Site hosted by Angelfire.com: Build your free website today!

[Mwanzo]    Rudi Table

[DIRISHANI - Afro 70 Band]

Nasimama dirishani oooh,

Naona mvua inanyesha,

Hakuna kilichobakia ooh,

Ila ni huzuni na uchungu tele,

Nakutafuta mpenzi unipoze moyoooo,

Lakini hakuna mtu wa kunipoza x2

 

Naomba urudi mpenzi wa roho,

Mimi mwenzio nakufa kwa upweke,

Ili tukionana tuoaneeee

Mpenzi nauliza utarudi lini   

Mateso yanitoke nifurahi nawe mpenzi

[Rudi mwanzo]

[Kuoana Jambo La Sifa -  Afro 70 Band] 
 
Kuoana ni jambo la sifa,
Kwa watu wawili waliopendana mpaka kifo kije kuwatenganisha,
Awali ya yote,
Kaeni na amani nawausia mpaka kije kuwatenganisha.
 
 
Kibwagizo:  
 
Kuweni na moyo wa mapenzi kwa kila mtu,
Mtaheshimiwa,
Mzaapo watoto wenu muwatunze vema,
Wawe na adabu,
Tena muwe wacheshi kwa kila mtu,
Ni sifa kubwa
Ukarimu kwa wazazi wenu wa pande zote,
Ni heshima kubwa.

Rudi mwanzo

[Nuru Yangu - Afro 70 BAND(Patrick Balisidya)]

Uweee karibu namiiii

Niukumbatie mwili wakoo

Wewe nikupendae 

 

Umbo lako mpenzi lanivutiaaaaaaaaa

Kwani u nuru yanguuuu

Ikiwa nitajaribu kukuacha,,

Nitaidhuru roho yanguuuu

Kwa vile nakupendaaaaaaaaaa 

 Penzi nililonaloooo

Halijapata kutokea mamaaaaaa

Kamwe sitajizuiaaa

Niwe nawe popote niendakooooooo

 Kwa vilee, nakupenda 

Wala kamwe sitakuacha mamaaaa

Kwani u nuru yanguuuu,

Ikiwa nitajaribu kukuacha.......

[Rudi mwanzo]