeee,
Binadamu kweli hatosheki.
Kibwagizo:
EEh jamani eeeh ,binadamu hatosheki,
Hata ukimpa , nini
Milele hatoridhika,
Leo mvua inanyesha, binadamu achukia,
Kesho jua linawaka, binadanmu achukia eeeh,
Eeeeh amani eeeh, binadamu hatosheki,
Hata ukimpa nini, milelel hatoridhika eeeh
Ukimpa tano leo,kesho atataka kumi
Eeeh jamani ,binadamu ......