Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

 

Usingizi sipati Mama kwa kukuwaza wewe

 Hata kula nashindwa roho imefanya donda

 Kitu gani nimefanya mimi 

 WATAKA ITOA ROHO YANGU DEDE

 -Bima Lee

 

Uko hapa moyoni mwangu
Mpenzi wangu macho yameona wengi  
Lakini ni wewe pekee ninayekupenda
                                                                                     -Maquis du Zaire

 

Huku nilipo wazazi wangu sina ndugu
Lakini kutokana na usia wenu wazazi wangu
Najiona kama, nipo nyumbani
Najiona kamaaaa nipo nyumbani ee mama

                         -Mlimani Park Orchestra

 

 

 

Usiniache pweke Neema

Nitalia na nani Mama

Usifuate wasemayo Wafitini

Hao wako mbelembele kuharibu mapenzi yetu 

Mimi nawe

-Bima Lee

 

Sura ya Sofi....

Imekuwa pana na fupi

Ana mashavu ya kumiminina mama lelelele yooo Sofi

-Bima Lee

 

Alianza kuweka chumvi kwenye chai, 

Nilikua na wageni wakatoka bila kuaga

Akaweka sukari kwenye mboga, 

Nikaonja haviliki tukalala na njaa

-Nico Zengekala

 

Laiti moyo ungekuwa aaa

Una kifuniko radhi nikuambie eee

Tizama uone unavyokereketa mama aa

-Bendi unknown

 

Aziza sasa naomba, Turudiane

Hayo yamekwisha , Kipenzi changu

Shetani katupitia ,Rudi mke wangu

Mimi mwenzio mama ninapata taaabu

-Juwata Jazz Band

 

Penzi limegeuka moyoni ...mama eee(x2)

Niliyetaaaaaka kuoa kanitoweka siku ya Harusi

-Bima Lee

 

 

 

Kadiri itavyokuwa Pamela  

Wema wako ni wa asili oh daada  

Nami wangu kwa vyovyoote vile  

Utakuwa ni wa kuiga tuuu  

Hautolingana kamwe pamela ....... 

-Juwata Jazz Band

 

Wala hakuna mvumbuzi
Aliyewahi kuvumbua mizani hiyo ulimwenguni
Aashibaye......

-Juwata Jazz Band

 

Kitu mapenzi kilianza zamani,
Toka wakati wa mababu zetu,
Na hata wao mapenzi waliyakuta,
Tokea enzi za Adamu na Eva,
                                                                                                                  -Kimulimuli

 

Baba na mama wamenihusia 

Rafiki wa kike karibu na nyumbani

Vibayaaaa aaaa atazua maneno ya uongo

Hatimayeeee eee kukosana na mke wa nyumbani

-Bima Lee

 

 

 

Shoga sasa nitakupasha...

Nywele za Tausi hazitaji kitana

Mguu wa tausi hauhitaji kiatu

Macho ya tausi hayapakwi wanja

Mimi ni binaadamu tausi ni ndege.....

Uzuri wake nitaupata wapi ?.....

Tausi mwenye rangi eee

-Kimulimuli 

 

Mapenzi ya pesa hayadumu Mama
Mapenzi ya roho ni ya maisha

Nimekupenda na wewe umekubali

Ukila kisamvu.......ooooooo

Kaza roho Mama
DAR-ES- SALAAM jiji umbeya mwingi

-Makassy

 

Tutasema tutagombana bure

Mambo ya unyumba usiingilie

Wakielewana tutabaki na aibu mama
Wakipatana tutabaki na aibu mamaaa

-Maquis du Zaire

 

Nilitaka kujitumbukiza ndani ya moto oo miye

Kumbe bwana yule hana KITANDA wala SHUKA

Pa kulala hana, analala kwenye STENDI ya Basi!

Pa kulala hana, analala kwenye KITUO cha UDA! Kalubandika yeyeee

Wacha vituko we bwana

-Maquis du Zaire

 

Mla nawe si mfa nawe mpenzi mama naamini

Utanikumbuka Klara ee

-Maquis du Zaire

 

 

 

Hawaende hivyo usiwe hivyo Mama

Unikumbuke ingawa kidogo eee

Kunjua uso wako Mama

Cheka kidogo Mpenzi Sarah

-Maquis du Zaire

 

Jamani leo ni kama ndoto,
Yuko mikononi mwangu eeeh  
Iyoyo iyoyo iyo,
Yuko mikononi mwangu...

-Maquis du Zaire

 

Usiku wa jana sikulala,
Nasikia moyo oooh unauma,
Wasiwasi mwingi roho inauma,
Kumbe ilikuwa utabiri,
Wa njama za majirani ooh mama,
Wanasema naringa oooh sana

-Maquis du Zaire

 

Ufitinaaaaa na upelelezi ni sumu ya mapeenzi,
Tumependana wenyewe bila ninyi kujua,
Sasa mwajua mwaanza kuleta matatizo,
Mimi kupendwa na yeye ooohhhh,  
Ninyi mwakerwa na nini ihhhhh,

-Maquis du Zaire

 

OOH Lila niinachooka,  nisamehe mume wangu, 

Hapana hapana mamaaa 

Ningoje kwanza nitubu,  

Ooh binadamu yeyote hukosa 

Ukiniacha nitakwenda wapi, 

Nitasema nini nyumbani kwa wazazi eeeh mama!   

-Marijani Raajab 

 

Mayasa mbona wanichana mbavu bibiye  

Sura yako mbona sasa imekuwa hivyo  

Nakuuliza mbona hata kunijibu hutaki?  

Umenikasirikia kama mimi ndio nilikutuma   

Sura yako na ulivyokasirika mama eee  

Ndio mimi wazidi kunichana mbavu Mayasa hooo   

-Marijani Raajab 

 

Ulipopata kauli yake, ukakubali bila kusita

Uliyotaka yamekuwa......

Kazi ikawa ni moja, ni mapenzi motomoto

Umempa pendo lenye huba,

Maneno matamu kama asali

-Marijani Raajab 

 

Anababaishwa na anasa za mjini 

Bibi kanitupa na watoto hawajali

Pesa zake zote zinaishia nje

Kwa makuku ya kukaanga

Mimi na mkate mkavu

-Marijani Raajab 

 

O jama niacheni e.....

Mwenzenu nimeshapenda jama

Asiyejua kupenda Mungu amsaidie yasimkute eee

-Marijani Raajab 

 

Makatili tunawapiga lana ee.......laana kuubwa.....

Watu gani wasio na huruma ee

Kuzitoa roho za watu bila sababu ee

Hata watoto wadogo wamekosa  nini ee?

Mtakwenda sema nini mbele ya Mungu ee

Makatili tunawapiga lana ee....laana kuubwa.....

-Marijani Raajab 

 

Nakuooona njiani unapita lakini kukuita ninashindwa aaaaa

Naonyesha ishara hunioni!

O Kaka we wanikondesha.....

Sogea karibu yaaangu nikuone

Utoe sauti yako nipate sikia.....

-Marijani Raajab 

 

Mmmhhh mapenzi yawaka moto

Naitika nilikukosea sasa nihurumie

Si ninafikiri zaidi kuliko wewe

Nakonda kama mnazi kwa mapenzi nilionayo

Nilalapo nakuota mchana kutwa sili

Moyo wanichechemea mwili damu hukauka

-Dr. Remmy Ongala

 

Hakuna kitu kibaya sana hapa duniani kama shida
Haichagui mtu siku wala mwaka eee
Shida huja popote tena shida iingiapo bila hodi
Si mkubwa wala mdogo wote shida
                            -Mbaraka Mwinshehe

 

Sherehe kubwa sana nitaifanya nyumbani
Majibu mazuri nikipata
Nadhiri niliyoweka nitaitoa siku hiyo
Hapo nitapokubaliwa

-Moro Jazz Band

 

Mategemeo yangu ni kukuona Salehe,

Mpenzi Salehe okoa Roho yangu

Usiku mchana nasubiri Barua yako….Salehe
Mbona kimya mpenzi waniumiza,
Salehe mi na wewe mpaka kufa,
Nakuomba unikumbuke japo kwa barua Salehe.

-Orchestra Safari Sound

 

Mara ya kwanza uliniomba tucheze,
Muziki wa kwetu siwezi kukataa,
Mara ya pili ukarudia tena,
SIO kwa kucheza ila kunifinya jicho.
                    -Orchestra Safari Sound

 

Shemeji usiondoke,

Sikiliza uwe shahidi eeh,

Mapenzi yamenipa kichaa,

Mpaka ikawa fujo,

Ziada yuko nyumbani yapata mwaka wa tatu,

Namuita Ziada sauti inakaa ndani bila kuitikiwa eeh,

Amenikatisha tamaa na mapenzi yake ohhhhh,

Mama oooyeeee

 

-Orchestra Safari Sound

 

Ni yeye hakuna mimi anipendezae, wala kulingana huyo simuoni  miye eee

Wala kulingana huyo simuoni  miye, peke yake mwana mimi nimuuguwae eee

-Taarab JKT Kiwira Mbeya 

 

Kuwa fukara sikupenda ....

Kwa nini iwe sababu ninakataliwa

Nisimuowe binti tajiri

Ama kweli ufukara jeraha la ulimwengu mama...

-Mlimani Park Orchestra

 

 

Afadhali pia ungenieleza makosa

Niliyokutenda yoo we Gama

Kabla hujaamua kuniachaaaaa

Ulilazwa hospitali miezi mitatu,

Miezi sita masomoni yote nimevumilia eee

-Mlimani Park Orchestra

 

Hiiba nimelibeba pendo lakoo

Kama mwana na mbelekoooo  

Nina maana kukwambia mchana usiku silali

Natafuta pesaa 

li tuishi vizuri na kujenga familia bora

Yenye thamani na penzi

Hiiba imekuaje mpenzi mbona umebadilika

-Mlimani Park Orchestra

 

Umekumbwa na kitu kipenzi changu nashangaa,  

Matatizo yako ni nini kufanya jambo la karaha,   

Hebu nieleze kosa langu,  Lililovunja mapenzi yetu,  

Ukaondoka bila kuaga,  

Wanishangaza we mke wangu ahaaaaa

-UDA Jazz Band

 

Nikuite nani weweee, 

Nikuite bwana mapenzi jina hilo halikufai,

Nikuite bingwa wa mapenzi  jina hilo halikufai,

Naona bora nikuite milionea wa mapenziii

-Bima Lee

 

 

Nilichomwa na jua toka asubuhi,

Mpaka saa nane Solemba

Sababu ya kukungoja wewe

Kumbe ulikua ndani ukichungulia dirishani

Nimeshituka Solemba

-Nico Zengekala