[Mwanzo] Rudi Table
Jana jioni, tulimaliza sherehe,
Sherehe za harusi,
Alipoolewa dada,
Na mume ampendaye,
Na Mungu awabariki,
Waje wapate watoto,
Wa kike na wa kiume,
Diana dada hongera sana!
Kibwagizo:
Kazi uliyofanya, Dia dada kazi kubwa,
Kwani vijana wa sasa hawapendi kuoa,
Nao akina dada hawapendi kuolewa,
Iliyobaki ni sisi ndio tunatia nguvu,
Twawaombea baraka, ( baraka kwa Mungu eeh)x2
Baraka kwa Bwana Mungu eeeh ( baraka kwa Mungu)x2
[Kisa Cha Foto Album - Kimulimuli]
[Wote]
Wameniambia mambo yako mama eee
Wamenieleza matatizo ya mume wako eee
Na kisa cha we Sheri Zinduna kufika kupewa TALAKA!
Wameniambia mambo yako mama eee
Wamenieleza matatizo ya mume wako eee
Japo mwenyewe hukutaka wanambie siri yako moyoni
Foto Album inaleta maneno katikati ya mji wa Mwanza
Kisa ni picha ilopigwa zamani katikati ya Dar-es-Salaam'a
(repeat)
(Chorus)
[Wote]
Sheri Zinduna nakupa pole Zinduna eee
Sheri Zinduna nakupa pole Zinduna eee
[Zahir]
Matatizo yanakukuta
Mkasa nyumbani kwako eee
Ndoa imevunjika mama eee kosa ni picha ya zamani ooo
[Wote]
Sheri Zinduna nakupa pole Zinduna eee
Sheri Zinduna nakupa pole Zinduna eee
[Zahir]
Afadhali ngekuwa labda mie nimewahi kufika Mwanza
Lakini toka nimezaliwa ee.....
Sijafika Mwanza aaa
[Wote]
Sheri Zinduna nakupa pole Zinduna eee
Sheri Zinduna nakupa pole Zinduna eee
[Zahir]
Kipato baba watoto ajue sijafika Mwanza ee....
Toka mimi nimezaliwa ee
Vitongoji navisikia kwa watu eee
[Wote]
Sheri Zinduna nakupa pole Zinduna eee
Sheri Zinduna nakupa pole Zinduna eee
[Zahir]
Kitongoji cha Nyama nacho...
Pamoja na Kirumba nasema
Kigogo na Isamba eee
Nimeelezwa na wenyeji aaa
[Wote]
Sheri Zinduna nakupa pole Zinduna eee
Sheri Zinduna nakupa pole Zinduna eee
[Zahir]
Ni sawa sawa ya Kanuta ee
Pamoja na Miti Mirefu mama ee
Pamoja na mtaa wa Sukuma ee
Wamenambia wenyeji aaaaa....
[Wote]
Sheri Zinduna nakupa pole Zinduna eee
Sheri Zinduna nakupa pole Zinduna eee........
Ulipokuwa ukikanywa, hukutaka kusikia,
Ile tabia mbaya, hukutaka kuibadilisha,
Dunia ya Mungu, sasa inakufunza,
Fungua macho ,
jaribu kujirekebisha Kabwe x2
Kila hila wazazi wako waloitumia,
Katika kukufundisha, ulizidi kuwa mtukutu,
Baba alipokukanya , ulizidi kuwa mtukutu,
Mama alipokukanya , ulizidi kuwa mtukutu,
Walimu wa shuleni kwenu Kabwe ukitaka kupigana nao,
Yote yanayokukuta, wa kulaumu ni we mwenyewe x2
Tabia ya udokozi Kabwe ulianza siku nyingi,
Wakubwa kubadilika, sasa ni jangili mkubwa weeex2
Habari zako zote, zinafika kwetu eeh,
Hatuji kukuona gerezani, si kama si tumekususa,
Watuona kimya, kazi zimetuzidi,
Kazi zimetuzidi ,kazi za ujenzi wa taifa letu changa x2
[Kabwe
Part II - Kimulimuli]
Kabwe rudi nyumbani,
Ukitoka gerezani,
Uje ujiunge nasi,
Sote tushiriane,
Kulijenga Taifa, Taifa letu hili changa Kabwe x2
Kibwagizo:
Kabwe yoyoyo,
Kabwe mwana kwetu karibu nyumbani oooh x2
Karibu Kabwe karibu,
Karibu kijijini,
Karibu Kabwe karibu,
Karibu kwetu Likwini,
Karibu mwana kwetu, kwenu ulikozaliwa Kabwe!
Kabwe katoka kwenye chuo cha mafunzo,
Wala hakutaka kurudia kwapukwapu
[Kama zamani yooo]
Karibu Kabwe karibu .....
Wazazi, wazazi wetu eee
Mashujaa tuliorudi, tumerudi kishujaa
Mashujaa walokufa wamekufa kishujaa
Lengo na nia yetu wazazi lilikuwa moja
Kuilinda hadhi yetu eeh
[Mmoja]
Tulipofika ...... na akachamaa
Tulipofika Entebe na akachamaaa .....
Kitu mapenzi kilianza zamani,
Toka wakati wa mababu zetu,
Na hata wao mapenzi waliyakuta,
Tokea enzi za Adamu na Eva,
Yalianza zamani nasi tuliyakuta x2
Inasemekana zamani sana,
Katika ile bustani maalum ya Eden,
Chui na mbuzi walikula pamoja,
Tohe na simba walishirikiana
Sote tu binadamu Christina elewa,
Ni aibu sana kwa tabia zetu,
Christina ahadi!
Kama ni kutengana tutenganishwe na kifo,
Hata huo sio mwisho tutakuja kukutana,
Tutakutana tena kesho kwenye Paradiso
Unatega masikio kusikiliza fitina mama
Dunia hii ya Mungu, watu ni wa aina nyingi mama
Wengine hawana huruma mama
Wanafanana na moto
Wacha kucheza na moto
Moto ni Moto huunguza
[Prelude]
Aaa ni maneno ya ugombanishi, ni maneno ya kuvunja nyumba
Aa shoga yangu unataka kunitenganisha na mume wangu
Nakupasha nimeshituka
Nimeshituka...
[Vyombo na mwanzo wa nyimbo]
Shoga leo nisikilize
Shoga leo nikupashe
Na urafiki wetu utakwisha leo
Nakuona una nia mbaya
Uje uniachishe kwa mume wangu.......
Oh shoga yangu eeeee
Shoga we ulisema maneno mengi
Lakini haya ya leo nashindwa kuvumilia
Naona mwisho nitakuja achwa....
Uje kunicheka aaaa
Shoga ni wewe uliyesema
Kwa kuwa mume wangu ni mwana miziki....
Kama kweli ananipenda....
Angeniimba kwenye nyimbo zake...
Na kunifananisha na ndege Tausi....
Oh shoga yangu eee
Shoga sasa nitakupasha...
Nywele za Tausi hazitaji kitana
Mguu wa tausi hauhitaji kiatu
Macho ya tausi hayapakwi wanja
Mimi ni binaadamu tausi ni ndege.....
Uzuri wake nitaupata wapi ?.....
Tausi mwenye rangi eee
[Zahir]
Umempasha vya kutosha mama ooooo
Atazaaame ustaarabu wa kwake yoyoyoyo
Umempasha vya kutosha mama ooooo
Atazaaame ustaarabu wa kwake yoyoyoyo
Asifate mambo yasiyomuhusu
Atazaaame ustaarabu wa kwake yoyoyoyo
Na kama kukusifu we mama watoto
Hilo ni jukumu langu
Na sasa naamua.....
[Wote]
Mama watoto pasenti mia moja
[Zahir]
Kwa ukarimu kwa wageni wetu nyumbani mama oooo
[Wote]Mama watoto pasenti mia moja.....
[TIKISA - Kimulimuli(Zahiri Ally Zoro)]
Tikisa amerudi salama kutoka Paris,......
Tikisa ana mambo ,tikisa huyu azungumzi kiswahili i!
Salam yake ni Bonjuu mensier! bonjour!
Savaur? savaa byee!
Chorus:
Hata siku moja uje kuwachukua mkeo na watoto wako ehee!
Watoto mali yako ni jasho lako maua!....
...........
Siku moja tikisa alijaribu kumrubuni mwanafunzi kwa kifaransa.............
Ikamkuta aibu yule dada alipojibu!
Excee mwa!
communicae mwa in kiswahili,kigogo kizaramo.....
Nimekubali
yanayosemwa na watuuu,
Ni kweli anayependwa na wengi siku zote
hufa angali kijana x2
Chiku wangu wee, kalale pema peponi
Chiku wangu weee, daima nitakukumbuka
Fadhila
na Rehema binti zetu, nitawatunza, nitawalea ipasavyo, naahidi mbele yako
Hawatapata
taabu hata siku kwa ukumbusho kwa mapenzi yetu
Chiku
wangu weeee
[Oliva
- Kimulimuli]
Oliv mama,
Mwana kwetu eeeh,
Sikiliza Oliva,
Nikupashee,
Nilipokutana nawe,
Japo mara ya kwanza,
Tabasamu lako,
Lilishika pendo langu,
Oliva, mama yoooo,ooh, ohhh x2
Kibwagizo:
Tutakapokubaliwa,
Tutafunga ndoa Oliva wangu,
Tutafunga ndoa Oliva wangu, x2