Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

Mwanzo    Rudi Table

[Mwenzio Naumia - Kilwa Jazz Band]  - Mtukwao


Napenda nipate lau nafasi, 
Niweze kusema nawe kidogo aaah mama aah, 

[Mwenzio naumia] 
Aaah mama aaah 
Mwenzio nateseka. 
[Aaah mama aaah] 


Hakika kuja kwako wewe wangu mpenzi, 
Ni kama mganga utayenitibu, 
Katika maradhi yanayonisibu, 
Hakuna mwingine ila ni wewe , 
Mpenzi fanya uje, 

Hakuna mwingine ila ni wewe, 
Mpenzi uje hima, 

Mwenzio naumia, 
[Aaah mama aaah] 
Mwenzio nateseka 
[Aaah mama aaah] 


Hakika la kufanya bado sijaliona, 
Nimeona bora leo nikuite, 
Huenda siku roho yako ikadunda, 
Ikaja siku ukaja nipoza moyo,oooh mama aaah 

Moyoni naumia, 
[Aaah mama aaah] 
Mwenzio nateseka, 
[Aaaah ,mama aah] 

 


[MANENO NI SUMU - Djakaba Stars]
 

Yanisikitisha moyoni mwenzangu,
Ona ninavyokonda mie eeeh,
Kuniwekea azimio sipendi,
Mimi na wewe tutengane, x2


Umesikia ya watu,
Watu wenye minong`ono pembeni,
Kazi yao ni kukaa barazani eeeh,
Na kuuza maneno x2


Kibwagizo:

Hawafanyi haraka uamuzi,
Huchunguza kwanza eeeh kwanza,
Illi wapate hakika ya maneno,
Maneno ni sumu x2

 

[Rudi mwanzo]


 

[PAMELLA - Simba Wa Nyika]

Nasikia waniita lakini Mama uningoje
Kwani najua unachokitaka Pamella x2

Lakini kazi zimezidi Mama ooo
Nikimaliza ntakuja nikuone Mama
Nikupe busu Mama Pamella

Kwani apendae ndiye mwenye kujua
Tabu na raha yote ya Mapenzi Mama

Kwa hiyo Pamella ukinipenda Mama
Nami kesho nitakupa mapenzi Mama

Kwa hiyo Pamella oo maliza masomo Mama
Yakiisha uje tuoane Mama

Uje tuoane yo yo yo
Uje tuoane Mama
Uje tuoane kijana
Uje tuoane Mama

 

[Rudi mwanzo]


 

[Maneno Sipendelei - Afrisa International] 

( Wana munisandesa )
  
Na maneno sipendelei,
Kusemwasemwa sikuzoea,
Mtanikondesha bure ,
Mie mwenzenu mama eeh x2
 
Nikipita mwaninyoshea vidole eeh mama,
Kisa hicho kisa sijakijua  
 
Kisa eeeh mama, kisa sijakijua
 
Kisa hicho kisa sijakijua.
 
 
Kibwagizo:
 
Oooh mama niacheni mie na maisha yangu,
Jamani eehe sijala cha mtu mie mwana wa mama eeh,
 
Ooooh mama niacheni mie na maisha yangu,
 
Ya kwenu yanawashinda, ya wenzenu midomo juu,
 
Oooh mama niacheni mie na maisha yangu


[Rudi mwanzo]

 

[Mwaka Wa Huzuni - Kepteni Komba] 

 

Ni mwaka wa matatizo, ni mwaka wa huzuni
Kwetu WaTanzania wote
Kamwe hatutamuona tena!

 

[Rudi mwanzo]

 

[Lilikuwa Jambo Dogo - King Kiki Double O] 
 

(Wana Embalasasa ,Muimbaji : Nana Njige. )
 
 
Lilikuwa jambo,
Lilikuwa jambo dogo tu mama x2
 
La mimi na wewe kuelewana eeeh  
La mimi na wewe kueleana eeh mama aaah Tabea,
 
Angalia sasa,
Angalia sasa wameshapeleka, x2  
 
Mitaani kote zimeshaenea eeeh mama,
Mitaani kote zimeshaenea eeh mama aah Tabea,
 
Kibwagizo:
 
Yame tubayai yoooyoo Tabea!
 
Hata kama tutarudiana tena eeeh mama,
Imeshakuwa ni aibu kubwa eeh mama,
Iliyobaki tupeane hali yee mama,
Iliyobaki tuangalie maendeleo ya mtoto wetuuuu Tabea 

[Rudi mwanzo]

 

[EEE MASIKINI - Jamhuri Jazz Band] - Chef

Eee Masikini
Mimi nina balaa sana
Tabu ni nyingi
Zinazonikaabili mie
Nitafanya nini oooh
Duniani hii
Niwe na maisha  
Kama wenzangu
 
   Chorus:  
   Nitafanya nini eeh
   Maisha yananiendea vibaya mie
   Kila ninalofanya mie ooh  
   Mauti yangu yangojewa kwa raha mie
   Hakuna wema duniani eeh
   Iliyobadi tumuombe Manani  (Tuwe Salama)
 
 
 
[Adelina - Jamhuri Jazz Band] - Mtukwao
 
Adelinaaaaa,
Aaadelinaaa,
Adelina mamaaaah,
Nakutolea asante unavyonitendea mema Adelina!
 
Nakumbuka,
Nawaza sana,
Nakufikiria aaaah,
Ukibadili nia nitaumia milele, Adelina!

 

[Salaam Za Wagonjwa - Salum Abdallah] - Mtukwao

 

Wakati umewadia wa salam za wagonjwa hospitalini leo tunawapa pole,
Ajuaye Bwana Mungu kwa mzima kuwa mfu,
mgonjwa kuwa salama leo tunawapa pole
 
 
Wote twawapeni,
Kipindi chenu chawapeni pole,
Mola atawajalieni mponex2

 

 

[Wenzako - Jamhuri Jazz Band] - Ngosha

 

Ni nini Mama unalia oooo
Unalizwa nini
Mimi ni wako wa zamani ooo mwenzangu shaka ondoa
 
Ninapokuaga matata hayaishi nifanye nini sasa
Mwenzangu wanitafuta lawama mbaya mimi mwenzio
 
Chorus
 
Wasiwasi kwangu ondoa jiepushe na majirani
Mimi ni wako ooo
 
Wenzako wanaona wivu
Tunavyoishi mimi nawe
Mimi ni wako oo usife moyo
 


[Jirani - Lovy Longomba] - tizedboy


kisa cha ugomvi mimi na wewe jirani
Ni kumukashifu bibi yangu bila sababu
Nneno uloingilia......
Halukuhusu wewe
Pilipili Shambani yakuwashia nini?
 
Mke wa mwenzio umupe zake heshima aa
Ulivyo na wako nami ndivyo nilivyo na wangu ee
Tupendane tuheshimiane kama ndugu
Ya nini ii kukorofishana?

 
 
[Paulina - Les Wanyika] - tizedboy


Paulina mama
Shemeji naleta mashitaka
Sielewi lengo la nduguyo oo
Vibaya sana mama aaa
 
Naona imani yake ee....
Ni ndogo kwangu mama

 


  
[Cicily - Kenyan Band] tizedboy


[Wote]
Cicily mama yeye......o mama
Cicily mwanangu e mpenzi
Mpenzi wangu a mi nakupenda
Mimi nawe pamoja nawe e Motema
 
[Mmoja]
Nakulia mama Cicily
Nakupenda e mpenzi o Cicily
Nimekwenda Mombasa sijamwona Cicily
Nimerudi NAKURU sijamwona Cicily e mama...
 
[Wote]
Cicily mama yeye......o mama

 

 
[NIPE UKWELI WAKO - MK (Beats/Group)] - Mtukwao

 
(Muimbaji: Kasongo Mpinda Clayton )
 
 
Eee bwana eeeh,
Tuliza roho yako ongea ukweli wako,
Ondoa wasiwasi bwana aah,
 
 
Naona mapenzi yakuzidia iyoo,
Hata midomo yatetemeka iyoooo,
Naona mwenzangu waumia eeh x2
 
 
Naona mwenzangu una neno kwaaangu,
Hata kuongea huwezi tena wakwetu,
Basi andika hata kwenye barua,
Au mtume rafiki yako,
Anieleze shida yako iyooox2
 
 
Kibwagizo:
 
Ni uzuri wako wanibabaisha mtoto wa mama,
mtoto wa mama aaah Ngalamba,
 
Napata kigugumizi cha ukubwa,
Mtoto wa mama, mtoto wa mama aaah Ngalamba
 
 
Naomba usiondoke mama yoyo,
Mtoto wa mama, mtoto wa mama aaah Ngalamba
 
 
Naomba unikubalie mwana kwetu,
Mtoto wa mama, mtoto wa mama aaah Ngalamba
 
 
Hakika nakupenda sina ujanja,
Mtoto wa mama, mtoto wa mama aaah Ngalamba
 
 
Ngulupa, ngulupa , tupatupa eeeeh

 


[Tumuombe Mungu - MK(Beats/Group)] - tizedboy


Tupige magoti tumwombe Mungu bwana
Atuondolee ugonjwa huu
Ugonjwa huu ambao hauna kinga

 


[Blandina - Jamhuri Jazz Band] - Mtukwao
 
Ooooh Blandina,
Ulivyofanya wala si vema dada,
Kuondokaaaa,bila kuniarifu,
Kuniachia masikitiko,
Na mawazooooo, hayaishi moyonix2
 
Kibwagizo:
 
Makosa yote ni yako dada,
Na ubayaaaaa,
Wafanya wewe
 
Kuniachaaa peke yangu,
Na mawazoooo,
Hayaniishi
 
Anza weweeee,
Mimi namalizaaa,
Bora tusielewane vibaya

 

 

[Embakassy - Les Mangelepa ] - tizedboy

Embakassy ninakwenda oo moyo
Natizama juu chini ee Mola aa
 
Ngai na kei  
Ngai na miso ya kolela yo Embakassy
Embakassy iii


[Sina Makosa - Les Wanyika] - tizedboy
 
Huyu ni wangu yule ni wako
Chuki ya nini kati yangu
Mimi na wewe
 
Nasema.....Sina Makosa eee bwana aa
 
Wewe una wako nyumbani nami nina wangu nyumbani
Chuki ya nini kati yangu mimi na wewe
 
 
Nasema........

 

 
[KADIRI KANSIMBA - Sambulumaa] - Ngosha
 
Uaminifu wa mapendo eee naonekana mjinga
Kadiri Kansimba naonekana mjinga
 
Nilikutimizia mahitaji yako ee ooo Mama
Nilikulindia heshima yako ee oo ee Mama
 
Wo wo wo nikupe nini sasa we Mama
Wo wo wo nifanye nini sasa wee Mama
Wo wo wo sasa tuko wapi ee Mama
Kadiri Kansimba unieleze ukweli wako Mama x2
 
Mara ya kwanza nimekuona nikakusamehe
Mara ya pili tena umenidanganya eti Mjomba wako
 
Wo wo wo Kadiri tumetoka mbali mimi na wewe
Wo wowo nikupe nini sasa we mama
Nifanye nini sasa we mama
wowowow sasa tuko wapi ee Mama
Kadiri Kansimba unieleze ukweli wako Mama
Kadiri Kansimba naonekana mjinga
 
[Kipacha]
Uaminifu wangu kwako Mama naonekana Mjinga
Nifanye nini sasa cherie sema nijue Mama
Nikupe nini sasa mimi sema nijue Mama
Kadiri Kansimba naonekana Mjinga
Kadiri kansimba hayo si maisha
 
Iringa CHUNYA Mwanza kote nimefika
Nifanye nini mimi sasa mapenzi yangu kwako ni bure
Nikupe nini sasa Mama Mapenzi yangu kwako ni bure
wowowwo sasa tuko wapi ee Mama
Kadiri Kansimba naonekana mjinga

[ASHURA - Magereza Jazz Band] 
 
 
Ashura mimi najuta,
Mwenzenu kweli najuta sasa,
 
Visa ninavyofanyiwa na bwana huyu [Bwana huyu]
Nimeamini methali isemwayo [isemwayo]
Mkataa pema,  
Oooh, pabaya panamwita x2
 
Leo hii mwenzenu ,
Kusema hivi mimi,
Nilimuacha mume wangu,nilidanganyika,
Kumuacha mume wangu, kumfuata bwana mwingine,
Kumbe ni mwizi baba, kumbe ni muongo.
 
Visa ninavyofanyiwa......
 
 
Kibwagizo:
 
Nawausia wanawake wenzangu wote eeh,
Muheshimu ndoa zenu zisijevunjika x2
 
 
Muachane na mabwana wadanganyifu eeeh,
Atakupenda wakati una mumeo ooh,
Ukishaachika wala hana habari nawe
[Hana habari nawe]
 
Atakudanganya kwa curl na relaxer,
Atakudanyanya kwa khanga za Mombasa,
Atakudanganya kwa vitende vya Zaire,  
Atakudanganya kwa chips na mayai,
Na starehe za muda hazina mwisho sikia
 
Nawausia wanawake.....

 

[Rudi mwanzo]


[SIKUJUA KAMA UTABADILIKA - SIMBA WA NYIKA] - Ngosha

Oh oh oh oh sikujua kama utabadilika x2
Najuta kupoteza wakati wangu nyumbani kwako
Baki salama kuonana nawe ni majaliwa
Oh oh oh oh ulimwengu kweli una mambo mengi
 
  [Rudia]
 
Chorus
oh oh samahani Baba Oh oh nimetosheka na maovu yako
 
Oh oh sikujua kama Oh oh ya kwamba Baba utabadilika
 
Cherie
Cherie  
 
Utakuja nitafuta Mashariki na Magharibi
Utakujalia kisha Baba usinione
 
Mbona matata wee
Mbona matata wee
Mbona matata wee
Mbona matatizo
 
Utalia utalia usinione
 
Mombasa mbali
Kisumu mbali
Kakamega mbali
Kisii mbali
Kendu Bay mbali
 
Mwanagu utatembea utatembea usinione
Utalia utalia usinione
 
Uganda mbali
Tanzania mbali
Europa mbali
 
Mwanagu utatembea utatembea usinione
Utalia utalia usinione
 
Mbona matatizo wee
 

[MALAIKA - Mbongo] - tizedboy

 
Malaika nakupenda Malaika(x2)  
Nami nifanyeje  
kijana mwenzio  
Nashindwa na Mali sina aaa  
Ningekuowa Malaika  
 
Kidege eee  
Wasumbua Roho yangu  
(repeat)  
 
Ningekuowa Mwali e  
Ningekuowa Dada  
nashindwa na mali sina eee  
NINGEKUOWA KIDEGE  

 

[Magomeni - Police Jazz Band] - mtukwao
 
Kumbe kuna bwana wako,
Mimi wanidanganya wenda Josephina kwa bibi yako,
Nimeshapata habari zako huko Magomeni dada Josephina x2
 
Kibwagizo:
 
Huko Magomeni unakokwenda,
Una bwana wako, taxi dereva,
Tena siku hizi ninakuona,
Hata tabia zako zimebadilika,
 
Wewe siku hizi umepata mwalimu,
Anayekufundisha, tabia mbaya,
Lakini waonaje , hayo maisha,
Ya mwalimu wako yalivyo mabaya!x2

 

 

[Shauri Yako - Super Mazembe] - tizedboy
 
Nilikueleza yaka we mama Fatu wangu mama
Mapenzi ya kwetu ee haitagawiana mama
Tabia yako na yangu haisikilizani eee
Unaona unaona sasa we mama(x2)
 
Unapenda kuvaa mimi sina namna mama
Unapenda kula vizuri mimi sina PESA o Fatu ee
Niibe Mali Sizoweye watanifunga
Niue mtu nipate dawa ya fedha
 
Niue mutu watanifunga  
Niue mutu Dhambi kwa Mungu
 
Shauri yako, shauri yako ee(x2)
Shauri yako wende lote Sena wangu
Siwezi kuuwa mutu mama
Dhambi kwa Mungu mamaye
 

 

[Mwenzio - Kilwa Jazz Band] - Mtukwao 
 
Napenda nipate lau nafasi,
Niweze kusema nawe kidogo aaah mama aah,
 
[Mwenzio naumia]
Aaah mama aaah
Mwenzio nateseka.
[Aaah mama aaah]
 
 
Hakika kuja kwako wewe wangu mpenzi,
Ni kama mganga utayenitibu,  
Katika maradhi yanayonisibu,
Hakuna mwingine ila ni wewe ,
Mpenzi fanya uje,
 
Hakuna mwingine ila ni wewe,
Mpenzi uje hima,
 
Mwenzio naumia,
[Aaah mama aaah]
Mwenzio nateseka
[Aaah mama aaah]
 
 
Hakika la kufanya bado sijaliona,
Nimeona bora leo nikuite,
Huenda siku roho yako ikadunda,
Ikaja siku ukaja nipoza moyo,oooh mama aaah
 
Moyoni naumia,
[Aaah mama aaah]
Mwenzio nateseka,
[Aaaah ,mama aah]  

 

[Unalewa Bila Kipimo - Polisi Jazz Band]  - Carbon14


Ulipokuwa shamba 
Ulikuwa mtulivu 
Kufika jiji la Darisalama umekuwa mlevi sana 

 

(Chorus) 
[Wote] 
Unalewa bila kipimo hata Watoto huwakumbuki.....huwakumbuki 
Nguo zimekwisha na wewe hata hujali 

[Mmoja] 
Hujali hata Bwana ee ooo hujali 

[Wote] 
Unalewa bila kipimo hata Watoto ..... [PamelaII - Les Wa Nyika]  - tizedboy

(......) 

(Chorus) 

[Wote] 
Jambo la muhimu 
Nakuomba Mama we 
Twende kwa wazazi nyumbani.....wakatuone 

[Mmoja] 
Wandugu zako wote nimeshawaona ee 
Waliobaki Wazazi wako Pamela ee aaa 

[Wote] 
Jambo la muhimu 
Nakuomba Mama we 
Twende kwa wazazi nyumbani.....wakatuone 

[Mmoja tena] 
Maneno ya busara kutoka kwa wazazi 
Nimeyapata na Dua njema Pamela ee aaa 

[Wote] 
Jambo la muhimu 
Nakuomba Mama we 
Twende kwa wazazi nyumbani.....wakatuone

 

[Edina - Magereza Jazz Band] - Uzegeni

karibu ndani karibu 
mchumba wangu Edina njooo x 2 

wala usiwe na wasiwasi 
mimi bado sijaoa 
usirudie mlangoni tu, hapa ni kwakoo 
karibuuuuuuuu 

(rudia mwanzo) 

(wote) Kibwagizo 
nakutegemea tuishi vyema kipenzi eh 
nakutegemea tuishi vyema Edina 
kwani silaha ya upendo ni tabia njema ahh mama X 2 

sina bibi wala mke Edina ahh 
wewe ni shada la ua ua 
pokea penzi langu kwa mikono miwili 
Edina chaguo langu mimi 

(wote) kibwagizo 

sina bibi wala mke Edina ahhh 
wewe ni shada la ua la upendo 
pokea penzi langu kwa mikono miwili 
Edina chaguo langu mimi 

(wote) kibwagizo

 

[MADO - ATOMIC JAZZ(John Kijiko)] - Ngosha

Mado Mpenzi wangu usiivunje ahadi 
Nilikupenda ungali mdogo 
Na hivi sasa umekua 

Fanya haraka Mado umalize masomo yako 
Tukamilishe ahadi yetu tuishi sote kwa raha 

Chorus 
oo Mado oo oo ooo Mado 
Nakungojea mwenzio 
Mimi sitaki mwingine oo oo 
Ni wewe Mado wangu