Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]    Rudi Table

 

 

[Naapa Sitopenda - Bendi]

 

Naapa sitopenda,

Mwingine tena,

Kukukosa wewe,

Mwingine sitopenda,

Umeniacha pekee,

Hali yangu mbaya,

Kukukosa dada Mwajuma,

Aheri ya kufa.

 

Kibwagizo: 

 

Ingawa umenitupa,

bila sasa yoyote,

......

Ufike nyumbani kwangu,

Ili tuyajadili , tuyamalize mpenzi!!

 

 

Naapa sitopenda .....

 

Rudi mwanzo

 

[It Can Be Done - Bendi]


Nyerere kasema.....
[Wote]
It can be done, play your part

[Mmoja]
iyele iyele
Mwalimu kasema

[Wote]
It can be done, play your part.........

Rudi mwanzo

   

 

[Watoka wapi - Bendi]


Kila siku mi silali nakuwaza wewe,
Mtoto mzuri ninayekupenda sana,
Niambie kule kwenu we unakotoka,
Niweze kufika niwaone wazee wako,
Niwafahamuuuuuu, x2

Kibwagizo:

Nakuomba nambie kwenu ni wapiii,
Nije niwaone wazazi wakooo,
Hata kwa ndege mimi nitafikaaa,
Nione kwenu unakotoka kwa wazazi wako,
Niwafahamuuu, x2

Nakuomba nambie kwenu ni wapiii,
Nije niwaone wazazi wakooo,
Hata kwa ndege mimi nitafikaa,
Nifanye nini na wewe,
Nambie kweliiii,
Watoka wapiiii??x2

Rudi mwanzo

   

 

[Unknown - Bendi]  

 

{Kiitikio}

Dada safina sogea kwanza nikupashe habari

Leo ni week end nilitembea kumbunga

Na vijana wa kimbunga

Walinifuraisha sana 

Kwa muziki wao x2

 

{Kiongozi }Nilimwona Athumani Hamisi akipiga solo

Juma na Mtwango, wakipa ridhimu.

 

{Kiitikio}

Rudi mwanzo

 

[MARIAM - Bendi]

 

Poa Mariam eeeh, tuelewane vizuri eeh,

Umeamua tupendane uwe wangu wa maisha,

Usije ukabadilika kuwa na tamaa nyingi,

Usione wale wanaong`aa kuwa wana raha mama eeh,

Shida wanazozipata wewe hutovumilia mamaeeeh, x2 

 

 

Kibwagizo:

 

Mariam wangu eeh,

vitenge nitanunua,

Aina za khanga zote utapata eeh,

Nyumba niliyojenga urithi wakoo Mariam x2

Rudi mwanzo

 

 

[Laiti Moyo - Bendi]

 

(Chorus)

[Wote]Laiti moyo ungekuwa aaa

[Mmoja]Laiti moyo kaka

 

[Wote]

Una kifuniko radhi nikuambie eee

Tizama uone unavyokereketa mama aa

 

Lakini yote yamekuwa bure mama aa

Nangoja niuguze kidonda cha moyoni eeee

Nifanye nini utambue nakupenda?

 

[Mmoja]

Moyo ukishapenda kuuzuwia ni shida

Nifanye nini mama utambue ee nakupenda aaa

 

[Wote]Laiti moyo ungekuwa aaa..........

 

Rudi mwanzo

 

[Ingekuwa Hatari - Bendi]

(Chorus)

........kama ukifika mwambie ajirekebishe

Mambo kama yale mabaya na yana hatari

 

[Mmoja wao]

Kusema kweli si vibaya na wala si dhambi

Ya nini kunificha na kunidanganya

 

(repeat chorus)

 

[Mmoja wao tena]

Vurugu nyingi nyumbani (sina hakika hapa) panga mkononi

Na kama nisingeruka ukuta ingekuwa hatari

(repeat chorus)

Rudi mwanzo

 

[Mawazo - Bendi]

Nilitembea jijini Daresalama nikakutana na binti mmoja,

Nikamweleza ninavyompenda,

Na yeye akasema amekubali,

Kisha yake akanipa ahadi,

Nniende kwake nikamtembelee,

Kesho yake niliamka mapema ili nipate kuwahi ile ahadi yangu,

Asije kwamba akanielewa,

Pengine mimi nna ahadi za kiswahili

        

  Nilipo fika nyumbani kwake ee ee,

  Niliyakuta makundi ya watu jamani ee ee

  Wakanambia Hadia amefariki usiku wa jana kuamkia leo, 

Mawazooo, mawazooo jamaniee

 Mawazo,

Mawazoo,

Mawazooo,

[Rudi mwanzo]

[Sakina - Bendi]

Wezee wangu nataka kuwaadithia

Mkasa wa mtoto wenu x2

Nilikuwa pale mjini leo

nilikuwa karibu na baa moja X2

Sakina kweli hatosoma tena, 

maishani mwake wazee wangu  chorus

Majira ya saa tatu ya usiku

nilimwona sakina amelewa sana 

na uso wake umevimba sana.

Sakina kweli hatosoma tena, 

maishani mwake wazee wangu  chorus

Amevaa shati la ndege

na sketi ya shule

na raba za nga'mbo

 Repeat chorus

[Rudi mwanzo]

[Wabaya Ni Hao Hao Bendi]

unakula nao nawabaya ni hao hao

unacheza nao nawabaya ni hao hao  

unasema nao nawabaya ni hao hao

[Rudi mwanzo]

 

[Lisa Bendi]

nimekuwa nikiangaika sehemu zote za hatari kukutafuta wewe Lisa

Naomba nisikie kilio changu mpenzi Lisa

Penzi ulilonipa Mpenzi lisa bado ni kumbukumbu kwangu

Nimekuwa nikiwaza nakuona dunia si yangu ni yawezangu mpenzi lisa.

Jaribu kuniambia nilichokufanyia mpenzi lisa  

Nasikitika kuona niko mbali na wewe mpenzi lisa

[Rudi mwanzo]

[Nyimbo Bendi]

Jumamosi jioni, alinijalia

Nilitoka Hospitali salama na mtoto wa kiume.......tena

Afya njema, bila matatizo

 

(Halafu kipande cha pili hiki)

[Wote]

Kama ni mtoto hata mimi nampenda

Ila uwezo sina....ewe bwana

Mola ndie mpangaji wa hayo yote

Kama kupata au kukosa

 

[Mmoja (TX William)?]

Nashangaa sana mimi kwangu kuwa Kioja

Mbona ni wengi......wengi sana

Wasiozaa aaa, na yote hiyo ni kazi yake Mola

Mimi siwezi bora niende zangu aaa  

[Wote]Kama ni mtoto......

 

[Rudi mwanzo]

 

[Mama Vicky - Bendi]

mama vicky kwa jina la mwanao mimi nakuita,  

kama kuna kosa nililokukosea,watoto wanakulilia..aaa  

wazazi wanakuuliza...aaa,hutamani kuwasaidia  mimi ninashindwa lakufanya sina.......

 

Rudi mwanzo

 

[Kifuko Cha Zambarau - Bendi]

 

Mtoto Jack eeeh! mpenzi wangu, najaribu kukusahau lakini nashindwa

Hasa ni kwa ile ndoto, niliyokuotea, nimeota umeniletea kifuko cha zambarau

Ndani yake kuna ..................................

 

Rudi mwanzo

[Unknown3 - Bendi]  
.........
.......
Nimeona boraa,
Nikueleze eeh,
  
Kwa maana kaka aaah,  
Ni taabu nyingi nimezipata kwakooo,
Na hukusikia mimi,
Ninasema kitu!

Kibwagizo:
Kaka eeeh,  
Usidhani nimeshindwa,
Kuachana nawe, mimi sikundindwa,
Nido maana mpaka leo siko nawe 

Rudi mwanzo

[Unknown4 - Bendi]

Ni lazima ujue kuogelea,
Pia na kupiga mbizi ndugu yangu eeh,
usishangae changu kujitolea,
Kwa chuchunge na mkizi ,
Ni kawaida  
 
Wewe bwana wewe
 
 
Wacha ndugu yangu wacha,
Uvuvi wewe hutouweza [hutouweza]x2
 
 
Kuna kukwepa miamba ,
Na hata zile pepo kali za kusiiiii,
utaupata muhali,
Upoteze maisha ,
Utuachie simanzi
 
Wewe bwana wewe
 
 
Wacha ndugu yangu wacha,
Uvuvi wewe hutouweza....

Rudi mwanzo

 

[Upepo Mkali - Bendi]
Chunga nguo zako Kaka na Dada
Zisipeperushwe na upepo mkali......sana
Chunga nguo zako.......

Rudi mwanzo

 

[TABU - Bendi] - Uzegeni

(Buchuka)
ni wewe kipenzi nikupendae
kwa jina unaitwa Tabu
mwenye sura nzuri ya kupendeza
tabia na heshima yako ni ya kusifika eh
japokuwa maana ya jina lako ni matatizo
kwangu lina maana ya furaha na faraja
 
ninalokuomba jihadhari na walimwengu
usione wakikuchekea ukaona ni marafiki na siri ya penzi letu ukawaeleza
watafanya kila njia waone tumetengana
kumbe penzi letu linawasibu moyoni
tafadhali chunga penzi letu kama benki inavyochunga fedha
 
(wote) kibwagizo
nakuapia watatuona  
 
(Bichuka)
uliyoyasema mimi nimeyasikia
 
(Wote) kibwagizo
 
(Bichuka)
kiapo chetu kiwe cha kweli mpenziiii
 
(wote) kibwagizo
 
(rudia kuanzia kibwagizo cha kwanza)

Rudi mwanzo

 
[Nifanyeje - Bendi] - tizedboy
 
Nikae chini nilie ee
kucheka sina mbavu mama ee
Baba wa Mwanangu kaingia Gerezani  
Nifanyeje?

Rudi mwanzo


[Nyimbo01 - Bendi] tizedboy


Huku sitaki na kule nataka
Kule hanitaki na huku hanitaki tena
 
Kule a sitaki na huku nataka
Huku hanitaki na kule hanitaki tena.....

Rudi mwanzo

[Nyimbo02 - Bendi] tizedboy


Mchezo huo uwache Hassani nakuambia
Utapoteza maisha yako Hassani jihadhari 

Rudi mwanzo

 

[Ujamaa - Bendi] - tizedboy
 
Hata baba yangu alinihusia
Ewe mwana mpotevu dunia hii itakulemea
Nenda kajiunge na wenzio
Katika kijiji cha ujamaa
 
Heri na fanaka hutokana na Ujamaa

Rudi mwanzo

 

[Sitorudia Tena - Bendi] tizedboy

Yamekwisha sifanyi makosa kama yale kaka
Kama yale.......
Mpenzi nisamehe sitorudia tena

Rudi mwanzo

[Masudi - Bendi] - tizedboy
 
O mama najuta e
O mama nifanye nini
Mama mabo yamenikuta....mwenzenu
Yamenikuta
 
[Mmoja]
Maneno mengi nilikwishakwambia
Nawe ukayapuuza
Mama......
 
Naondoka.....Masudi...naondoka mama....
 
O mama najuta e.........

Rudi mwanzo

 

[Chande Jirekebishe - Bendi]  - tizedboy

(......) 
Juzi juzi nilikukuta 
Wamteta mke wangu uu Chande 
Kuwa sisi ni-wachafu 

Nakuomba Chande 
Nakuomba ndugu jirekebishe 
(.........) 

Rudi mwanzo