Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]    Rudi Table

 

 

[Asia - BIMA] - Mtukwao
 
Asia yeee mama Asia eeeh,
Asia yeee mama Asia eeh,
Aisa wa mama,
Umenihuzunisha,
Asia wa mama,
Umenisikitisha,
Umenikimbia, bila ya taaarifa,
Asia we Asia vipi weee unafanyax2
 
Kibwagizo:  
 
Watu hukosana kila mara [kila mara mama]
Na husameheana mwana mama,
Wengine hutengana mbalimbali [mbalimbali]
Na wakarudiana bila bila taabu
 
Fanya hima kwa haraka rudi nyumbani mama,
Fanya hima kwa haraka rudi nyumbani mamax2 

 

[AZIZA - BIMA LEE(Shaaban Dede )]

 

Pokea wangu waraka,kipenzi wa Imani Aziza Mamax2

Nimekuteua Mama huna mshindani,ni wewe nuru ya roho yangu Mamax2

 

Nakonda sitamaniki,pendo lanisonenesha niokoe mwenzio nisizivae nguo kichwani

Nitatabasamu moyoni tukionana wawili fahamu sina mwingine ni wewe pekee

 

(CHORUS)

[Wote]

Aziza mboni ya jicho langu,Aziza njoo uniokoe

 

[DEDE]

Usingizi sipati Mama kwa kukuwaza wewe

Hata kula nashindwa roho imefanya donda

Kitu gani nimefanya mimi 

WATAKA ITOA ROHO YANGU DEDE

Ukinikataa nitakufaa

 

[Wote]

Aziza mboni ya jicho langu,Aziza njoo uniokoe...........

 

Rudi mwanzo

 

[LELI - Bima] 

 (Chorus)

[Wote]

Mtoto muaminifu, mtoto mwenye huruma

Mtoto mwenye heshima LELI sitomuacha

 

[Mmoja]

Tujiepushe LELI na watu wabaya

Tujiepushe LELI na zao fitina

Tusiyashike yao maneno neno

Mungu atujalie LELI tuishi salama

 

[Wote]

Mtoto muaminifu.......  

Rudi mwanzo

 

[BOMU LA SIMANZI - BIMA(DEDE)]

 

[DEDE]

Penzi limegeuka moyoni ...mama eee(x2)

Niliyetaka kuoa kanitoweka

Niliyetaaaaaka kuoa kanitoweka siku ya Harusi

 

Na wakina mama waliokuwa chumbani kwa bi harusi

Wakicheza kwa shangwe, 

Wakijimwaya mwaya kwa furaha aaa wakingojea mimi

 

BOMU la simanzi limepasuka hadharani ee

Nilipoingia ndani nisimkute Salma ee

Tausi wangu miye katoweka

 

(chorus)

[Wote]

Pete ya harusi ilikuwa kitendawili kilichokosa mfumbuzi jamani eee

 

Rudi mwanzo

 

[BUSU PANDE TATU - BIMA]

(Bima Lee, mwaka 1989 kibao kilitungwa na Max Bushoke, kuimbwa

nae pamoja na Jerry Nashon, Athumani Momba, na Bwana Mugunda)

(Bushoke)
vipi penzi lajisuta lenyeweeeeeee

vipi sasa mbona lajisuta lenyewe
ulipokubali kunipenda ah ah
hukulazimishwaa
uliahidi kwa ahadi na viapo pia
uliahidi kwa ahadi na viapo pia
mwanzoni ilikuwa penzi motomoto
busu pande zote tatu za uso ohooooo

(wote)
ukweli nimeuona kwenye hili penzi letu
mwenye pendo la udanganyifu sasa ameonekana
kwenye mapenzi ya kweli
watu hushirikiana sheri
kwenye dhiki na faraja
kote hushirikiana
viko wapi sasa jamae
maneno ulionieleza
NAKUPENDA HAKUNA MWENGINE TENA
KUMBE YOTE NI UONGO

(Nashon)
uko wapi sasa moto wa mapenzi yetu mimi na wewe.. mimi nawe mamaa
uko wapi sasa moto wa mapenzi yetu mimi na wewe
mbona umezimika hata majivu hayaonekani
mamiii mamiiiii

(wote) Kibwagizo
ama ni kweli mapenzi hayana mdhamini
nimeamini
yaweza vunjika wakati wowote

(Nashon)
ama ni kweli mapenzi hayana mdhamini
duniani duniani siku hizi
I love you busu nyingi ........ uongo huo
mamii mamiii

(wote) kibwagizo

(Nashon)
uko wapi sasa moto wa mapenzi yetu mimi na wewe
mbona umezimika hata majivu hayaonekani
mamii mamii

(wote) kibwagizo

Rudi mwanzo

 

[Makulata - BIMA(DEDE)]

 

[Wote]

Eee Makulata mama, halooo Makulata mama

Nakutafuta sikuoni bibi, Katika tarumpeti sikupati yeyeyeyeee

 

[Mmoja]Ni umbali Gani ulipo?

[Wote]Nijulishe, nipigie simu namba 26-56-1

(repeat)

 

[Gerry Nashon]

Wakila eya melakembe, walakembe Makulata

Yalobanzii Makutala e sela mbele ya wazeee

Usifanye mchezo na pendo

[Wote]Nakupenda aaaaaa

[Mmoja]Naapa kwa jina la mama Suzana ee

[Wote]Nakupenda aaaaaa

 

(Chorus)

[Wote]

Popote ulipo nakuhitaji uje unihakikishie mapenzi yetu

Kama kweli tutaoana

Uendelee na tabia yako ya ukarimu (x2)

Tamaa mbali mbali mbali nawe

Pesa mbali mbali nawe........uendeleee........

(Mwisho)

 

Rudi mwanzo

 

[Milionea Wa Mapenzi - Bima]

 

Nikuite nani weweee, 

Nikuite bwana mapenzi jina hilo halikufai,

Nikuite bingwa wa mapenzi  jina hilo halikufai,

Naona bora nikuite milionea wa mapenziii!

 

Umetuweka ndanii

Sisi wanawake watatu

Khanga na vitenge sie kwetu ni sumu

Mchele wa kitumbo kwetu ni alimasi

Nusu kilo ya sukari utaigawa vipi mara tatu ?

 

(chorus)

Mpenzi rejea mama aaaa

Mimi naondoka

Waondoka kwa nini mama?

Huoni nilivyokonda

Wakondeshwa na nini mama aaa?

Shida zimezidi....

 

Kwa heri ee, mpenzi yooyo

Narudi kwa baba na mama walionilea

Sio kama sikupendi, bali ni njaa...

Inayonifanya nikimbie nyumba yako iyele yele

 

Rudi mwanzo

 

[Neema - Bima]

Nimesimama kwenye Mnara wa Bismin

Barabara kuu iendayo Bandari ya Salama

Majonzi yamenijaa machozi yanidondoka

Naiwaza sura ya Neema

Naiwaza sura ya Malaika wangu eeee eee

Nitoe nitoe kizimbani niwe huru ooo niwe huru 

(CHORUS)

Usiniache pweke Neema

Nitasema na nani Mama 

(Nitalia na nani Mama )

Usifuate wasemayo Wafitini

Hao wako mbelembele kuharibu mapenzi yetu mimi nawe

(DUDUMIZI)

Meneno mengi sana nilishasema

Usifuate ya wambea watakuja kutuvurugia

Unayaona sasa yametufika Mpenzi

Tumetengana bado tunapendana

Fanya hima............. 

Usiniache pweke Neema

Nitasema na nani Mama

Usifuate ya wasemayo wafitini

Hao wako mbelembele kuharibu Mapenzi yetu mimi nawe

 (Njemba)

Ulipotamka Adios Amigo

Uliniacha Mama ninateseka Mpenzi

Sina mwingine Neema ooooo 

Sina mwingine mama

Fanya uje ....

 

USINIACHE PWEKE NEEMA...............

[Rudi mwanzo]

 

 

[Radhi Ya Wazazi - Bima]

 

Baba na mama leo yamenifika mlosema ni ya kweli hakika nimetubu

Wanawake wema sana baadhi yao sio wema kazi yao ni uongo

Wamevunja nyumba yangu watoto wangu wapata tabu

Mama yao katoroka kwa hasira ya maneno , maneno ya uongo

(Aa sikia maneno)

 

(repeat)

 

(Chorus)

Baba na mama wamenihusia rafiki wa kike karibu na nyumbani

Vibayaaaa aaaa atazua maneno ya uongo

Hatimayeeee eee kukosana na mke wa nyumbani

 

[Mmoja wao]

Maneno ya wazee yasikilizwe ajisi na dharau mbaaya

Usipoyashika utapata tabu, yatakukuta kama mimi mwenzio

 

(repeat chorus)

 

Rudi mwanzo

 

[Sofi - BIMA]

 

Ndugu marafiki iiii...........

Niweleze uzuri na sifa alizokuwa nazo...... mama yeeeeyeye yooo  Sofi

 

Sura ya Sofi....

Imekuwa pana na fupi

Ana mashavu ya kumiminina mama lelelele yooo Sofi

 

Umbo la Sofi....

Si mnene si mwembamba wa kadri

Ana macho ya gololi mama leelele yooo Sofii

 

(repeat from start)

 

[Wote]

Ndugu rafiki iii

Huo ni uzuri wa Sofi iii

Unaofanya nimpende yeyeyeye

Hata nisiwe na imani

(repeat)

 

(Chorus)

[Wote]

Sofi Sofi nampenda mimi sana aaaa

Sofi Sofi nampenda mimi sana aaaa

 

[Mmoja]

Kwa mavazi jamani Sofi...mwana aaa

Hachukizi asilani Sofi oooo

Sofi Sofi yooo hawezekani mama

 

[Wote]

Sofi Sofi nampenda mimi sana aaaa

Sofi Sofi nampenda mimi sana aaaa

 

[Mmoja]

Akifika shambani Sofi......mwana aa

Kwa majembe begani Sofi...yeye ooooo

Sofi Sofi oo mama...hachoki upesi iii mama

 

[Wote]

Sofi Sofi nampenda mimi sana aaaa

Sofi Sofi nampenda mimi sana aaaa

 

[Mmoja]

Kwa mapishi jamani Sofi....mwana aaa

Akiingia jikoni Sofi....yeye oooo

Sofi Sofi yooo mama ......hawezekani mama

 

[Wote]

Sofi Sofi ..........

Rudi mwanzo

 

[Pendo - Bima] 
  
(Mwimbaji: Cosmas Thobias Chidumule )
 
 
Pendooooo!
 
Pendo umeondoka roho yangu inanyong`onyea aah
Pendooooo
 
Aha aaah, aaah Pendo!
 
 
Ati huwezi kuvaa mitumba bibi Pendo x2
Ati heshima yako,
Itashuka Peeeendo!
 
 
Aaah, aaah, aaaaah Pendo!
 
Mimi mumeo kazi yangu ni kibaruaaaa,
Wa kuponda kokoto hapa mjini ,
Masikini !
 
 
Mimi mumeo,
Ni lofa Pendo,
Mimi Mumeo  
masikini Pendo,
 
Siwezi kuwa Meneja,
Nahuzunika Pendo,
Siwezi kuwa karani ,
Nasikitika Pendo
 
Pendo, pendo, pendo bibi
 
Pendooooo,
Pendo umeondoka roho yangu inanyong`onyea......
 
 
Ulipokuja kwetu kunioa,
Ulisema wewe ni meneja wa benki
 
 
Unajua Pendo,
Mwanamume unapompenda mwanamke,
Uongo lazima uwepo, japo kidogo

Rudi mwanzo

 

[SIRI - BIMA] 
 
Kitendo unachofanya kimefanya nisikuthamini,
Nikuelewe vibaya aaah,
Ni mengi unayofanya moyoni unajidanganya,
kwamba unafanya siri eeh,X2
 
 
Siku nyingi nilisikia,
Watu wengi wakikusimulia,
Habari zako wewe mitaani zimeenea,X2
 
 
Kibwagizo:
 
Siri yako ni yako eeeh  
[eeh siri] x2
Akishiriki mwingine si siri tena
 
Wengi hujidanganya kwa kufanya siri, [sema]
Na huku wakinenaaa,
Utadhani kasuku,
Watu huipata wakaitangaza,
Nao wakijua ,
Hupati kujua, hivyo oooh siri si siri tena!
 
 
Siri yako ni yako eeh

Rudi mwanzo

 

[Nanawa Mikono - BIMA] - Uzegeni


(Utunzi wake Shaaban Dede (super tingisha) solo hapo linapigwa na Joseph Mulenga 

wakati huo walihama pamoja DDC na kujiunga na wana Bima.)

(Dede) 
nanawa mikono 
naupumzisha moyo wangu 
labda jeraha linalonisumbua laweza kuwa nafuu 
jerahaaa jerahaaa sitokuwaza tenaaaa 

sikutarajia kashfa ohh kutoka kwako ohh ya wewe kunisifia ujinga X 2 
ninapotaka tukutane mamaa 
wewe utoke kila mimi nikuonapo hubabaika 
na kujisachi nilichonacho bila wewe kuniomba 

(wote) 
nanawa mikono eheee 
ahadi zako zimenichosha 

(wote) kibwagizo 
anayejua mapenzi hawezi kunilaumu 
mimi kukupa nilichonacho 
nilipokuwa nakupenda X 2 

(Dede) 
fedha nikitoa ni zawadi eh .... ni zawadi 
japo penzi ni maelewano 
mkono mtupu haulambwi 
yoyo weeeeeeee ..... jamani ehe eh 

(wote) kibwagizo 

(Dede) 
ukiwa kimwaagaaa unaitwa bwege 
ukibana matumizi unaitwa mkono wa korosho mama ohh 
lipi la farajaaa ah kwenu wanadamuu 

(wote) kibwagizo 

Rudi mwanzo

 

[MESENJA KALETA BALAA - BIMA] - Uzegeni

(Bushoke) 
Wee Mesenjaaaaaaaaaa 
halo sekretari ...... eh be 
eheee Mesenja yuko wapi ...... sijui bosi 
mara mesenja anaibuka na kusema ..... 
naam bos nilikuwa uani tumbo linaniletea matatizo mie 
eee bosi akasema nenda posta ofisi kachukue barua za ofisini na zanyumbani 
za ofisini lete ofisini na za nyumbani peleka nyumbani 

Mesenja kaleta balaa nyumbani kwa meneja bila kufahamuuuuu uhuu 

(wote) 
Mesenja kaleta balaaa nyumbani kwa meneja bila kufahamuu uhuuu 

(Bushoke) 
wakati anatoka posta ofisi anawaza moyoni 
mzee mie darasa la tatu la mkoloni 
mke wangu na wanangu wamelalia ugali wa muhogo na chunga la kuchemsha jana 
akaingia Kariakooo anaikimbiza mia wakati siku hizi mia imeota matairi 
kutoka posta ofisi akakuta ofisi imefungwa 
na mlango yupo mlinzi 
akajaribuuu kumbembeleza apokee zile barua akakataa 
akazipeleka nyumbani kwa bosi wake akamkuta mkewe 
mke wa bosi akabidi azichambue kwa kuwa si desturi barua za ofisini kufika nyumbaniii 

siiri imefichuka siriiiii imefichuka 
kosa la mesenja kaleta balaa 
kosa la mesenja kaleta aibuuu 

(wote) 
siiri imefichuka siiri imefichuka 
kosa la mesenja kaleta balaa 
kosa lamesenja kaleta aibuuuuuuu X 2 

akaanza kuzichambua 
kachukua ya kwanza kaweka kando 
kachukua nyengine kaweka kando 
kuchukua nyengine akaona mwandiko umelalia kushoto 
hati kama ya kike 
akaifungua kichwa cha habari haloo darling 
akazimia nusu saa masikini 

siiri imefichuka siiri imefichuka 
kosa la mesenja kaleta balaa 
kosa la mesenja kaleta aibuuu 

alipozinduka kamkuta mwanae mdogo amemuegemea 
anasema mama nasikia njaaaa 

mimi sipiki akija baba yako mwambie aje apike 
kuna anawajengea majumba na kuwanunulia magarii 

mimi nimekosa nini jamaaaa 

aliporudi bosi anagonga mlango akaambiwa 
akalalte huko huko kwa anaowajengea majumba na kuwanunulia magari 
akabembeleza akfunguliwa mlango 
ile kuingia ndani zogo kubwa likaanza 
mara maneno mara kavuliwa koti 
mara kachaniwa shati 
mesenja kaleta aibu jamaaa 

(wote) 
siiri imefichuka siiri imefichuka 
kosa la mesenja kaleta balaa 
kosa la mesenja kaleta aibuuuuu X 2 

 

Rudi mwanzo