Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]    Rudi Table

 

[ASHA MWANA SEFU - Juwata Jazz Band]

 

Asha mwana Sefu

niambie mpenzi wangu

imekuwaje leo mama upo kimya hivyoo

ni lipi jambo lilokuudhi nieleze leo

sema Asha sema sema mpenzi wangu 

kama mimi nimekuudhi unielezee

 

nashukuru mume wangu 

kwa kuniulizaa oh 

unakunywa pombe uonekani hata siku tatu

nachekwa na wenzangu 

watoto wanateseka 

hata huruma huna 

kwa hawa malaika

 

(wote) kibwagizo

ulevi ulionao bwana unanitia aibu

huna mapenzi eh 

kwangu mimi na watoto

 

(TX)

ah mama nimekubali

maneno yako mama ....... oh mama

wakale walisema

mjinga pa kwenda

pa kurudi anajua 

pabaya na pazuri nasema

 

(wote) kibwagizo

 

(Zengakala)

natubu mbele yako 

na hata kwa hao malaika

unisamehe duniani

hata mbinguni ...... oh oh

 

(wote) kibwagizo

[Rudi mwanzo]

 

[AZIZA - Juwata Jazz Band ]

Aziza nisamehe sana,

Kugombana kwetu kusiwe moyoni mwako,

Mimi hapa nilipo , 

Ninajuta sana,

Kugombana na wewe Aziza ni vibaya sana x2  

 Kibwagizo:

Aziza sasa naomba, Turudiane

Hayo yamekwisha , Kipenzi changu

Shetani katupitia ,Rudi mke wangu

Mimi mwenzio mama ninapata taaabu x2

Rudi mwanzo  

 

[JEFA - Juwata Jazz Band]


Jefa mwanangu,
Ni uamuzi wako kutengana na Hanifa,
Lakini kumbuka Jefa,
Hanifa kavumilia mengi ya shida,

Ulipomuoa ,
Alikukuta na wanao bado wadogo,

Na baadaye ,
Ulifungwa jela,

Sasa umefunguliwa na umepata kazi nyingine,
Leo unamuona Hanifa hafai,
Na kwamba ana balaaaaaaaaa,

Ooooh ,oooh Jefa mambo yote hupangwa na Mungu x

Rudi mwanzo  


[Mariamu Ninakujibu - Juwata Jazz Band]

 

[Wote]

Mariamu ninakujibu kwa maneno uliyoyasema

Mimi sikukusudia kuvunja ahadi yetu

oo Mariamu eee ( x 2)

(repeat x2)

 

[Maalim Ngurumo]

Nilipofika mjini dada Mariamu...

Kusema kweli nilishika mambo ya mjini

(repeat)

 

[Wote]

Sasa Mariamu eeee  ninachokujulisha dada

Ujitayarishe kuhusu ahadi yetu

(repeat)

 

Nimefikiri sana, kwa kweli nimekosa

Dada Mariamu nakuomba radhi

(repeat)

 

 Ooo Mariamu eee, ooo MAriamu

Wazeee wamenisema sana

Kuhusu kitendo nilichotenda

Naomba unisamehe sana, kwa kosa nililokukosea

(repeat)

 

Oo Mariamu eee, ooo Mariamu eee......

Rudi mwanzo  

 

[Umefanya Visa Vingi - Juwata Jazz Band]

Nilikupeleka kwa wakwe zako, 

ukaonane na ndugu zangu eeeh, 

Hata mama yangu alifurahi sana, 

Na ndugu zangu walikupenda sana,x2   

 

Mipango yetu dada ni kuoana, 

Kama tukichunga heshima yetu, x2  

 

Kibwagizo:  

Sasa nasikia umefanya visa vingi eeeh 

Hata mama yangu ,  Humthamini   

Ikiwa mambo yenyewe ni hivyo,  Mbona mazito, 

Hapo sasa mimi nitashindwa,  Siwezi kukuoa tena!!  

 

Kibwagizo   

Maji yalokwisha mwagika eeh,  Hayazoleki , 

Iliyobakia sasa majuto,  Nenda kwenu salama,  

 

kibwagizo  

nilikueleza toka zamani  kitu kimoja 

uchunge heshima kwa wakwe zakoo  ukapuuza   

Sasa nasikia ....


[MSAFIRI KAKIRI - Juwata Jazz Band]

(Utunzi ni wake TX Moshi William, solo kupigwa na Abdi Ridhwan 'totoo' au siku hizi Pangamawe, 

rythim na Pishuu, bass na Issa Ramadhani. Katika wimbo huu Sax zimepulizwa barabara kabisa na Mnenge, 

Abdi Mketema, na Hagai Kauzeni)


(TX Moshi)
Mini mwendapole ninakuja  
msafiri kakiri
walisema waswahili nenda ukitizama mbele na nyuma
 
moyo wanidunda nilidhani  
tena kwa uoga wa safari
yakutafutaa
maisha mazuri
 
najikaza kiume nakwenda  
nawapisha wenye haraka  
waje wapite mimi naja taratibu
 
oh Ridhwani sema
 
najikaza kiume nakwenda
nawapisha wenye haraka  
waje wapite mimi naja taratibu
 
(sax murua)
 
(wote) kibwagizo
msafiri kakiri .....kakiri
mwendapole ninakuja
nawapisha wale warudio na waendao kwa haraka
 
(Lusungu)
safari ni hatuaa
mwenda pole hajikwai
penye nia pana njia
lengo langu litafikia eh
 
(wote) kibwagizo
 
(Lusungu)
kwa kuwa duniani  
kuhandaika ili ufanikiwe  
pasi nitasafiri kila pembe  
iko siku mungu atanisaidia eh
 
(wote) kibwagizo
 
(Lusungu)
Mwendapole hajikwai
akijikwaa haanguki
akianguka haumiii
kuumia kwake kidogo tu
 
(wote) kibwagizo
 
(Lusungu)
kwa kuwa duniani kuhangaika ili ufanikwe
basi nitasafiri kila pembe
iko siku mungu atanisaidia eh

Rudi Mwanzo

 

[PAMELA  - Juwata Jazz Band]

 

(Kibao Pamela kilipigwa na wana Msondo ngoma magoma kitakita, 

kuimbwa nae Fresh Jumbe akisaidiana na sqwadi zima la wana msondo, 

solo gitaa lilipigwa na Saidi Mabera, gitaa la kati lilipigwa na baba Isaya, 

bass na julius Mzeru na kujumuisha wana msondo enzi hizo)  

 

[Jumbe]  

Nakiri udhaifu na fahari kwa pamoja  

Ndani ya nafsi yangu oh mieeee  

Kila ninapofikiria wema wako dadaaa  

Ambao umenitendea  

Hata hii leo kuwa kipimo cha utu wangu  mimi ninajiuliza 

Nikupe nini wewe  mimi ninajiuliza nikupe nini wewe   

 

[Wote]

Sikijui cha kukulipa pamela  aa 

Kulingana na wema wako dadaaa  

Wema wako Pamela ni wa asili oh dadaaaa   

 

[Jumbe]  

Kadiri itavyokuwa Pamela  

Wema wako ni wa asili oh daada  

Nami wangu kwa vyovyoote vile  

Utakuwa ni wa kuiga tuuu  

Hautolingana kamwe pamela ....... 

Hautolingana kamwe oh pamela   

 

[Wote]

Sikijui cha kukulipa pamela  aa........

Rudi mwanzo  

 

[Ashibaye  - Juwata Jazz Band]


Wala hakuna mvumbuzi

Aliyewahi kuvumbua mizani hiyo ulimwenguni

Aashibaye......

Rudi mwanzo  

 

[ABEDI  - Juwata Jazz Band]

Ohh Abedi ohh
hebu mkanye mwanao
vitendo anavyofanya
kumtorosha binti yangu
siku mbili tatu mwana simuoni nyumbani
majirani walinieleza
walimuona na mwanao

siku mbili tatu mwana simuoni nyumbani
majirani walinieleza
walimuona na mwanao

(Wote) Kibwagizo
tena natoa tahadhari Abedi ..... Abediiii
usije niona mbaya bwanaaa ...... Abedi kakaaa
tena nasema ujirani utakwisha juu ya watoto bwanaa x 3

 

Rudi mwanzo  

 

[NGAPULILA - Juwata Jazz Band]

(Kibao Ngapulila aliimba Adam Bakari (Sauti ya zege) pamoja na sqadi la wana Pambamoto awamu ya pili, sauti katika wimbo huu zimetiwa naksh na Maneti, Adamu Bakari, Benjamini, bwana Khamisi, solo limepigwa na Shaaban Yohana (wanted) rythim na Manitu (baba watoto) bass chini ya Semhando, kinanda kikipapaswa kiufundi na Abdul Salvador)

(wote)
rafiki yangu nakuaga mimi oh
nataka kuzamia meli niende ng'ambo
kutafuta maisha eh
kweli naona maisha ya hapa nyumbani kakae
yamenishinda
kula kwa taabu
kuvaa kwa tabu eh
kulala kwangi geto
basi naona shida tupu eh shida tupu eh

sina raha masikini mimi oh
sina raha hata kidogo
sina raha masikini mimi oh
sina raha hata kidogo Ngapulila eh

(wote)kibwagizo
maisha ya kuzamia melini yana hatari kubwa eh
kutoswa baharini na kupoteza maisha yako
Ngapulila eh achana na mawazo hayoo
Ngapulila una hatarii eh

(Maneti)
Ngapulila mwenzio kashikwa ughaibuni
kazamia meli na kukutwa na madawa ya kulevya
na sasa yupo kifungoni ...... lahaula
Ngapulila Ngapulila kaka unahatari ehh

(wote)kibwagizo

(Eddy Sheggy)
fanya kazi kwa bidiii
utapata kaka
tamaa ya kufika ng'ambo eh
imeponza wengi
wengine walijaribu ......... kuteka ndege nyeraa kutumia silaha za bandiaa eh
Ngapulila una hatari eh

(wote) kibwagizo  

 

Rudi mwanzo  

 

[FATUMA(Oo Maisha) - Juwata Jazz Band]

[Mmoja]
Fatumaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa
(taaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa)

Nasafiri mamaaaaaaaaaa
Baki salama o o o o Fatuma
Nitarudia mama

Fatuma niombee dua nitarudia
Fatuma niombee dua nifike salama
Mbali sana ninakokwenda aa Fatuma

Kitu ninachokuomba utunze watoto
Ujitunze na wewe...Fatuma mama aaaa

Ukibadili tabia yako Fatuma eee
Ujuwe nitaambiwa, nitaona vibaya
Tutatengana aaa

Oooooo Fatumea eeee

(Chorus)
[Wote]
O Maisha.......o maisha
Kweli ni visa....kweli ni visa
Kulala mbali, kwa ajili ya peeeeeeesa

[Mmoja]
Nalala mbali mimi kwa kutafuta pesa aaa
Mke na watoto nawaacha mbali eeee

[Wote]
O Maisha.......o maisha

Rudi mwanzo  

 

[SINA RAHA NA MKE WANGU - Juwata Jazz Band]

 

[Fresh Jumbe]

Siku hizi sina raha na mke wangu nyumbani  

Nirudipo kazini humkuta kajiinamia  

Nikimuuliza vipi mke wangu mbona umekasirika  

Ashindwa kunijibu hubaki analia  

 

Nazidi kumbembeleza sana sana mke wangu eh  

Mwishowe akaamua kunielezea  

Eti anafahamu mambo yangu yote nifanyayo nikiwa kazini

Eti nina wanawake wengi sana mie 

Kwa hiyo anataka tutengane  

 

Nazidi kumtoa hofu ya hayo maneno mke wangu  

Nami sito kubali namsaka mbeya huyooo   

 

[Wote]

Ama zake ee ama zangu  

Ole wake akae akijua  labda nisimtambue   

 

[Jumbe]

Naelewa nia yake ni kutaka kutukosanisha

Nimekuwa sikai nikafurahi mimi na mke wangu   

 

[Wote]

Mtu huyoo adui yangu ....... adui yangu  

Kanitafuta kwa siku nyingi  naona amenipata   

 

[Jumbe]

Naelewa nia yake ni kutaka kututenganisha

Nimekuwa sikai nikafurahi mimi na mke wanguuu  

 

[Wote]

Ama zake ee ama zangu  

Ole wake akae akijua  labda nisimtambue

 

Rudi mwanzo

 

[MWANA ACHA WIZI Juwata Jazz Band]

Majirani wenzangu,

Naomba mnisaidie,

Mkanyeni mwanangu, 

Labda atakusikieni,

Nimemkanya aache wizi mwanagu kanishinda,

Labda nyie wenzangu mtaweza kunisaidia,

 

Asante ndugu, tutajaribu kumuelisha,

Kiasi cha uwezo wetu,

Huyu mwanetu.

 

Ewe mwana tulia, Tukueleze,

Tabia uliyonayo ya wizi haikufai,

Ulipelekwa shule , elimu umepata,

Ya kuweza kukusaidia 

Kuliko kutaka utajiri wa harakaharaka.  

 

 

(Kibwagizo)

 

Ehhe mwana hukusikia niliyokwambia,

Balaa kutuletea nyumbani 

eeh mwana.

Wazee wenzagu pia walikuketisha chini,

Wengi walikueleza mwana acha wizi,

Nawe hukusikia ukazidisha vitendo vya wizi.

 

 [Ngurumo]

Umevunja duka la Ushirika,

Bunduki imelia,(mama weeee)

Shaba yaingia mwilini mwako waona uchungu!

 

 

Leo uko taabani ,

Hospitali umelazwa,

Pingu ziko mikononi mwako mwanangu umefungwa!!

 

 

Ehee mwana hukusikia   

[Rudi mwanzo]

 

[Priscila - Juwata Jazz Band]

 

(wote)

kwa tabia zako bibi eh mimi sitokuacha

hasa upole wako mpenzi eh , kamwe sitakuacha,

Hata kama watu watasema sana,

Sitawajali haoo Ooooh ,

kwa vile najua uzuri si shani ,

ubora tabia x2 

 

(wote) Kibwagizo:

kuishi wawili ni kusikilizana

hapo mapenzi ndipo yanapodumu

(Mbwembwe)

Kwa kuwa tunapendana, mengi utasikia,

Lakini usijali eeeh

Mpenzi wangu eeehh,

 

(wote) kibwagizo

 

(Zengakala)

Ukipata shida kidogo,

jaribu kuvumila Priscilla,

Kwani hayo yote Priscilla, 

Ni ya muda sana maamaaa,

Elewa Priscila eeeh Kipenzi eeeh

 

(wote) kibwagizo

 

(Zengakala)

Tuzae wetu watoto waweze kutusaidia badaye

tukishakuwa wakongwe watatufaa mamaaa

elewa Pricilla eh kipenzi eh

 

(wote) kibwagizo

[Rudi mwanzo]

 

 

[QUEENKASE Juwata Jazz Band]

Kaka yangu kafariki

chonde mtoto wetu

mke na watoto utarithi wewe

ili ukoo wetu usipotee

 

oh baba na mama mnisikilize kwanza

kwa haya ntakayosema naomba mnikubalie x 2

 

kuridhi ndoa ya kaka kwangu mimi ni vigumu

na kumuacha queenkase ni vigumu pia x 2

 

(Kibwagizo)

[Wote]

sikatai ombi lenu bali ninajishauri 

kumuacha queenkase kwangu mimi ni muhali

 

[Zengakala]

Maneno mliyosema enyi wazazi wangu 

mimi nimeshindwa ooh jamani eeh

queen amejaa rohoni mama 

queen amejaa rohoni mama

 

(Kibwagizo)

[Wote]

 

[Suleiman Mbwembwe]

maneno uliosema wazazi tumesikia

lakini kumbuka kwanza shemejio na watoto

ni kuwakumbusha uwpo wa marekemu kaka yakoo

 

(Kibwagizo)

[Wote]

 

[Zengakala]

naahidi mbele yenu

watoto nitawatunza 

na hata mama yao kweli

simtupi kamwe

lakini kase kase kase nipo nayeee

lakini queen kaseke nipo naye

 

(Kibwagizo)

[Wote]

[Rudi mwanzo]

 

[Nanawa Mikono Juwata Jazz Band]

 

Nanawa mikono naupumzisha moyo wangu,

Na jeraha lililokuwa likinisumbua linaanza kupata nafuu

naahidi mbele za Mungu sitokuwaza tena,

sikurajia kashfaa kutoka kwako ya wewe 

kunisifia ujinga, tunapopanga tukutanee kipenzi 

wewe huwa hutokei, na kusema eti nikuonapo 

na babaika, na wewe kuanza kunisachi nilichonacho

bila wewe kuniomba, Nanawa mikono mimi tabia zako

zimenichosha.

 

anaejua mapenzi hawezi kunilaumu

mimi kukupa nilichonacho ni kwa kua

nakupenda, ukiwa kimwaga unaitwa

bwege, ukibana matumizi unaitwa 

mkono wa korosho mama eeeh, iyo iyo

 

kila nikitoa nizawadi .......

[Rudi mwanzo]

 

 

[FAULATA - Juwata Jazz Band]

 (Kibao kimeimbwa naye mwenyewe Joseph Lusungu , Moshi William, Suleiman Mbwembwe, Joseph Maina,

Juma Akida Hamisi Kitambi na Tino Masenge, solo chini yake Mabera, rythim na Pishuu, bass na Issa Ramadhani,

drums kucharazwa na Saidi Mohamed, Mohamed Haroub kwenye tumba, Julius Betto na Zitto Mbunda kwenye trumpets,

 Mnenge, Abdi Mketema na Hagai Kauzeni kwenye midomo ya bata (sax) )

 

(Mwanzo)

Ilikuwa siku ya jumanne asubuhi

nataka kwenda kazini

ndipo ulipotamka neno kuwa umechokaa

kuishi na mimi

 

kosa gani eh 

ewe Faulata 

sikupata jibu jengine ila sikutaki eh

sikutaki tuuu

 

kuchunguza kuchunguza kumbeeeeee

umempata awezae kumiliki maisha yako

kunishinda mimi

 

[wote] Kibwagizo

ama kweli oh maradhi yote ugua

lakini kuchacha usiombee

 

[Lusungu]

naomba unisikile kwa makini

haya ninayokuambia 

kuibuka na kuchacha mola ndiye mpangaji wa yotee

 

[wote] kibwagizo

 

[Lusungu]

umekuwa kama mzigo wa moto ..... lo salale

haubebeki wala haushiki

nakuruhusu wendee ....... nenda

utaiona dunia eh

 

[wote] kibwagizo 

[Rudi mwanzo]

 

 

[NIDHAMU YA KAZI Juwata Jazz Band]

(Kibao Nidhamu ya Kazi kimeimbwa na Bichuka, Akida na Lusungu,

Keybord kikipapaswa na Mzee mzima Waziri Ally huku Abdallah (Dulla) akipiga tumba.)

(Bichuka)
nidhamu ya kazi ni msingi wa mafanikio mema kazini
viongozi na wafanyakazi
lazima wote muwe na nidhamu

(wote)
migogoro na migongano
ya kazini ni ukosefu wa nidhamu

(rudia mwanzo)

(wote)
viongozi pia wajibu wenu mkubwa
ni kulinda heshima ah
na kudumisha
nidhamu ya kazi
na kudumisha
nidhamu ya kazi

 

Rudi mwanzo

 

[Uamuzi Wa Kuoa Sina - Juwata Jazz Band]

 

Mwana oooh, vipi mwana,

Nimetuma barua nyingi za kutosha,

Lakini naona kimya kimezidi,

Ushauri wangu mwana ,

Napenda kukufahamisha,

Tafuta mchumba ,

Mwana uoe!

Barua yako nimeipata mama oooh,

Uliyosema, uliyosema yote nimeyasikia,

Lakini kwa kifupi tu,

Napenda kukufahamisha ooh,

Uamuzi wa kuoa sasa hivi sina,

Sina hata chumba cha kulala,

Uamuzi wa kuoa sasa hivi sina,

Kulala ninalala kwa rafiki,

Uamuzi wa kuoa sasa hivi sina

Subiri kwanza nijitayarishe,

Uamuzi wa kuoa sasa hivi sina,

Nikiwa tarari nitawajulisha,

Uamuzi wa kuoa sasa hivi sina!

[Rudi mwanzo]

 

[BAHATI - Juwata Jazz Band]


(Chorus)
[Wote]
Nakupenda BAHATI mama iyolele
Bila wewe mimi nitateseka
 
[Mmoja]
Ingawa KIGOMA ni mbali Sheri eee
Nitakuja mimi eee
Nikuone wewe
Nitakuja MWANZA a twende RUVUMA
 
[Wote]
Nakupenda BAHATI.......

[Rudi mwanzo]

 

[Rudi Mpenzi Zarina - Juwata Jazz Band] 
 
[Wote]
 
Mpenzi Zarina...ooooooo
 
Tumeishi kwa muda mrefu
 
Umeondoka bila kuniaga
 
Kwa ndugu na jamaa zako kote nimefika
 
Hawajui huko uliko
 
Unanipa wasiwasi mpenzi Zarina.....
 
(repeat)
 
 
 
[Bichuka]
 
Kama umzima huko uliko
 
Unanisikia nakuomba urudi
 
(repeat)
 
 
 
[Wote]
 
 
 
Kama kuna kosa......
 
 
 
[Bichuka]
 
Nililokukosea niko tayari kujirekebisha
 
Ninakuomba....
 
 
 
[Wote]
 
Ninakuomba rudi Zarina ili tuishi kama zamani

(Chorus)
 
[Wote]Wanipa wasiwasi mpenzi zarina
 
[Mmoja]Toka umeondoka sina raha hata kidogo.....Mpenzi zarina
 
[Wote]Wanipa wasiwasi mpenzi zarina
 
[Mmoja]Nirudipo kazini najiona niko pekee eee nyumbani iii
 
[Wote]Wanipa wasiwasi mpenzi zarina
 
[Mmoja]Wanitia majonzi Zarina...rudi rudi nyumbani mama ooo
 
[Wote]Wanipa wasiwasi mpenzi zarina
 
[Mmoja]Toka umeondoka sina raha hata kidogo.....mimi mwenzio
 
[Wote]Wanipa wasiwasi mpenzi zarina
 
(Ooo Zarina......)
[Rudi mwanzo]

[Amina - Juwata Jazz Band] - Ngosha


Amina aaaa kumbuka dada
Ntamuomba Mola atupatanishe
 
[Gurumo]
Nia yako dada nimeigundua Mpenzi
Lakini mwenzio sina kinyongo na wewe
 
Amina aaa kumbuka dada
Ntamuomba Mola atupatanishe
 
[Gurumo]
 
Uongo mbaya mi nakwambia Mpenzi
Umenigombanisha na rafiki zangu Mama
 

[WAZAZI HAWAKUBALINI - Juwata Jazz Band] - Mtukwao
 
Wazazi wake Jeni,
Hawakupenda binti yao aolewe nami,
Vipingamizi vyao vilizidi,
Na kwamba sina pesa za kumtunza.
 
Jane alipoelewa,
Aliamua kuwabembeleza,
Ili aolewe nami,
Na kwamba jambo la muhimu ni maelewano,
Hata hivyo hawakukubali,
 
Kibwagizo:
 
Nilipokutana na JEni,
Nilimshauri [nitampata wapi]
Akubaliane na mawazo ya wazazi wake x2
 
Kwani hao walikuleaaaaa,
Wakakupeleka shuuuuule,
Wakakupa mafunzo,
Ya kila aina mama,
 
Nilipokutana na JENI,
Nilimshauri,akubaliane na mawazo ya wazazi wake,
[Msondo ngoma]
 
Kama hukusikia,
Maneno ya wazee,
Utakosa radhi,  
Hatuwezi kuishi kwa rahaa aeeeh,
 
Nilipokutana na JENI,
Nilimshauri, [nitampata wapi]
Akubaliane na mawazo ya wazazi wake,
 
Kwani wao walikuleaaaaa,
Wakakupeleka shuleeeee,
Wakakupa mafunzo ya kila aina kipenzi,
 
Nilipokkutana na Jeni.....

 

[UMENITOA KIVULINI - Juwata Jazz Band] - Mtukwao
 
Kaka yangu Ada,
Ulivyonitendea,
Labda nitasahau,
Siku ya kufa,
 
Tulipooana,
Tuliishi kwa raha,
 
Tulisafiri sanaaa,
Moshi, Arusha, Dodoma, kote tulifika.
 
Wakati uliponiacha,
Miaka minne ikapitaaaaah,
Ukanirudia aaah tena,
Nami sikukataaaaa,
Kwa kuwa nilikuwa bado nakupenda!x4
 
Imekuwaje sasa leo wasema nitafute bwana mwingine?
 
 
OOOh mimi Amina,  
Najuta, najuta sana,
Ningeliajua hayooo,
Nisingekubali kamwe.
 
 
Nilifikiri kaka umejirekebisha kumbe mambo ni yaleyale!
 
 
Asante, asante sana,
Kunitoa kivulini kaka kuniweka juanix4
 
 
Kibwagizo:
 
Wacha wacha visa vyakox3
 
Wacha wacha visa vyakox3

[JULEKA - Juwata Jazz Band] - Mtukwao 


Waimbaji: Hassan Rehan Bichuka na Saidi Mabera.
 
Nifanyeeee nini jamani,  
Mawazo yamenizidi,
Huzuni moja kwa moja la kufanya sina eeeh!x2
 
 
Nilihisiiiiiiii, nitaishi naye mpaka kufaaaaaaaaaaaah.
 
 
Kipi chasumbua kichwa chaaako ewe ewe mume wangu?x2
 
 
Kama ni wanawakeeee,
Wengi wamezaliwa,
Na watazidi kuzaliwa,
Wazuri hawaishiiiiiiiiii!
 
Wacha kunitesa na watooooto,
Mimi mama watoto wako
 
Kibwagizo:
 
Kama si mimi na wewe, nani atunze watoto,
Zena hulia kila siku, baba yuko wapix2
 
Wakati wa shida,
Nilivumilia,
Sasa twapata raha wanitupa,
Mimi Juleka nitakufa kwa mawazo.
 
Kama si mimi na wewe.....
 
Ahadi yetu wakati wa ndoa,
Umeisahau,
Siku hizi pa kushinda na kulala,
Hapaeleweki!
Mimi Juleka nitakufa kwa mawazo.
 
Kama si mimi na wewe......
 
 
Nitacheza na nani,  
msondo ngoooooma eeeh,
 
Nitakwenda na nani,
Magoma kitakita eeeeh

 

[Christopher - Juwata Jazz Band] - Mtukwao
 
(Waimbaji: H.R.Bichuka na Saidi Mabera)
 
Christopher,
Uliahidi ukitoka ng`ambo,
Kwenye masomo yako,
Utajirekebisha,
Tabia ile ya kusahau nyumbani tukiteseka
 
 
Sasa nashangaaa,
Umerudi nyumbani Christopher,
Unanidharaux2
 
Kozi umemalizaaaaaaa,
Nyumbani umerudiiiii,
Cheo umepataaaaaaaa,
Na mshahara umezidi.
 
Hata mwezi bado Christopher,
Umebadili nia!x2
 
Kibwagizo:  
 
Nasikia minong`ono huko mitaani ya kwamba, unaye Anjela,
Mtoto wa Mwanza!
 
Nami sijasema neno,
Christopher,
Lakini naona,
Unawatupa watoto!x2
 

[UZURI SI SHANI - Juwata Jazz Band] - Mtukwao

(Muimbaji: Bichuka )
  
Nasikitikaaaaaaaaaaaaaaaaaah,
Kubadili mawazo yako wewe.
 
Kijana una umbo la kupendeza,
Mrefu mnene,
Na mwanya wa wastani x2
 
Hakika, uzuri si shani.
Utu wa mtu ni tabia njemax2
 
 
Nasikitika,kijana eeeeh,
Kubadili mawazo yako nakuonea hurumax2
 
Umempata wako,
Wa kukuweka ndani,
Fani zote za ndani anakutimiziax2
 
Nasikitika kijana eeeh
 
Umemkataaa eti ni mzee,
Na yeye bado kijana jama eeeh
 
 
Utampata wapi [atakayekutunza]
Kama yule kijana,
Kweli nakwambia eeeh
 
Wanakudanganya,
Kijana eeeh,  
Usiwatie maanani , watakupoteza.
 
Tulia uzae,
Kijane eeeh,
Wazuri ni wengi dada, utapata shida!
 
 
Abala yeyeee [Nasikitika kijana]
Busungu yeyee   [Nasikitika kijana]
 
Mwanyiro yeyeee   [Nasikitika kijana]
 
Akida yeyeee    [Nasikitika kijana]
 
Kakere yeyeee   [Nasikitika kijana]
 
Abedi yeyeye   [Nasikitika kijana]
 
Attutu yeye   [Nasikitika kijana]
 
Mabera yeyey  [Nasikitika kijana]
 
Bichuka yeye   [Nasikitika kijana]
 
Mnenge yeye    [Nasikitika kijana]
 
Mkonga yeyey  [Nasikitika kijana]
 
Midodi yeyeye   [Nasikitika kijana]
 
Waziri yeyeye    [Nasikitika kijana]
 
Dhahama yeyeee  [Nasikitika kijana]
 

[Nyimbo - Juwata Jazz Band] - tizedboy


Mola mzidishie busara
Na nguvu Mwenyekiti
Na walio chini yake wape busara na heshima
 
Waiongoze Nchi yetu kwa moyo
Wa Kimapinduzi
Kusudi CCM yetu ee....iendelee


[Josephina - Juwata Jazz Band] - tizedboy


Natafuta Mganga wa kunitibu mmwandani
Hajapatikana................
 
(Chorus)
Rudi kwanza Josee
Nipate nafuu
Mwenzio nateseka mama
Fanya huruma

 

[TUMA - Juwata Jazz Band] - Uzegeni
 
(TX)
nimesimama kwenye kona
ya uhuru na msimbazi
 
natizama wanaopita wanaorudi ..... mama
huenda nikaiona sura yake Tuma
 
nimesimama nikiwazaa
ahadi yetu tuliyopanga
 
tukutane Darisalama Tuma .... mama
nia na madhumuni wazazi watuone
 
nikarudi nyumbani
na mawazo teletele eh
 
shoga yake kanijia na kunieleza
Tuma eh Tuma eh keshaolewa
 
ah nikapatwa na mnutsuko
moyo wangu kenda mbio ohh
 
sikutegemea Tumaa kama angevunja ahadi yetu
ama kweli penye udhia, penyeza rupiaaa
 
(wote) kibwagizo
usinione nimekonda ewe Tuma
hakuna lengine mama ila ni wewe Tuma
 
(TX)
usiku wotee nalala nikikuwaza
nakuita jina lakooo  ...... oh oh Tuma
naomba dada kama unanisikia  
unijulishe japo kwa barua ... mama ah
 
(wote) kibwagizo
 
(TX) rudia